Sakata la Richmond: Dr. Mwakyembe amkaanga Lowassa, Kumburuza Mahakamani...

BungelaKatiba2014tz

JF-Expert Member
Feb 18, 2014
1,231
648

Mwakyembe Lowassa.png

Mhe Mwakyembe amkaanga Lowassa kuhusu kadhia ya Richmond na kusema kuwa asikwepe maana tume ya Bunge ilimkuta na hatia na ikabidi ajiuzulu Uwaziri Mkuu.

Ameeleza hayo kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais kupitia CCM Mhe JPM leo huko Kyela katika mfululizo wa kampeni za mgombea huyo. Mhe Mwakyembe kaeleza kadhia hiyo kwa maelfu ya wananchi waliokuwa wakishangilia tangu mwanzo hadi mwisho na wameahidi na kuapa kutotoa kura zao kwa Lowassa!

Alieleza kuwa leo waTanzania wanalipia umeme kwa bei ya juu kutokana na uroho wa Fisadi huyo kwavile Tanesco iliingizwa kwenye mkataba mbovu na pia gharama za mabilioni zilizolipwa kufuatia mkataba mbovu na kesi zilizojiri baada ya mkataba kusitishwa!

Wakati huo huo aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe Mwakipesile, aliyestaafu ameuambia mkutano huo kuwa yeye hawezi kukihama chama cha Mapinduzi kilichomsomesha na kukulia kama mwanachama.

Hii inavunja uongo uliozushwa dhidi yake kuwa kakihama chama hicho na kuhamia UKAWA!

mwakyembe.jpg

"Kwa sasa ninasubiri nione iwapo (kesho) leo wakati wa uzinduzi wa kampeni za Ukawa litagusiwa, nitaweka bayana mambo yote ambayo hayakuongewa bungeni kipindi kile," Dk Mwakyembe

Mbeya
Mgombea ubunge jimbo la Kyela, Dk Harrison Mwakyembe amesema moto wa kashfa ya mkataba wa kufua umeme wa dharura na kampuni ya Richmond haujazimika, hivyo mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa anaweza kufunguliwa "kesi ya magendo".

Dk Mwakyembe, ambaye alikuwa mwenyekiti wa Kamati ya Bunge iliyochunguza sakata la kuipa kampuni hiyo ya Marekani zabuni ya kufua umeme wa dharura mwaka 2008, aliliambia Bunge wakati wa majumuisho ya mjadala kuwa kamati yake haikusoma taarifa kamili ya suala hilo kwa hofu kuwa Serikali nzima ingeondolewa na kuomba uchunguzi mpya ufanyike ili yaibuliwe mengi zaidi.

Lakini miaka saba baada ya kashfa hiyo kuisha kwa Lowassa kujiuzulu uwaziri mkuu, Dk Mwakyembe ambaye ni mwanasheria kitaaluma, ameliibua tena wakati wa kampeni za mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli mjini Kyela.

Akizungumza katika mkutano huo jana, Dk Mwakyembe alisema suala la Richmond lilikuwa limekwisha, lakini anaona kuna watu wanalifungua.

"Kwa sasa ninasubiri nione iwapo (kesho) leo wakati wa uzinduzi wa kampeni za Ukawa litagusiwa, nitaweka bayana mambo yote ambayo hayakuongewa bungeni kipindi kile," alisema Dk Mwakyembe.

"Nimesikia mtu mmoja akisema ‘jamani kama mgombea wa urais wa Ukawa alikuwa na makosa mbona hamkupeleka mahakamani?' Unajua wanasema elimu ndogo ni janga, naomba wote wanisikie mimi ni mwalimu wa sheria, kesi zote za jinai hazina ukomo, acha kuchezea moto kwenye petroli. Tunaweza kufungulia kesi ya magendo, " alisema Dk Mwakyembe kwa ukali na akishangiliwa na wakazi wa Mbeya mjini.

"Chondechonde, atakayekuja kuwa rais (Magufuli) anachukia sana ufisadi na alishatangaza ataunda mahakama maalumu ya mafisadi. Chondechonde, tusiichezee Tanzania, naomba wana-Mbeya kura zote kwa Magufuli."

