Dr Mwakyembe aunga mkono nauli mpya

Dr Mwakyembe aunga mkono nauli mpya

mgomba101

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2011
Posts
1,822
Reaction score
711
Dk Mwakyembe alisema upandishwaji huo ulifuata vigezo vyote hivyo hakuna sababu za kulalamika. Alisema kiwango kilichopandishwa ni kidogo ukilinganisha na jinsi wamiliki wa vyombo husika walivyokuwa wameomba.

Alizitaja hatua zilizopitiwa kuwa ni pamoja Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), kuitisha mikutano ya wazi na wadau kwa ajili ya kupokea maoni yao.
Hata hivyo, aliwaonya wamiliki wa vyombo hivyo watakaokiuka na kupandisha nauli kwa kiwango cha juu akisema lazima ‘atakula nao sahani moja'.

Alisema wawakilishi wote wa abiria waliambiwa kama ongezeko hilo dogo la Sh100 hawaridhiki nalo, sheria inawaruhusu kukata rufani katika Baraza la Ushindani na kwamba hakuna aliyefanya hivyo na kubaki kulalama nje ya taratibu.

"Mimi kama Waziri wa Uchukuzi sina tatizo na ongezeko hili dogo la nauli za daladala. Tatizo langu ni tabia yetu ya Watanzania wengi kukacha vikao halali vinavyojadili mambo yanayotuhusu na kuja kulalamika baadaye," alisema Dk Mwakyembe.

Alisema awali watoa huduma ya daladala waliomba kupandisha nauli kutoka Sh300 hadi Sh872 kwa abiria sawa na ongezeko la asilimia 149.

Alisema baada ya majadiliano hayo, Sumatra ilikubali nauli hiyo iongezwe kwa Sh100 tu kwa watu wazima na Sh50 kwa wanafunzi ili kugawana maumivu ya gharama za uendeshaji kwa watoa huduma.

Dk Mwakyembe alisema ni kweli gharama za uendeshaji kwa wenye mabasi zimeongezeka ikiwamo bei za mafuta pamoja na vifaa mbalimbali kama matairi.

Waziri huyo pia aliunga mkono ongezeko la nauli katika usafiri wa reli na mabasi yaendayo mikoani kuwa nauli zao hazijapandishwa kwa kiwango kikubwa hivyo haoni ni kwa nini Serikali isikubali.

Chama cha kutetea abiria hawakualikwa wala kushirikishwa! Sumatra na wamiliki walikaa wenyewe wakapandisha nauli.

Dr Mwakyembe ni mnafiki na mchumia tumbo! Madhara ya polonium yanaanza kuonekana!

Je daladala watabeba abiria level sit?? Mabasi mengi ya mikoani ni chasis za malori/chuma chakavu!!
 
"Mimi kama Waziri wa Uchukuzi sina tatizo na ongezeko hili dogo la nauli za daladala. Tatizo langu ni tabia yetu ya Watanzania wengi kukacha vikao halali vinavyojadili mambo yanayotuhusu na kuja kulalamika baadaye," alisema Dk Mwakyembe.

unafiki tu huu,sasa yeye aliyeingia kwenye hicho kikao msimamo wake ulikuwa nini?nauli iongezwe au isiongezwe.
the decision was already made nauli ingepandishwa tu!!!

kwa hiyo anasema watu wote walioingia kwenye kikao waliunga mkono ongezeko la nauli kwa 100% kwa manufaa ya nani?? Madhara ya polonium mabaya sana.
 
Ha haa! ndani ya ccm hakuna alie bora.tushirikiane kuitokomeza 2015.
 
Dk Mwakyembe alisema upandishwaji huo ulifuata vigezo vyote hivyo hakuna sababu za kulalamika. Alisema kiwango kilichopandishwa ni kidogo ukilinganisha na jinsi wamiliki wa vyombo husika walivyokuwa wameomba....
Kuwapa wamiliki ongezeko kiduchu kulinganisha na hali halisi ya gharama haitaleta mabadiliko ya ubora wa huduma. Kama serikali inawajali watu wake ifikirie utaratibu wa ruzuku kwa usafiri wa mijini.
 
Nchi ya watakatifu wenye utii kwa serikali yao na mamlaka zake hata kama hawawandewi haki. Kama wakati
mwingine mnalipishwa na makonda nauli isiyo rasmi [Tsh 1000 - Tsh 2000] na mnalipa 'mnajishaua' nini sasa hivi?
Hiyo nauli mliyokua mnalipishwa isivyo halali ndo imehalalishwa sasa.. Kama hamtaki 'tembeeni kwa mguu' kwenda
magogoni pale kumweleza mkuu wa kaya.. :crying::crying::crying:
 
Chama cha kutetea abiria hawakualikwa wala kushirikishwa! Sumatra na wamiliki walikaa wenyewe wakapandisha nauli.

Dr Mwakyembe ni mnafiki na mchumia tumbo! Madhara ya polonium yanaanza kuonekana!

Je daladala watabeba abiria level sit?? Mabasi mengi ya mikoani ni chasis za malori/chuma chakavu!!

...Unaweza kudhibitisha hayo madai yako?isije kuwa hiko unachokiita "Chama cha Kutetea Abiria" ndio miongoni mwa hawa anawazungumzia "Mwakyembe"...

