Dr. Shein naye ameanza "usanii"?

Brooklyn

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
1,459
284
Jana katika taarifa mbalimbali za habari, Makamu wa Rais Mh. Dr. Shein alisikika akiwahutubia wananchi kwamba serikali inatambua matatizo ya waalimu kama ambavyo yeye na viongozi wenzanke wanavyoyafahamu majina yao, sanjari na hilo, akitembelea kivuko cha Kilombero, alikaririwa akisema serikali inakumbuka ahadi zote ilizotoa mwaka 2005 juu ya kuwapatia wananchi wa Kilombero kivuko kipya, na kwamba wataalamu wako kwenye upembuzi yakinifu ili kuhakikisha suala hilo linapatiwa ufumbuzi wa kudumu.

Binafsi namuheshimu sana kiongozi huyu, ambaye ameonekana ni mtulivu pengine kuliko viongozi wengi katika baraza la mawaziri la awamu ya nne. Lakini kauli zake za hivi karibuni zimeanza kunipa hofu kwamba pengine mheshimiwa ameanza kuingia kwenye kauli za "kisiasa" zaidi ambazo hazilingani na jinsi alivyojipambanua katika jamii.

Watanzania tumechoka na kauli kama hizi, upembuzi gani unaofanyika toka mwaka 2006?? Kama matatizo ya waalimu wanayafahamu vyema, kwa nini wasiyatafutie suluhisho la kudumu???
 
yaaani huuu uchaguzi 2010 unaleta mambo ...hii message sent kwa waalimu ili watoe kura zao bila hiana .. sisi walimu tumechoshwa na kauli zenu za uongo na kweli

wizi mtupu
yetu macho
 
Anahofu na kura za kule hapo 2010. Lakini anasahau kuwa kuna wale wa Zombe kule mahenge, hawatadanganywa na Kivuko. Mwehu gani ataamini kuwa upembuzi yakinifu unafanywa toka 2006 hadi 2009??? Yaani upana wa mto wa pale kwenye ngalange (samaki wa kukaanga) unahitaji miaka mitatu kwa upembuzi yakinifu..!!!!!???? Hivi kama upembuzi unachukuwa muda huo, ujenzi utachukuwa muda gani. Yaani Sheni na Pinda kauli zenu siku hizi siwaelewi. Kweli kwenye msafala wa mamba na kenge wamo................ Nahisi hata mijusi, vinyonga (wa kubadilikabadilika), mende nao pia manakuwemo......Duh Dr. Mbona unaanza ukinyonga....????!!! WHY..???? KWA NINI..????
 
Last edited:
Shekhe Dr SHEIIIIN UNASEMA UONGO KWELI HUMWOGOPI MWENYAAZI MUNGU.
IMEFIKA MAHALI NASI TUACHE UOGA WATU KAMA HAWA YAFAA KUPIGWA MAWE HADI K..A TUMECHOKAAAAAAAH!!
 
yaaani huuu uchaguzi 2010 unaleta mambo ...hii message sent kwa waalimu ili watoe kura zao bila hiana .. sisi walimu tumechoshwa na kauli zenu za uongo na kweli

wizi mtupu
yetu macho

If you could edit your post please delete the word kweli.
 
yaaani huuu uchaguzi 2010 unaleta mambo ...hii message sent kwa waalimu ili watoe kura zao bila hiana .. sisi walimu tumechoshwa na kauli zenu za uongo na kweli

wizi mtupu
yetu macho

Darling wangu kumbe wewe mwalimu? Pole kwa misukosuko mnayopata kutoka kwa serikali dhalimu ya CCM isiyoheshimu umuhimu wenu. Nakumbuka nilivokuwa mdogo nilijiwekeaga miadi ya kuoa mwalimu, ningekutana na wewe ningeshakuweka ndani ya nyumba.
 
ivi Chain anaweza kubaki Makamu? Au itabidi akae benchi akitimiza miaka kumi?
 
Jana katika taarifa mbalimbali za habari, Makamu wa Rais Mh. Dr. Shein alisikika akiwahutubia wananchi kwamba serikali inatambua matatizo ya waalimu kama ambavyo yeye na viongozi wenzanke wanavyoyafahamu majina yao, sanjari na hilo, akitembelea kivuko cha Kilombero, alikaririwa akisema serikali inakumbuka ahadi zote ilizotoa mwaka 2005 juu ya kuwapatia wananchi wa Kilombero kivuko kipya, na kwamba wataalamu wako kwenye upembuzi yakinifu ili kuhakikisha suala hilo linapatiwa ufumbuzi wa kudumu.

Binafsi namuheshimu sana kiongozi huyu, ambaye ameonekana ni mtulivu pengine kuliko viongozi wengi katika baraza la mawaziri la awamu ya nne. Lakini kauli zake za hivi karibuni zimeanza kunipa hofu kwamba pengine mheshimiwa ameanza kuingia kwenye kauli za "kisiasa" zaidi ambazo hazilingani na jinsi alivyojipambanua katika jamii.

Watanzania tumechoka na kauli kama hizi, upembuzi gani unaofanyika toka mwaka 2006?? Kama matatizo ya waalimu wanayafahamu vyema, kwa nini wasiyatafutie suluhisho la kudumu???

huyo mnafiki ndugu zake pemda wanakufa kwa matatizi kila siku.

na hapo yupo kwanafasi ya muungano yaani kwao na hata bongo lakini hana faida yoyote na ndungu zake wapemba kuwatete yeye na mawaziri wenzake kutoka kwa wapemba huko.

kazi kutizama matumbo yao na kuwaua wenzao huko zanzibar.

ni wasaliti walionunuliwa ili kuiua zanzibar na kujaza adili mbaya na mila mbaya pamoja na hao wengineo watumwa na wasaliti walio zanzibar.
 
wakati watu wako busy na ufisadi, yeye yuko mkoani anaweka mawe ya misingi kwenye vyoo vya shule zisizo na walimu.
 
Heshima ya Mzee wetu Dr Shein ilikuwa juu kuliko wanasiasa wote wa CCM,nadhani wanaomshauri kwamba aanze kutetea kiti kwa gia hiyo wamemdanganya!

Mzee Shein tulia tu kama zamani mkuu,achana nao hao mafisadi,wakikuandikia hotuba ,kataa kuzisoma!

''Kama unalina asali,mikono ikitapakaa asali,UKWELI unailamba tu,lakini chonde chonde mzee Shein hiyo mikno iliyokwishatapakaa asali ya CCM,,ISUGUE KWENYE UDONGO,TENA WA KICHUGUUU!
 
lakini hivi mlitegemea acheze ngoma ya peke yake katika bendi moja?
in politics you always dance to the current tune,akiaza kufanya ya kwake peke yake atajikuta nje ya ulingo
 
if he is not against them he is with them. Simshangai kusema hivyo, ni wale wale. Pengine anafanya mazoezi ya kuzungumza, c anataka na kule Zanzibar?
 
Back
Top Bottom