Wanasheria walonga

Kauli hiyo ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeibua hisia tofauti kutoka kwa wanasheria, huku wakili wa kujitegemea, Semgalawe Charles akikubaliana na kutokuwapo kwa kikomo cha kesi za masuala hayo, lakini akasema Lowassa hakupatikana na hatia wakati ripoti ya Kamati ya Mwakyembe iliposomwa bungeni.

Alisema mahakama na vyombo vingine ndivyo vyenye mamlaka ya kutoa hukumu na endapo kungekuwa na hukumu Lowassa asingepata nafasi ya kugombea urais.

Maoni kama hayo yalitolewa na mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba ambaye alisema wakati ripoti ile ikisomwa, hakukuwa na hukumu badala yake Waziri Mkuu wa kipindi kile aliambiwa ajipime na kujitathmini.

Akizungumza jana, mwanasheria mwingine, Fulgence Masawe alisema tatizo watu wanashindwa kutofauti tuhuma za kisiasa na jinai za mahakama, Lowassa alikuwa na tuhuma za kisiasa na ndiyo maana alijiuzuru.

"Kama ingekuwa ni jinai angechukuliwa hatua mapema hata urais asingeweza kugombea," alisema Masawe.

"Tatizo la nchi hii ni kutochukua maamuzi kwa wakati matatizo yake ndiyo haya. Wanakumbuka shuka kumeshakucha. Lowassa aliwajibika kisiasa siyo jinai. Kama jinai sidhani kama angepata fursa hii anayogombania hivi sasa," alisema Masawe.

CHANZO: Mwananchi(29/08/2015)

Sumaye Na Hiza Wamchefua Mwakyembe Muda Wowote anakinukisha

Habari Iliyonifikia Hivi Punde Tu Ni Kwamba Baada Ya Sumaye Na Richard Tambwe Hiza Jana Kupinga Kwa Nguvu Zao Zote Kuwa Lowassa Siyo FISADI Na Kwamba SAKATA Lile La Richmond Hakuhusika Na Kwamba Tume Ya Akina Dr. Mwakyembe ILIMCHAFUA Tu Sasa Jambo Hili Limechukua Sura Mpya Na Muda Wowote Mwakyembe Ataitisha Press Conference Kueleza UKWELI MTUPU Na Kwa Jinsi Gani Lowassa AMEHUSIKA Na Hawezi KUKWEPA Na Richmond Na Kama Hiyo Haitoshi Habari Za Ndani Kabisa Kuna Uwezekano Muda Na Wakati Wowote Mgombea Urais Wa UKAWA Lowassa AKAKAMATWA Na KUFUNGULIWA Mashitaka Ya Suala Zima La Richmond.

Habari Zaidi Zinazidi Kusema Kwamba Kumbe Hata Jana Wakati Sumaye Na Hiza Wanakaribia Kwenda Pale Kuzungumza Kuna Baadhi Ya Wana Sheria Wa CHADEMA + UKAWA Wenye Akili Waliwaonya Kuwa Hata Kama Wakiwapiga Madongo Wana CCM Ila Wasiligusie Kabisa Hili Suala Kwani Kuna MTEGO Mkubwa Wa KISHERIA Wametegwa Lakini Kwakuwa Sumaye Na Hiza Walikuwa Wanatafuta KIKI Pale Uwanjani WAKAUVAGAA MTEGO Na Sasa Mvua Kamili Ya SAKATA ZIMA LA RICHMOND Inanyesha Muda na Wakati Wowote Kuanzia Sasa. Na Nimeambiwa Kuwa Ktk Hiyo Press Conference Atakuwepo Pia Na Mzee Sitta Na Wajumbe Baadhi.

