Mkuu Zitto nimekupata hapa, lakini pia hili linawezekana tu pale PCCB watapofuata utaratibu unaokubalika sio kukurupuka tu kwamba leo tunamtaka fulani basi wanapiga simu kumuita.
Nina amini msimamo wa Mwakyembe kukataa kuhojiwa ni sahihi na kwamba utafungua njia mpya ya hawa watu kuacha kutaka kunyamazisha watu fulani eti kuwa tu wana mamlaka ya kuwanyamazisha
.Akawasikilize kina nani? Kwani wao PCCB rushwa wanazopokea nani huwa anawahoji? The point ni kuwa yeye Hosea,uchafu wake kausafisha lini,na kama kupokea posho mara mbili ni rushwa,vipi wao PCCB wanapojaza Imprest za uongo na wanajidai kwenda kukamata watuhumiwa wa rushwa,kisha wanaishia kwenye mabaa kubwia maji ya Ilala (beer) nani huwa anawahoji? Tunaishi nao,na tunawafahamu vizuri sana.
mheshimiwa zitto tunaomba vifungu (kanuni za bunge, katiba au sheria nyingine yoyote) vinavyotoa hiyo kinga maana hapa kidogo mnatuchanganya, hasa mnapozungumzia kinga sasa hivi, huku hamkusema chochote kuhusu kinga ya mbunge hasa pale mheshimiwa basil pesambili mramba (kesi ya misamaha ya kodi) na mheshimiwa andrew chenge (kesi ya kusababisha ajali) walipohojiwa na kesi zao kwa sasa ziko mahakamani!
"10 (1)Special Power of Investigation
An officer of the Bureau investigating an offence under this Act may
a) Order any person to attend before him for the purpose of being interviewed orally or in writing in relation to any matter which may assist investigation of the offence."
Na hiyo ndio nguvu ya kweli kwenye chombo cha uchunguzi amna wa kuachwa, sawa sawa hata kama wengine bado hawajafikiwa huu ni mwanzo mwenye kosa na asie na influence ndio aanziwe awe Mwakyembe sijui nani. Cha muhimu hapa ni kuanza kumaliza huu utamaduni wa hizi tabia zao mbaya ambazo zimekuwa ignored for too long.
Wakuu zangu,
Mimi nilikaa pembeni kusikiliza wachangiaji lakini kuna maswali ambayo nashindwa kuyajibu ikiwa kweli tutatafsiri hizi sheria kwa jinsi tunavyojisikia..
Ningependa kujua ni wakati gani TAKUKURU wanaruhusiwa kuwahoji Wabunge?..Mathlna Takukuru wamewahi kufanya uchunguzi wa Richmond kabla ya kamati ya Mwayembe (kama Mnakumbuka) Je, ni Mawaziri ganmi waliohojiwa na TAKUKURU kama sio hao hao Wabunge!..
Pili tusichanganye makosa ya mbunge ktk utendaji akiwa nje ya Bunge, mathlan Mbunge ambaye ni waziri akifanya wizi wizarani sidhani kama sheria inakataza asihojiwe kwa wizi huo kwa sababu ni Mbunge hilo moja, ila sheria inakataza Mbunge asihojiwe maswala yoyote yanayohusiana na BUNGE..(kama sikosei).
Mfano ni kuhojiwa kwa Mramba, huyu kweli aliikuwa Mbunge lakini kesi yake ilihusioana na utendaji kazi wake akiwa waziri wa wizara na sii Mbunge.. hivyo inakubalika kisheria..Tukipinga hili ni lazima tujiuliza je ni wakati gani wabunge wanaweza kuhojiwa.. mathlan kina Rostam, who's to question them..maanake hata Rostam ni mbunge!
