Nadhani kila mtu anayefuatilia siasa za Tanzania anasikitiika na hali hii ilivyo!! Kila mtu anatamani Dr Mwakyembe aseme kinachomsibu huku watu wengi wakiamini kuwa huenda ukawa ndo mwanzo wa mabadiliko makubwa nchini, Lakini Dr. yeye pia anayo haki na uhuru wa maamuzi yake binafsi ya kusema au kutosema milele.
Kwa hiyo, ningeshauri iundwe kamati ndogo kutoka hapa hapa JF imtembelee Dr. kujionea hali yake pamoja na kumpa pole,lakini ikamhoji kupata ukweli. Na baada ya hapo, tuweze kujulishwa members wote kupitia hapa jamvini.
Ikumbukwe kuwa, ni hapa hapa jamvini! JF member aliweza kutoa taarifa za hali ya Dr. mwaka jana ndipo Mhe. Rais Dr. JK akapewa taarifa na wasaidizi wake kuhusu hali yake, ndipo akaamua kumtembelea na baada ya muda mfupi tukapewa taarifa za kupelekwa Appolo. Kwa hiyo, tujitendeeni haki wanaJF na tuendelee kuzitendea haki nafsi zetu kwa kutafuta ukweli na kuuweka wazi.