Kama Ni Picha Nadhani Yale Tuliyoyaona Ktk Ufunguzi Wa Kampeni Za Wiki Iliyoisha Ya CCM Na Ya Jana Ya UKAWA Zote Ni Matrela Tu Sasa Dr. Mwakyembe Anaenda Kuanzisha PICHA KAMILI. Kupayukapayuka Hovyo Kwa Sumaye Na Hiza Jana Jangwani Sasa Kunaenda Kumtokea Puani Lowassa Na Sijui Kama ATATOKA Kisheria Kwani Kuna Wataalam Wa Sheria Hizi Walikuwa Wanapasha Moto Kwanza Ila Jana Akina Sumaye Na Hiza Ndiyo Wamewaambia Waingie Uwanjani Sasa Kucheza.

Na Hapa Ndipo Mtamkubuka Dr. Slaa Na Lipumba. Mbowe Andaa Majibu Ya Kutosha Kwa Wana CHADEMA + UKAWA Wote Kwani UMEWAPONZA Na Sasa Sijui Hata Kama Kampeni Zenu Zitaenda Vizuri Kwani Muda Mwingi Najua Mgombea Wenu Atakuwa Anahudhuria Tu Kesi Mahakamani Na Kuna Uwezekano Pia Kesi Hii Ikaendeshwa Haraka Haraka Na Hukumu Yake Kutolewa Kabla Ya Katikati Ya Mwezi September Na Mtu Akala MVUA Zake 15 Za Kuitia Hasara Jamhuri Na Serikali. Poleni Sana Wana UKAWA Wote Ila Wa Kuwalaumu Ni Sumaye Na Hiza Japo Mapema Sana Jana Walionywa Wasiseme Lolote Kuhusiana Na Sakata Zima La Richmond.

Ndiyo Maana Sipendi SIASA Na Sina Chama Chochote Ninachokishabikia Japo Kwa Mbali Sana Nakipenda Chama Cha CHAUSTA.

Nafasi ya Urais sio nafasi ya kupata "kama zari".

Hata uwe kiongozi mzuri kiasi gani huwezi kushtukizwa na kupewa mikoba ya nchi kirahisi rahisi tu.

Lazima uwe umejipanga, umejiandaa na uko tayari.

Hotuba za Magufuli zinadhihirisha kuwa aliingia kwenye kinyang'anyiro kwa kujaribu. Membe alitangaza nia Lindi, Makamba alitangaza nia Mlimani City, Muhongo- Musoma, Mh.Lowassa;Arusha n.k.

Magufuli alitangaza nia wapi? Alitaja vipaumbele gani? Nini kauli mbiu yake? HAKUNA. Huwezi kumpa mtu 'miaka 5 ya kujiandaa' kuongoza nchi. Tunataka mtu aliyejiandaa an akiingia ikulu aanze kuongoza nchi mara moja. Kuna tofauti kubwa kati ya Magufuli na Lowassa.

Wote ni wepesi katika kufanya maamuzi. Lakini mmoja hufanya maamuzi yenye tija wakati mwingine hufanya maamuzi yenye madhara.

Tuangalie mifano: Mh.Magufuli 'alipiga' bei nyumba za serikali na leo hii serikali inatumia mamilioni kuwapangishia hotelini watumishi wake.HASARA!
✔Mh.Lowassa amesimamia ujenzi wa UDOM na kuongeza idadi ya wataalam mbalimbali nchini.FAIDA.

Ndg.Makufuli amenunua vivuko, pantoni na mashine za tiketi kwa mabilioni lakini hazifanyi kazi/ hazina ufanisi.HASARA.
✔Mh.Lowassa alisimamia ujenzi wa bomba la maji kutoka ziwa Victoria mpaka Shinyanga huku akipuuzia vitisho vya Wasudani na Wamisri vya kuhodhi matumizi ya maji ya Victoria kwa mkataba wa kikoloni.FAIDA.

Mh.Magufuli alibomoa fuel station "shell" huko Mwanza, serikali ikashindwa kesi, tukalipa mabilioni.HASARA.
✔Mh.Lowassa alivunja mkataba wa City Water, hatukushtakiwa.FAIDA.

