Upepo na hali ya siasa kwa mbunge huyo si shwali wilayanikyela kama lilivyokuwa 2010, tofauti na watu wengi wanavyodhani kupitia vyombovya habari akionekana mchapakazi kitaifa lakini jimboni kwake wamemchokakwasababu amelitelekeza jimbo lake.
Katika hali ya kushangaza na kusikitisha, kuna tetesi kwambaDr Mwakyembe Mbunge wa Kyela amejikuta anapata kashfa na aibu kubwa jimbonikwake Kyela baada ya kutoa na kuahidi misaada mbalimbali wilayani humo; ikiwani njia ya kujibu mapigo kwa Asasi na makamanda wa CHADEMA waliotoa misaada wilayani hapa.
Inasemekana kashfa na aibu ya kufungua mwaka 2013, imempatawaziri huyo baada ya kujifanya ametoa msaada wa magodoro 40 na mashuka 60kwenye hospitali ya wilaya ya Kyela, kumbe ni msaada uliotolewa na Kampuni yaBioland. Aidha, Dr Mwakyembe ameahidi kutoa madawati 180 kupitia mgongo wa benkiya NBC, tawi la Kyela, hata hivyo kuna taarifa kuwa benki hiyo imemkatalia yeyekuwa ndiye ametoa madawati hayo kwa kigezo kuwa benki haiendeshi shughuli zakekisiasa na itakabidhi msaada wa madawati hayo muda wowote itakapoona inafaa. Yote hayo alikuwa anajaribukujibu mapigo ya Asasi ya SCSA au Pambana Saidia Jamii iliyotoa madawati 100kwenye shule ya msingi Ikombe.
Kama haitoshi, Dr Mwakyembe akiwa kwenye mkutano wa hadharakata ya Ngonga karibu na nyumbani kwake aliahidi kutoa mifuko 100 ya sarujiakijibu mapigo ya Diwani wa CHADEMA, kamanda Tamali aliyetoa mifuko 20 kwenyekata hiyo. Ahadi hiyo imeibua hasira kubwa kwa wanakyela kutokana na ukweli kwamba mbunge huyo haonekani jimbonikwake na ahadi nyingi alizotoa jimboni hapa hakuna iliyotimizwa, ndio maana wanakyelahawana imani naye tena.
Kutokana na hali hiyo, kikao cha ndani cha dharura cha CCMwakiwemo wazee kiliitishwa wilayani hapa ambacho kilikuwa mahsusi kumuonya mbungekuhusu mambo hayo aliyofanya kwani ni kuwadanganya wananchi ikizingatiwa kuwaahadi nyingi alizotoa jimboni hapa hajatekeleza.
Upepo na hali ya siasa kwa mbunge huyo si shwali wilayanikyela kama lilivyokuwa 2010, tofauti na watu wengi wanavyodhani kupitia vyombovya habari akionekana mchapakazi kitaifa lakini jimboni kwake wamemchokakwasababu amelitelekeza jimbo lake.
Nawasilisha................
Source: Mdau kutoka Kyela.
issue sio majungu wala chuki bali kinachotakiwa ni kujitoa kwake mwenyewe na sio kupitia mgongo wa wengine na hilo ndilo wanachama wake wanahoji piamajungu kwa wanaume sio kitu kizuri
Cha msingi wote mmetoa kwa maendeleo ya watu wa kyela
au mnatoa ili mpongezwe? kushindana ni kuzuri kama anaefaidika ni mwananchi wa kawaida so nyie endeleeni kushindana
alitakiwa kusema msaada huu ni kutoka kampuni husika na sio yeye kuwa ndiye mtoajiUnajua watu hawafikirii kabisa, inawezekana hayo makampuni yakatoa kama mbunge ndo kaenda kuinfluence unafikiri nani amekuwa msaada wa kupatikana kwa huduma husika kumbuka mbunge ni muwakilishi wa wananchi yeye ndo anajua matatizo ya watu wake zaidi kuliko mtu mwingine hasa yule ambaye yupo committed. Kwa hiyo hii si kashfa safi sana hangaika popote kwa ajili ya watu wako.
mimi nilifikiri ameiba hela ya serikali, kumbe hajaiba, sasa mayowe yote ya nini? au mnataka kumnyang'anya jimbo lake la kyela?
Wadau,
Ukisoma hicho kinachoelezwa kama tetesi hapo juu kweli ni tetesi na wala hakuna uhalisia wowote. Mbunge kama mwakilishi wa wananchi anayo nafasi ya kutafuta namna ya kushawishi wadau mbalimbali wa maendeleo kuchangia shughuli za wananchi. Iwe ni benki, asasi ya kiraia au hata serikali kuu mara nyingi utayari wao kuchangia shughuli za raia hutokana na ushawishi wa mtu aliyeko katika uongozi mfano; mbunge!
