Dr. Mwakyembe na Powerpool: Kuna mgongano wa maslahi na Dowans/Richmond? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Mwakyembe na Powerpool: Kuna mgongano wa maslahi na Dowans/Richmond?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kachanchabuseta, Nov 25, 2011.

 1. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #1
  Nov 25, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  [h=2][​IMG] Dr. Mwakyembe na Powerpool: Kuna mgongano wa maslahi na Dowans/Richmond?[/h]
  Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania Toleo No. 4689 la tarehe 15 Machi 2009 chini ya kichwa cha habari "Dk. Mwakyembe Aumbuliwa" imeripotiwa kuwa Dk. Harrison Mwakyembe ni mmoja wa wamiliki wa kampuni ya kufua umeme na ndio sababu anaipiga vita kampuni ya Dowans ambayo ni mshindani wa kampuni yake. Nukuu ya vipande vya taarifa hiyo ya Mtanzania ni kama ifuatavyo:-

  "SIRI nzito za kimaslahi zinazomhusu Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM, pichani) zimeanza kuibuliwa.

  Imebainika kuwa Mbunge huyo ni miongoni mwa watu tisa wenye hisa katika kampuni binafsi ya kufua umeme kwa kutumia nguvu za upepo.

  Kampuni hiyo inaitwa Powe Pool East Africa Limited. Namba zake za usajili ni 49624. Makao Makuu yapo katika majengo ya Posta ya Zamani jijini Dar es Salaam. Aidha kampuni hiyo imeishapata maeneo ya kuwekeza - Makambako mkoani Iringa na Singida. Maeneo hayo yana upepo mkali amabo ndiyo malighafi muhimu.

  Wachunguzi wa mambo wanaamini kuwa ushujaa wa Dk. Mwakyembe kuishambulia kampuni ya Richmond, na baadaye Dowans, unatokana na mgongano wa kimaslahi.

  Kwa maneno mepesi, wanasema Dk. Mwakyembe na wenzake wanapinga Dowans kununuliwa ili wapate mwanya wa kuuza umeme utakaozalishwa na kampuni yao ya Power Pool East Africa Limited, ingawa nao kwa vyovyote vile utakuwa haujatosheleza mahitaji ya umeme nchini.

  Dk. Mwakyembe na wenzake walianzisha kampuni yao kabla ya ujio wa kampuni iliyozua utata mkubwa wa Richmond. Matarajio yao yalikuwa kwamba wazalishe umeme na kisha waiuzie Tanesco, lakini ujio wa Richmond ulionekana kutaka kuwakwaza. Richmond ilisababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, ajiuzulu Februari mwaka jana.

  Akiwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza Richmond, hakuwahi kutangaza hata mara moja mgongano wa kimaslahi aliokuwa nao kwenye suala hilo.

  Pamoja na Dk. Mwakyembe anayemiliki hisa 1,485 katika kampuni hiyo, wengine wenye hisa katika kampuni hiyo ni Emmanuel Kasyanju (99), Victor Mwambalaswa (99), Mwacha Kagoswe (4,455), Josephine Pina (99), Athumani Ngwilizi (99), Prosper Tesha (99), TBC (199 Limited inayomilikwa na Isaac Mwamango (297) na MECCO Limited, inayomilikwa na Maungo Kwabibi hisa moja.

  Kwa hisa hizo Dk. Mwakyembe ni mtu wa pili kwa maamuzi katika kampuni hiyo, kwani kwa mujibu wa kanuni za makampuni, nguvu na uwezo wa mtu hutokana na hisa zake. Mwenye hisa nyingi ni Machwa Kasogwe.

  Wengine ni Beston Mwakalinga (99) Niels Dahlmann (891) na Leonard Tenende (99).

  Wanahisa wote, isipokuwa watatu, anuani zao zinaonyesha kuwa wako nje ya nchi..........

  Dk. Mwakyembe, akionekana kuwa msitari wa mbele kuhakikisha kuwa mitambo ya kampuni ya Dowans hainunuliwi, anashupalia msimamo huo kutokana na mgongano wa maslahi. Aliwahi kusikika akisema kuwa ni heri nchi iingie gizani , hoja iliyowafanya watu wengine kusema kwama alistahili kukamatwa.

  Katika Power Pool East Africa, Mbunge huyo anamiliki hisa 1,485, lakini anaweza kuwa na hisa nyingine zaidi kupitia kampuni zake mbili tofauti. Kupitia kampuni ya kwanza ya TBC (199 Limited amabyo anamiliki hisa 297 na kampuni nyingine ya MECCO limited ana hisa moja."

  (Taarifa inaendelea lakini ya muhimu kuhusu Dk. ni hayo) inserted by Invisible

  SOurce: tk was JF

  More:https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/25691-dr-mwakyembe-na-powerpool-kuna-mgongano-wa-maslahi-na-dowans-richmond-11.html
   
 2. g

  greenstar JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 390
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  so boring,,,,,ile ilikuwa Kamati Teule ya Bunge na siyo Mwakyembe...............mtu akisimamia sheria anabatizwa jina lake? ona hata Dr.Magufuli akisimamia sheria anaoneka ni yeye binafsi....Tanzania ni nchi ambayo haina watu makini kwa kupenda ushabiki....tazama sasa hivi watu wanashabikia maandamano bila kujua wanacho kitaka......Tanzania itaendelea kunufaisha wageni.Good example Quality Center imejaa kampuni za wakenya hadi Waziri Mkuu wao ndiyo mgeni rasmi ktk uzinduzi utakaofanyika Kesho.


  :smash:Naombeni support naanzisha chama cha kisiasa......A New Hope For Tanzanians
   
Loading...