Mh.Magufuli alikamata wavuvi "halali" tumeshitakiwa, tumedondokea pua, tutawalipa meli yao na gharama nyingine kadhaa, hapo hujajumlisha gharama za utunzaji wa wale samaki.HASARA.
✔Mh.Lowassa, wakati ndege za Malawi zishaanza kuzurura maeneo ya Kyera na Nyasa huku tukiwachekea, alitoa tamko Bungeni...."tuko imara, tumejipanga...". Wakafunga Virago.FAIDA.

Ndg.Magufuli amewanyang'anya kandarasi wajenzi kadhaa kwa matamko tu bila kuzingatia taratibu za mikataba. Wametushtaki, wameshinda, tumewalipa.HASARA.
✔Mh.Lowassa alitaka kuvunja mkataba wa Richmond, kama sio AG Johnson Mwanyika kuomba..."mapumzik ya saa moja nje ya mkutano" ili awasiliane na mamlaka ya juu na baadae kurejea na agizo kuwa..."imeagizwa; mkataba usivunjwe.." pengine leo tusingekuwa tunazungumzia Richmond, baba yake na Dowans, babu wa Symbion Powers. TUNGENUFAIKA. UCCM wangu hauwezi kunipofua nisiuone ukweli huo hapo juu. Ujirani wangu na Mh.Magufuli hapa Chato hauwezi kunishinikiza nimuazime miaka 5 ya kujiandaa badala ya kutawala. NITAMPIGIA LOWASSA. Sambaza Kw watu 20 Kw SMS, Whatsapp.Twitter, Facebook, Instragram nk.
 
Mhe Mwakyembe amkaanga Lowassa kuhusu kadhia ya Richmond na kusema kuwa asikwepe maana tume ya Bunge ilimkuta na hatia na ikabidi ajiuzulu Uwaziri Mkuu. Ameeleza hayo kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais kupitia CCM Mhe JPM leo huko Kyela katika mfululizo wa kampeni za mgombea huyo. Mhe Mwakyembe kaeleza kadhia hiyo kwa maelfu ya wananchi waliokuwa wakishangilia tangu mwanzo hadi mwisho na wameahidi na kuapa kutotoa kura zao kwa Lowassa! Alieleza kuwa leo waTanzania wanalipia umeme kwa bei ya juu kutokana na uroho wa Fisadi huyo kwavile Tanesco iliingizwa kwenye mkataba mbovu na pia gharama za mabilioni zilizolipwa kufuatia mkataba mbovu na kesi zilizojiri baada ya mkataba kusitishwa!
Wakati huo huo aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe Mwakipesile, aliyestaafu ameuambia mkutano huo kuwa yeye hawezi kukihama chama cha Mapinduzi kilichomsomesha na kukulia kama mwanachama. Hii inavunja uongo uliozushwa dhidi yake kuwa kakihama chama hicho na kuhamia Ukawa!

huyu msomi anajidhalilishe kwa sababu ya tumbo gharama ya umeme inasababishwa na IPTL ambayo imezaa escrow na Lowasa ameshasema kuwa alizuiwa na mamlaka ya juu na haingii akilini kuwa Lowasa ndio amesababisha haya yote kwani kulikuwa hakuna Rais ?
na huyo mwakipesile asitudanganye ccm ilianza mwaka 1977 yeye kasomeshwa enzi za tanu tena na kodi za watanzania na sio ccm
sasa hivi watanzania sio wapumbavu kama wanavyofikiria na hatudanganyiki tena

mwakyembe nae atuambie kuhusu mabehewa feki aliyoyaagiza toka india
 
MH. MWAKYEMBE AMLIPUA LOWASSA.

Mhe Mwakyembe amkaanga Lowassa kuhusu kadhia ya Richmond na kusema kuwa asikwepe maana tume ya Bunge ilimkuta na hatia na ikabidi ajiuzulu Uwaziri Mkuu. Ameeleza hayo kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais kupitia CCM Mhe JOHN POMBE MAGUFULI leo huko Kyela katika mfululizo wa kampeni za mgombea huyo. Mhe Mwakyembe kaeleza kadhia hiyo kwa maelfu ya wananchi waliokuwa wakishangilia tangu mwanzo hadi mwisho na wameahidi na kuapa kutotoa kura zao kwa Mzee Lowassa!

