Dr. Mwakyembe: Sikumhoji Lowassa kwa sababu ushahidi dhidi yake ulikuwa unajitosheleza!

Kipindi kile alimnyoa akiwa waziri wa wizara gani vile???
Kumnyoa ni kumwondolea marupurupu anayopata kama waziri mkuu mstaafu! Nyie na Mwakyembe wote hamna kitu kichwani! Utamwitaje mtu fisadi huku ukiendelea kumlipa? Hovyo kabisa nyie watu......
 
Si bungeni alipata nafasi ya kuongea? Akaishia kusema tatizo ni eti kiti chake. Utafikiri alizaliwa nacho.

Kama hakuhusika na Richmond basi bosi wake ndio alihusika. Si angesema?

Akaamua kuishia na siri
 
Kumnyoa ni kumwondolea marupurupu anayopata kama waziri mkuu mstaafu! Nyie na Mwakyembe wote hamna kitu kichwani! Utamwitaje mtu fisadi huku ukiendelea kumlipa? Hovyo kabisa nyie watu......

Anaogopa mpunga utapungua?
 
Hivi hakuna dawa ya kuzui kuchubuka kwa ubongo
 
Kumnyoa ni kumwondolea marupurupu anayopata kama waziri mkuu mstaafu! Nyie na Mwakyembe wote hamna kitu kichwani! Utamwitaje mtu fisadi huku ukiendelea kumlipa? Hovyo kabisa nyie watu......
Nyie si ndo mlizunguka nchi nzima mkimuita fisadi? Halafu mkazunguka nchi nzima kumsafisha? Mkidhani watanzania ni wajinga...
 
Nyie si ndo mlizunguka nchi nzima mkimuita fisadi? Halafu mkazunguka nchi nzima kumsafisha? Mkidhani watanzania ni wajinga...
Sawa, hilo litakuwa lilifanyika baada ya kubaini ukweli-sasa tusaidie kujibu swali hili: kwanini 'fisadi' Lowasa anaendelea kulipwa na serikali inayoongozwa na akina Mwakyembe na wewe mpiga debe wao?
 
MBUNGE ATUHUMIWA KUTAKA KUINGIA NA KONYAGI BUNGENI
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari ametuhumiwa bungeni na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe kuwa alitaka kuingia kwenye eneo la Bunge akiwa na chupa ya Konyagi.
Hata hivyo Nassari amekanusha kuhusika na tukio hilo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika Viwanja vya Bunge, mjini Dodoma leo.
 
Huu ni Upumbavu,

Mwakyembe ni Kiongozi wa Serikali sio Bunge!
Kama yeye kamuacha Bashite afanye kazi yake ya Ku deal na Wasanii isiwe ndio kigezo cha yeye kuungilia Mamlaka ya Bunge
 
PhD holder anajaribu kutengeneza scandal hapo kwa Nasari. Kweli chuki zao huwa hadharani ukiwagusa kuhusu Bashite.
 
Kwani alilalamikia nini kuhusu ile Kamati iliyochunguza issue ya Bashite kuvamia Clouds? Si angewauliza kwanza wajumbe wa Tume hiyo kama walikuwa na ushahidi wa kutosha wa kutohitaji kumhoji Bashite pia? Ph.D nyingine unakuwa nazo shaka sana aisee...
 
Sawa, hilo litakuwa lilifanyika baada ya kubaini ukweli-sasa tusaidie kujibu swali hili: kwanini 'fisadi' Lowasa anaendelea kulipwa na serikali inayoongozwa na akina Mwakyembe na wewe mpiga debe wao?
Kabla sijajibu swali lako...hebu nisaidie mimi na watanzania kutuelimisha kuwa ni UKWELI gani ambao mliubaini na kuanza kutwambia kuwa sio fisadi tofauti na awali ambapo mlituaminisha kuwa ni kubwa la mafisadi?
 
Yaani Nassari kurudi bungeni ndio anarudi na huu upuuzi??? Alienda kusoma au kuvuta bangi?
 
Eti huyu ndio Dr.wa sheria!!!
Kaka tunafuata kanuni na taratibu na si kuhemuka tu,halafu Nasari kuleta jambo la Lowassa leo baada ya miaka kibao ni kutumia muda na rasmali za Watanzania hovyo,siku zote alikuwa wapi au ndio kujikomba kwa Lowassa?Wabunge wanatakiwa kutuhurumia badala ya kujadili mambo ya maana yaliyopo mezani tunajadili mambo ya akina Lowassa wakati Nassari anava kaptula ,huu kama si ujinga ni nini?Chadema mnatupeleka siko halafu huo muda na hizo hela wanazotumia kuongelea ujinga zingesaidia kutuletea tija ,wabunge wa Chadema sijui akili zao zikoje.
 
Yaani Nassari kurudi bungeni ndio anarudi na huu upuuzi??? Alienda kusoma au kuvuta bangi?
Anaongelea upuuzi uliotokea wakati akivaa kaptula shule ya msingi huko kwao Arumeru,sijui hayo anayoongelea ndio ilani ya Chadema ?mambo ya mwaka 47 anayaleta leo bungeni,anapoteza muda na pesa bure kwa kuongelea utumbo,toka lini Nasari ana uchungu na Vuvuzela pamoja na Mamvi kama sikupotezeana muda bure ,nilidhani angekazana kuzungumzia swala ala ardhi ambalo Wameru kila leo wanaandamana
 
Mwakyembe ni aina mojawapo tu ya wasomi wetu wasioitendea haki taaluma yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…