Swala la Mwakyembe kuhojiwa lipo wazi kabisa kuwa ni makosa...kwa sababu lipo ktk kifungu cha pili..Kazi zote za kamati za Bunge zilipewa baraka za Bunge pamoja na rais mwenyewe..sote tunakumbuka hili, hivyo kama kulikuwepo na malipo ya posho mbili -mara zote sheria za uhasibu mkosa ni yule aliyelipa posho hizo kinyume cha sheria..iwe ni muidhinishaji wa malipo ya posho za Bunge, shirika, wizara au taasisi husika kwa sababu kabla hujalipa poshi au fedha zozote ni lazima kuwepo na suppoting document ambayo huidhinishwa kulingana na tumizi tarajiwa..Ni kazi ya Auditors kufanya uchunguzi huo na kuwakilisha mahesabu yao, kulipwa posho mara mbili sii kosa la kukihusisha chombo kikubwa kama TAKUKURU kama vile wamekosa kazi..
Hao waliolipa waliweka mahesabu ya posho hizo ktk kifungu gani na iliidhinishwa na nani?..Na ikiwa sehemu zote za kikazi ziliidhinisha posho hizo kimakosa hili sii kosa linalotakiwa kufikishwa mahakamani isipokuwa ni chombo husika (i.e Bunge) kukata (as a refund) fedha zote walizolipa kwa mbunge huyo kama ziada ya malipo.. Unless Bunge lenyewe ndilo lipeleke malalamiko haya TAKUKURU na kuomba uchunguzi ufanyike.
Mkuu kwa mtazamo wangu Takukuru wana makosa ikiwa BUnge au rais hakutoa amri hiyo... Sii kazi yao kuchunguza posho na malipo ya wabunge ktk kazi za bunge..sasa hapa mkuu umenielewesha vyema........ila wasipinge takukuru kuwahoji....mimi nionavyo ni kwamba Takukuru wanafanya uchunguzi kwanza...na kuhojiwa si kosa kabisa
Huyu Hosea ndio aliwasafisha wale matapeli wa Richmond then akawa busted lakini cha ajabu hakuna chochote kilichomtokea,huyu anatakiwa kuwa jela sasa hivi ,wapuuzi kama hawa ndio wanatumaliza na hakuna chochote wanafanya zaidi ya kugeuza chombo muhimu kama PCCB/TAKURURU kuwa cha kisiasa na revenge kwa wote wanaoonekana kama ni hatari kwa serikali yao...kuna rushwa za mabilioni kila siku lakini hakuna prosecution yeyote kila siku ni kanyaboya tuu hawa matapeli wa TAKURURU,huyu Hosea lazima aondoke!
yaani hunigusi hata kidogo na hoja yako. kumbuka mtu unapoitwa kwa mahojiano njia moja tu ndio inayokubalika nayo ni kwa njia ya Summons tena ya maandishi. niambie ni lini umewahi kuona summons ya simu??ndugu yangu hiyo haipo hata mie ningeitwa kwa staili hiyo nisingekwenda.
Mind you tena PCCB wanafanya kazi yao kienyeji tena kwa dharau kubwa sana hebu fikiri anamuita Mbunge akamhoji halafu anamuuliza summons iko wapi anamwambia we njoo tu utakuta barua yako getini. je ndo hivi tunavyotakiwa kufanya kazi kwa dharau na kujidai hata pale tunapokuwa tunashughulikia wakubwa. si hivyo hata kidogo. mwacheni Mwakyembe atajipanaga aende akiitwa kiustaarabu na sio kwa njia waliyotumia kumuita NASEMA HAIPO KISHERIA HATA UENDE WAPI. "Government works with Papers" bwana na hapa naongelea summons ya maandishi ndugu yangu na sio mtu alete upuuzi wake wa kupiga simu.
Tukirudi kwenye issue ya PCCB kudai wabunge wamepokea posho mara mbili ni posho gani hiyo unayoingelea. hivi ofisi yako ikikulipa posho ya kikao halafu ikaja ofisi ya waziri Mkuu ikakulipa posho ya chakula je posho hizo zinafanana?? tazama kwanza hayo ni majina mawili tofauti hata uende wapi. sasa huyo PCCB anayeitafuta posho ya mara ya pili ni ipi. PPC kama umekosa kazi za kufanya kaa chini ukapambane na ma rushwa makubwa unataka tukuandikie hapa na hasa tukianza na wewe mwenyewe HOSEA una uozo mwingi wa kwako mwenyewe sasa sijui tukuundie TUME??? tukufichue ngoja nipe muda