Alieleza kuwa leo watanzania wanalipia umeme kwa bei ya juu kutokana na uroho wa Fisadi huyo kwavile Tanesco iliingizwa kwenye mkataba mbovu na pia gharama za mabilioni zilizolipwa kufuatia mkataba mbovu na kesi zilizojiri baada ya mkataba kusitishwa!

Wakati huo huo aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe Mwakipesile, aliyestaafu ameuambia mkutano huo kuwa yeye hawezi kukihama chama cha Mapinduzi kilichomsomesha na kukulia kama mwanachama.

Hii inavunja uongo uliozushwa dhidi yake kuwa kakihama chama hicho na kuhamia Ukawa!

CCM NI KAZI TU: UMOJA NI USHINDI.
 
Nafasi ya Urais sio nafasi ya kupata "kama zari".

Hata uwe kiongozi mzuri kiasi gani huwezi kushtukizwa na kupewa mikoba ya nchi kirahisi rahisi tu.

Lazima uwe umejipanga, umejiandaa na uko tayari.

Hotuba za Magufuli zinadhihirisha kuwa aliingia kwenye kinyang'anyiro kwa kujaribu. Membe alitangaza nia Lindi, Makamba alitangaza nia Mlimani City, Muhongo- Musoma, Mh.Lowassa;Arusha n.k.

Magufuli alitangaza nia wapi? Alitaja vipaumbele gani? Nini kauli mbiu yake? HAKUNA. Huwezi kumpa mtu 'miaka 5 ya kujiandaa' kuongoza nchi. Tunataka mtu aliyejiandaa an akiingia ikulu aanze kuongoza nchi mara moja. Kuna tofauti kubwa kati ya Magufuli na Lowassa.

Wote ni wepesi katika kufanya maamuzi. Lakini mmoja hufanya maamuzi yenye tija wakati mwingine hufanya maamuzi yenye madhara.

Tuangalie mifano: Mh.Magufuli 'alipiga' bei nyumba za serikali na leo hii serikali inatumia mamilioni kuwapangishia hotelini watumishi wake.HASARA!
✔Mh.Lowassa amesimamia ujenzi wa UDOM na kuongeza idadi ya wataalam mbalimbali nchini.FAIDA.

Ndg.Makufuli amenunua vivuko, pantoni na mashine za tiketi kwa mabilioni lakini hazifanyi kazi/ hazina ufanisi.HASARA.
✔Mh.Lowassa alisimamia ujenzi wa bomba la maji kutoka ziwa Victoria mpaka Shinyanga huku akipuuzia vitisho vya Wasudani na Wamisri vya kuhodhi matumizi ya maji ya Victoria kwa mkataba wa kikoloni.FAIDA.

Mh.Magufuli alibomoa fuel station "shell" huko Mwanza, serikali ikashindwa kesi, tukalipa mabilioni.HASARA.
✔Mh.Lowassa alivunja mkataba wa City Water, hatukushtakiwa.FAIDA.

Mh.Magufuli alikamata wavuvi "halali" tumeshitakiwa, tumedondokea pua, tutawalipa meli yao na gharama nyingine kadhaa, hapo hujajumlisha gharama za utunzaji wa wale samaki.HASARA.
✔Mh.Lowassa, wakati ndege za Malawi zishaanza kuzurura maeneo ya Kyera na Nyasa huku tukiwachekea, alitoa tamko Bungeni...."tuko imara, tumejipanga...". Wakafunga Virago.FAIDA.

