Dr. Mwakyembe afunguka kuhusu Richmond na dhamira yake kugombea Ubunge tena - Oktoba 23, 2015

Nimeshangazwa sana Na kauli za uongo za Dr. Mwakyembe juu ya suala la Richmond.Dr.Mwakyembe usitufanye Watanzania hatuna nakala ya ripoti uliyoisoma bungeni.Dr.Mwakyembe Lowassa hakujiuzulu kwa kuwa ni mhusika mkuu.Mh.Lowassa kwa mujibu Wa ripoti yako mlimtaka ajiuzulu kwa kushindwa kuwasimamia mawaziri aliokuwa ana waongoza.Na kama alikuwa in mhusika mkuu kulikuwa Na ugumu gani Mh.Rais kumfukuza Kazi badala ya kumtaka Lowassa aamue cha kufanya? Dr.Mwakyembe MWOGOPE MUNGU WAKO kumbuka kuna maisha ya Mbinguni hiyo DHAMBI YA UONGI itakutafuna.MUNGU MUHUKUMU YULE ANAYEPOTOSHA HAKI KWA KUSEMA UONGO.Dr.Mwakyembe kumbuka Malipo in hapa hapa Duniani.Dr.Mwakyembe ni nani ndani ya CCM aliyepata MALI ZAKE/UTAJIRI KWA KULIMA MAHINDI NA MTAMA?
 
Mwakyembe mnafiki sana, yeye ndio amechangia malumbano ya richmond kwani aliingiza siasa kwenye sheria, alisahau zile pesa alizopewa zilikuwa kodi ya wananchi akaweka utii wake kwa serikali badala ya wananchi aliotumia kodi zao.Kama mambo aliyosema jana angesema kipindi kile leo lowasa asingethubutu hata kuchukua fomu wacha kugombea urais.lowasa ndie alihusika na richmond na mwenzake rostam aziz lakini alizunguka zunguka matokeo yake leo lowasa anadai hausiki
 
anaongea kwa kusitasita utadhani hakuwa na uhakika wa aliyokuwa akiongea.

Wanasiasa wa CCM wameifanya PHD kuonekana ni kitu Cha ovyo kabisa.

Sio la richmond tu, Yaani Jana nilimfuta kabisa katika list wa wasomi wenye uwezo wa kupambanua mambo, Pamoja na Muuliza maswali sijui hao jamaa wa Star tv huwa wanasomea wapi.

Yaani muuliza maswali ananyweea utadhani yeye ndio anafanyiwa interview
 
Jana nilimfuatilia startv, inaonekana dhahiri ile ni propaganda tunapoelekea kwenye uchaguzi kesho. After all, usitegemee balanced story kupitia startv katika kipindi hiki. Eti Lowassa angewajibishwa na bunge asingejiuzulu,mara Waziri mkuu ana mamlaka kamili kama rais, mara hakushtakiwa kwa kuwa baadhi ya vyombo vya dola havikutekeleza majukumu.. Confusion upon confusion.. Wanahaha.
 
Puuuu....nikijumlisha na ya Kinje leo huko huko star tv naanza kuona mbingu zikifunguka na malaika wakishuka kumlaki Magufuli salenda bridge. Nasi tuliosalia tutanyakuliwa pamoja nao kumlaki tinga tinga magogoni. Na wooote tuseme Ameeeen


Mkuu humjui Kinje wewe, huyo ni Kinje wenu wa Star tv. Mtaumbuka sana mwaka huu.
 
anaongea kwa kusitasita utadhani hakuwa na uhakika wa aliyokuwa akiongea.

Wanasiasa wa CCM wameifanya PHD kuonekana ni kitu Cha ovyo kabisa.

Sio la richmond tu, Yaani Jana nilimfuta kabisa katika list wa wasomi wenye uwezo wa kupambanua mambo, Pamoja na Muuliza maswali sijui hao jamaa wa Star tv huwa wanasomea wapi.

Yaani muuliza maswali ananyweea utadhani yeye ndio anafanyiwa interview

Hizi ndio athari za siasa za kijamaa ni kushabikia chama tu dini elimu hakuna analeta mazungu baada ya habari sometimes wanapiga push up!!
 
Nahilo pia limekwisha pita. hata la yule dr mwingine wa mihogo likija litapita pia. kesho kura kwa LOWASSA.
 
Rais aliisha enda Monduli akamshika mkono akatangaza EL ni mtu safi. Alipata ajali tuu ya kisiasa. Leo anasema nini huyu.
Hawa ma doctor wana matatizo gani. Angalia yule mwenzake Slaa. Kaandaa ilani ya chadema lakini alipoona mwenzake anaitangaza kasema mbaya. Huyu nae report kaiandaa mwenyewe ipo bungeni leo anakuja na swaga tofauti. Ina maana mtu akiwa doctor kuna tatizo anapata kichwani.
Ntazuia mwanangu asifike huko.
 
Mwakyembe kasoma sheria lakini anashindwa kuelewa ushahidi unaweza kukusanywa na ukawa na kila chembe ya ukweli, lakini haimanishi mhusika anahatia kwa Mazingira mengine ya kawaida. Mastermind wa crime kahakikisha hakuna trace inayoelekea kwake.mjomba kahakikisha anaekamatwa ni small fish tu bwana edo.swali linakuja je walimhoji bwana edo? Je walimhoji mjomba? Jibu mi sina.
Pia nimefurahi kaongea ukweli kasema pesa hubadilisha watu na kweli kabisa amebadilika na nina hakika kabisa saiv nywele hazitomtoka tena.kakubali sasa.
 
Mwenyekiti wa kamati iliyochunguza sakata la Richmond Dkt Harrison Mwakyembe amevunja ngome ya UKAWA kwa kubainisha jinsi mgombea wao alivyoshiriki katika sakata hilo hali iliyochangia kuwepo kwa tatizo la umeme hadi leo hii.
 
So Mwakyembe anasema baada ya EL kujiuzulu mgao wa umeme umeisha huko au?
Kwanin amekuja sasa kutuambia? Si alipewa mda bungeni? Hayakuisha?
Njaa mbaya sana! Ndio maana akapewa 'ugonjwa' labda ni 'adhabu' yake kwa kusema uongo
 
Mwanasiasa mkongwe nchini tanzania anayeheshimika kutokana na taaluma yake ya sheria (Mwalimu wa wanasiasa wengi nchini pale chuo kikuu cha Dar es salaam) Dr. Harrison Mwakyembe jana akiwa katika studio za StarTv Mwanza alianika uozo mwingi ulioratibiwa na aliyekuwa waziri mkuu wa awamu ya kwa ya Rais Jakaya Kikwete juu ya Ufisadi hususani ule wa Richmond na Dowans.
Kutokana na taarifa hiyo aliyoielezea kiundani zaidi ya ripoti iliyowasilishwa Bungeni mwaka 2008 (Ilimuondoa Lowasa madarakani) na namna anavyoudanganya umma juu ya Rais kutoa shinikizo ambapo baadhi ya wanasiasa wakongwe nchini wameona ni sawa na kumvua nguo kwani hana la kujitetea.
​
 
11223649_168345296842851_4476293965748472397_o.jpg
 
Back
Top Bottom