Alisema wawakilishi wote wa abiria waliambiwa kama ongezeko hilo dogo la Sh100 hawaridhiki nalo, sheria inawaruhusu kukata rufani katika Baraza la Ushindani na kwamba hakuna aliyefanya hivyo na kubaki kulalama nje ya taratibu.

"Mimi kama Waziri wa Uchukuzi sina tatizo na ongezeko hili dogo la nauli za daladala. Tatizo langu ni tabia yetu ya Watanzania wengi kukacha vikao halali vinavyojadili mambo yanayotuhusu na kuja kulalamika baadaye," alisema Dk Mwakyembe.
 
kwa hiyo anasema watu wote walioingia kwenye kikao waliunga mkono ongezeko la nauli kwa 100% kwa manufaa ya nani?? Madhara ya polonium mabaya sana.

...Najua hesabu ni tatizo kwenye nji hii lakini unaweza kweli kudhibitisha hilo ongezeko la nauli kwa 100%??, mie mgeni nji hii...

...N.B: Wenye vyombo vya usafiri hawatoi huduma kama wasamalia wema, wapo kibiashara, kama gharama za uendeshaji zimekuwa kubwa hakuna namna kwao bali kuongeza nauli, by the way ongezeko la Sh 100 baada ya miaka 3 ukiongeza na ongezeko la foleni mbalo in turn linapunguza idadi ya root kwa siku, ni mpuuzi tu ndiye atakayesema hili ni ongezeko kubwa, maisha magumu ya "wananchi" yasiwe kigezo cha kuwaumiza "wamiliki" wanaofanya biashara halali....
 
Kuwapa wamiliki ongezeko kiduchu kulinganisha na hali halisi ya gharama haitaleta mabadiliko ya ubora wa huduma. Kama serikali inawajali watu wake ifikirie utaratibu wa ruzuku kwa usafiri wa mijini.

...Pamoja sana mkuu...
 
Huyu teja huwa wakati mwingine huwa anachemka sana...Hakuna cha polonium wala nini! Huyu jamaa sisi tunamjua kuwa mingwengwe plus unga unamtesa...hakuwahi na hajawahi hata siku moja kuwatetea Watanzania. Huyu ni oportunist mchumia tumbo kama ilivyo kwa wengi ndani ya CCM! Anawazidi wenzie kwa uwezo wake wa kuzusha kama alivyomzushia Chizi kisha akamweka binamu yake pale ATCL ...
 
Hii nauli mama ntilie mwenye wanafunzi watatu kila siku waende na kuludi shule....maisha bora kwa kila mtanzania ndo haya bana!!
 
Mwaka 2010 akiwa kijijini Kasumulu-Kyela alitumbia kuwa hagombei tena 2015 lkn juzi akiwa kijijini Malungo kathibitisha kuwa ATAGOMBEA tena 2015 eti kumalizia kazi aliyo ianza 2005!Huyu ni opportunist tu na itamkumba aibu Kyela 2015!
 
...Haa ha ha Malafyale, sasa unamsikitikia nini "opportunists"? si ufurahi tu agombee hiyo 2015 ili akutane na hiyo "aibu"? ila nina uhakika haitakuwa rahisi, Mwakyembe pamoja na ujasiri na uzalendo wake lakini pia ni "mwanasiasa" mzuri kwa maana halisi ya "siasa", so mpinzani wake inabidi awe kwenye "form" hasa ili amwangushe, otherwise...
 
Huyu teja huwa wakati mwingine huwa anachemka sana...Hakuna cha polonium wala nini! Huyu jamaa sisi tunamjua kuwa mingwengwe plus unga unamtesa...hakuwahi na hajawahi hata siku moja kuwatetea Watanzania. Huyu ni oportunist mchumia tumbo kama ilivyo kwa wengi ndani ya CCM! Anawazidi wenzie kwa uwezo wake wa kuzusha kama alivyomzushia Chizi kisha akamweka binamu yake pale ATCL ...

Jamaa kumbe teja? so alisingizia sumu kumbe ni unga,nadhani atakua anawajua wasambazaji hebu naomba information zaidi ni PM kuna issue nataka nikuulize private please!
 
huyu mzee mi kama baba yangu na mara zote nimekuwa nikimpa kura yangu ila toka limwagiwe tindikali limenifanya nilione lichumia tumbo tuu na roho la madaraka.pesa tamuu muda wa kuachia wengine huu agombee 2015 wakati aliaga.....hahahahaaa
 
...Kweli unamheshimu sana huyo baba yako mpaka unawita "li"; by the way ata akigombea mwaka 2015 uamuzi wa mwisho hautakuwa kwake binafsi bali ni kwako na wanaKyela wenzako, so hiyo siyo issue sana, Wanakyela mtaamua...
 
Huyu mwkyembe ni mchum ia tumbo hana haya anawaeleza wananchi maskini wanaoish maeneo mskin kama tandale, mwananyamala,temeke kuwa nauli ya mia ni ndogo kwa sababu baada ya kuondoa watendaji bandarin na kuweka vbaraka wake anapata 40% kwenye mgao ndio maana anaona mia ni ndogo...eeeeh tuepushe nan hawa wanafk
 
Back
Top Bottom