Ndg.Magufuli amewanyang'anya kandarasi wajenzi kadhaa kwa matamko tu bila kuzingatia taratibu za mikataba. Wametushtaki, wameshinda, tumewalipa.HASARA.
✔Mh.Lowassa alitaka kuvunja mkataba wa Richmond, kama sio AG Johnson Mwanyika kuomba..."mapumzik ya saa moja nje ya mkutano" ili awasiliane na mamlaka ya juu na baadae kurejea na agizo kuwa..."imeagizwa; mkataba usivunjwe.." pengine leo tusingekuwa tunazungumzia Richmond, baba yake na Dowans, babu wa Symbion Powers. TUNGENUFAIKA. UCCM wangu hauwezi kunipofua nisiuone ukweli huo hapo juu. Ujirani wangu na Mh.Magufuli hapa Chato hauwezi kunishinikiza nimuazime miaka 5 ya kujiandaa badala ya kutawala. NITAMPIGIA LOWASSA. Sambaza Kw watu 20 Kw SMS, Whatsapp.Twitter, Facebook, Instragram nk.

Hilo jizi ccm nu hata mlibebe kwa mbeleko ya misumari mnashindwa asubuhi kweupeeeee
 
Mhe Mwakyembe amkaanga Lowassa kuhusu kadhia ya Richmond na kusema kuwa asikwepe maana tume ya Bunge ilimkuta na hatia na ikabidi ajiuzulu Uwaziri Mkuu.

Ameeleza hayo kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais kupitia CCM Mhe JPM leo huko Kyela katika mfululizo wa kampeni za mgombea huyo. Mhe Mwakyembe kaeleza kadhia hiyo kwa maelfu ya wananchi waliokuwa wakishangilia tangu mwanzo hadi mwisho na wameahidi na kuapa kutotoa kura zao kwa Lowassa!

Alieleza kuwa leo waTanzania wanalipia umeme kwa bei ya juu kutokana na uroho wa Fisadi huyo kwavile Tanesco iliingizwa kwenye mkataba mbovu na pia gharama za mabilioni zilizolipwa kufuatia mkataba mbovu na kesi zilizojiri baada ya mkataba kusitishwa!

Wakati huo huo aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe Mwakipesile, aliyestaafu ameuambia mkutano huo kuwa yeye hawezi kukihama chama cha Mapinduzi kilichomsomesha na kukulia kama mwanachama.

Hii inavunja uongo uliozushwa dhidi yake kuwa kakihama chama hicho na kuhamia UKAWA!

Siasa.za kupakana matope azisaidii,watu wakiamua wameamua tuu uwezi kuwabadili,,Sawa alifanya Kosa miaka 8 iliyopita,mbona mpk leo umeme wa mgao,na hayo manjanga mengine ya rushwa kipindi yeye hayupo serikalini..?? ..wajipange CCM
 
BREAKING NEWS.

MH. MWAKYEMBE AMLIPUA LOWASSA.
Mhe Mwakyembe amkaanga Lowassa kuhusu kadhia ya Richmond na kusema kuwa asikwepe maana tume ya Bunge ilimkuta na hatia na ikabidi ajiuzulu Uwaziri Mkuu. Ameeleza hayo kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais kupitia CCM Mhe JOHN POMBE MAGUFULI leo huko Kyela katika mfululizo wa kampeni za mgombea huyo. Mhe Mwakyembe kaeleza kadhia hiyo kwa maelfu ya wananchi waliokuwa wakishangilia tangu mwanzo hadi mwisho na wameahidi na kuapa kutotoa kura zao kwa Mzee Lowassa!
Alieleza kuwa leo watanzania wanalipia umeme kwa bei ya juu kutokana na uroho wa Fisadi huyo kwavile Tanesco iliingizwa kwenye mkataba mbovu na pia gharama za mabilioni zilizolipwa kufuatia mkataba mbovu na kesi zilizojiri baada ya mkataba kusitishwa!
Wakati huo huo aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe Mwakipesile, aliyestaafu ameuambia mkutano huo kuwa yeye hawezi kukihama chama cha Mapinduzi kilichomsomesha na kukulia kama mwanachama.
Hii inavunja uongo uliozushwa dhidi yake kuwa kakihama chama hicho na kuhamia Ukawa!
CCM NI KAZI TU: UMOJA NI USHINDI.

He ve he heee sasa hii nayo habari wadau..wote tushajua richmondi ni nani...lowasa kaweka mambo wazi na mkichokonoa kesho patachimbika jangwani
 
Back
Top Bottom