Jile79,
Mkuu maneno yako msumari na hili ni fumbo kwa wale wasiojua uchafu wa siasa..
Huu mpango wote sii kwa ajili ya kutafuta ukweli isipokuwa mwanzo wa kuivunja nguvu report ya Mwakyembe..Kazi yote hii ni kuonyesha kwamba Mwakyembe na kamati yake sii watu wa kuaminika, wakiomba takrima ktk ofisi za seriikali jambo ambalo linaweza thibitishwa na hundi walopokea kama posho.. It might have been offered na ofisi husika lakini kwa vile hawa kina Mwakyembe hawakufahamu dhumuni la posho hizo walichukua...
Now, kama Mwakyembe na wenzake walichukua, na kisheria kuchukua kwao ni kinyume cha taratibu za bunge na kamati zake hapo mkuu wangu kachemsha..lakini navyofahamu mimi kamati zote nchini huchukua posho nje ya malipo ya awali isipokuwa hawa jamaa wanadai kwamba kamati hizi (ikiwa ni pamoja na ya Mwakyembe) HUOMBA TAKRIMA ktk vikao vyao..Hapa Mwakyembe akae wima laa sivyo ndio wamemmaliza na kuikata makali report ya kamati yake, Ushindi kwa Richmond na Mafisadi..
kweli watz hatuko serious mambo kibao ya kipuuzi yanatokea tunayachunia tu........watu wanatuingiza gizani kwa makusudi tumekaa kimya.....pccb tumewapa kazi ya kuchunguza mkataba wa richmond wamekuja na ripoti ya kuficha ukweli tumeundiwa kamati teule na waheshimiwa tuliowachagua wamekuja na ripoti tofauti kabisa...bado tumekaa kimya wanaendelea na ajira zao......ningekuwa na uwezo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!ningeandamana hata peke yangu kupinga hawa wapuuzi kuendelea kufanya kazi ambayo hawaiwezi,,,,,,,,tunachukuwa hatua gani kwa uozo wote huu jamani kweli tutaendele kulalamika mpaka lini?
Nakumbuka hili lilitokea Karatu (ambako Halmashauri inaongozwa na Chadema) madiwani walikataa kulipia malazi ya ujumbe wa Makamu wa Rais kwa vile tayari walisha lipwa posho na ofisi zao walikotoka.
Hili la posho sioni kama ni suala la PCCB. Ni suala la kiutawala zaidi katika sehemu zinazohusika. Suala hili linakuzwa na magazeti ya Rostam na swahiba wake Lowassa kwa sababu ya chuki zao binafsi dhidi ya watu kama akina Mwakyembe. Wanafanya vituko vingi sana mafisadi hawa ili kulipiza kisasi baada ya kuumbuliwa kwenye Richmond. These two guys are very vindictive! Mie binafsi nimepoteza imani kabisa na vyombo kama PCCB. Kuna kesi kubwa nyingi za rushwa walijifanya wanachunguza lakini matokeo yake hatuyaoni. Kuna rushwa za waziwazi kwenye mikataba kibao ya nishati, wizi wa kutisha wa Kagoda, Commodity Import Support. Deep Green, nk. Lakini hakuna kinachoendelea. Sasa suala la watu kupewa posho (tena bila kuomba) linakuaje suala kubwa kiasi hicho! Tuwe serious jamani....
samahani mkuu unao uthibitisho wa manenno haya?... hivi kweli Rostam alisema hivyo.kama alivyodai Rostam kwamba anajivunia Biashara waliyofanya mababu zake karne ya kumi na tisa during slave trade huko Tabora
PASCO,Kwa maoni yangu, Mwakiembe hakamatiki kwa ajili ya matamshi yake ya Dodoma, unless PCCB walimtaarifu spika kwa maandishi kuwa wanamuhitaji Mwakiembe kwa mahojiano, huku Mwakiembe mwenyewe amepelekewa samansi ya PCCB kuitwa kwa mahojiano,akakaidi, ni kweli anakamatika.
Jamani ni malipo gani ya mara mbili unayoyaongelea ndugu yangu mbona huelewi mambo. kama unalipa Bunge inatoa posho maana imekasimu ktk bajeti yake na wizara au taasisi ikitoa posho maana yake imekasimu ktk bajeti yake sasa hapao kuna double payment?? unataka hiyo posho iliyokasimiwa kwa ajili ya Vikao vya Wabunge hata kama iko nje ya Bunge apewe nani upewe wee then baadaye utakuja kuiaccount vipi?? mwisho wa siku hiyo posho iliyokasimiwa na wizara au taasisi husika itatakiwa kuonekana kweli imelipa wabunge na Si vinginevyo. eti PCCB wana hoji malipo ya posho 2 wapi ?????
mzee umeishiwa sera sasa umeanza kushabikia hata upuuzi. Kweli wajinga ndio waliwao kwa kupenda kulaMbona wewe wamkatisha tamaa HOSEA? Hakuna aliyesema Mwakyembe akate tamaa. Yeye aendelee kuwashughulikia akina HOSEA na Richmond ila akumbuke milele maneno ya KIKWETE kuwa " UKITAKA KULA BASI KUBALI NA WEWE ULIWE KIDOGO".
Sasa yeye wakimgusa kidogo anaruka utafikiri bikira, ehhh Kaza moyo Mwakyembe, ndiyo SIASA hiyo na hapa si sheria tena.
huyo ingia ndivyo alivyo na kijana mdogo sikonge ni watu wa hisia na wakati mwingine huwa wanabishana na ukweli. sasa sijui kama tatizo ni ugumu wa kuelewa au ndio huwa hawaelewi kabisa. Hapo hakuna rushwa bali ni ubabaishaji tu. na kisheria mwakyembe anaweza kukataa kuhojiwa na badala yake anaweza kwenda kusemea mahakani. hapa hapana tatizo kabisa, Mwakyembe ni muelewa kuliko hawa wakina inginia na sikonge wanavyodhani. Huwa tabia ya hawa watu ni much know sana kiasi cha kupinga hata pasipo kuelewa. kila siku nawaambia mwakyembe hakamatiki na ni kiongozi anayefaa kwani anaonyesha njia na si mtu wa kubuluzwa na upepo. Sasa wewe etim uhojiwe na takukuru kwani kuna rushwa hapo? na kisheria mtoa rushwa naye anamakosa ikiwa ametoa rushwa bila kuwatonya watu wa takukuru. sasa kwenye rushwa lazima awepo mtoa rushwa naye ashitakiwe kwa kutoa rushwa. Na je kuna hela ya moto aliyokamatwa nayo mwakyembe? sasa ahojiwe nini? kama ajakamatwa na rushwa!. Hapa ni kutaka kupima sumu kwa kulamba. Masanilo stay putNipo Kyela unanihamisha?
wewe ndiye umeishiwa na hiyo mango tree yako.mzee umeishiwa sera sasa umeanza kushabikia hata upuuzi. Kweli wajinga ndio waliwao kwa kupenda kula
Susuviri,
Jina kuonyesha yupo kwenye active user haina maana kwamba yupo actively aki surf net au akisoma thread husika. Kwa mtu mkongwe JF kama wewe unatakiwa ulijue hili.
Kama hujui nafikiri unahitaji tuition toka kwa Invisible.
Kama huja log out jina lako linaendelea kuonekana. Pia kuna watu wengine hasa nje ya TZ ambao PC zao muda wote zinakuwa on na wao kama haja log out jina lake linaendelea kuonyesha hata kama yeye kasafiri.