Kwamba kuna mabenki (NBC) yanataka kutoa misaada/mchango bila kutumia mgongo wa mbunge na kwamba yeye anawalazimisha hizo ni porojo za kisiasa.
Taarifa za kiinteligensia zinaeleza kuwa Dr. Mwakyembe yuko jimboni kwake kwa takribani wiki ya 2 hivi sasa kuanzia tarehe 30 Disemba, 2012 kwahivyo hoja kwamba haonekani jimboni kwake ni uongo wa wazi.
Nakumbuka huko nyuma hoja dhidi ya nguli huyu wa siasa za Tanzania zilijikita kwenye ujenzi wa barabara ya Ipinda na nyingine wilayani. Hivi sasa barabara hiyo inafanyiwa matengenezo makubwa na itawekwa lami kwa kilometa zisizozidi 5 (mwenye takwimu sahihi ataeleza), lakini nyingi za barabara za viunga vya wilaya hii zimekuwa zikiwekewa matuta na makaravati ili ziendelee kupitika kipindi hiki cha mvua. Mfano wa barabara moja wapo, ni kile kipande cha kutoka lilipo daraja la mto Nsesi hadi ziwani kule Katumba Songwe.
Suala la mchango/msaada wa magodoro 40 hii nayo ni nongwa inayoenezwa na "political cynics" katika siasa za Kyela. Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika ni kuwa magodoro hayo kwanza hayakuwa yote kwa ajili hospitali ya wilaya. Nimewahi kuzungumza na wasaidizi wa Dr. Harrison naye akanieleza kuwa magodoro hayo yalitolewa maalumu kwa ajili ya vituo vya afya na zahanati zilizoko wilayani ambapo baada ya ziara iliyofanyika huko nyuma iligundulika kuwa kuna uhaba mkubwa wa magodoro kiasi kwenye baadhi ya vituo wagonjwa wamekuwa wakihudumiwa juu ya vitanda vilivyotandikwa mikeka.
Katika ushushushu wangu niliweza kushuhudia magodoro hayo yakisafirishwa kutoka nyumbani kwa Dr. Mwakyembe Dar kwenda kyela, na kwa uhakika vipande vingine ililazimika vikaongezwe siku ya safari ili kukidhi hitaji la vituo hivyo vya afya. Swali linakuja, Je, ni kwamba hao Bioland walinunua magodoro hayo na kupeleka nyumbani kwa Dr. ili yakafanye nini? Na hata baada ya kufika Kyela yalifikishwa kwanza nyumbani kwake pale Ikolo kabla ya kukabidhiwa (wakazi wa eneo hilo wanaweza kuwa shahidi muhimu kwani gari iliyobeba magodoro hayo ilikaa pale kwa siku kadhaa).
Kubwa kuliko yote ni kuwa hata hao wanaosemekana kugomea kupokea magodoro hayo kwa sababu wanamjua aliye nyuma ya mchango huo hiyo siyo hoja: wao walihitaji mchangiaji au tatizo lao ni uhaba wa magodoro katika vituo vya afya? Ni ujuha! Magodoro yamekuja pokea yaanze kutumika labda kama kuna ajenda nyumba ya mgomo huo.
Naomba kuwasilisha kwa uchache wa ninayoyafahamu!
kipimo chake subiri uchaguzi 2015 halafu ulingalishe na chaguzi za miaka ya 2005 na 2010Oooooh TANZANIA, SIASA NA UONGO MBELE....
WAMEMCHOKA MWAKYEMBE??? KWENYE JIMBO LIPI HILO??
Mmmmh sijui lakini labda utupe kipimo chako ni kipi???
Mtoa maada ni muathirika wa uchapakazi uliotukuka wa Dr Mwakyembe, nahisi ni mtoto wa mmoja wa Directors waliosimamishwa pale bandarini au yule polisi mwizi wa shaba..
Ahsante kwa Tetesi:Katika hali ya kushangaza na kusikitisha, kuna tetesi kwambaDr Mwakyembe Mbunge wa Kyela amejikuta anapata kashfa na aibu kubwa jimbonikwake Kyela baada ya kutoa na kuahidi misaada mbalimbali wilayani humo; ikiwani njia ya kujibu mapigo kwa Asasi na makamanda wa CHADEMA waliotoa misaada wilayani hapa.