Dr Mengi na prof Muhongo tumechoshwa na malumbano yenu hayana tija kwa taifa ni vyema mkakaa chini

Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
47,862
2,000
Mwanzo wa malumbano kati ya Dr Mengi na Prof .Muhongo wengi tulifikiri yana lengo la kujengana na kulisukuma gurudumu la maendeleo mbele.

Ni kawaida kabisa watu kutofautiana kwa hoja na mitazamo na pengine kwa watu kama Mengi na Muhongo vyovyote vile tungependa malumbano yao hasa kwa hoja yawe yenye kujengana zaidi na kuhakikisha wanarekebishana na kufikia muafaka hili kutimiza malengo ya kuleta maendeleo kwenye nchi yetu.

Ni aibu sana kwa watu wenye umri kama wa wakina Muhongo na Mengi kutumia muda mwingi kulumbana kuliko kufikiria kulijenga taifa kwa nafasi zao.

Pengine lazima watanzania wataamini kabisa wote mmeshindwa kutimiza majukumu yenu ipasavyo na mmejikita kwenye malumbano na kila mmoja akiwaza nini mwenzie ataongea na nini atamjibu, mnaonekana kutumia muda mwingi kufikiri jinsi ya kulumbana badala ya kufikiri kutatua matatizo ya watanzania kwa nafasi zenu.


Bila shaka wengi tulifikiri malumbano yenu yangefika tamati ya kukaa chini pamoja na kuelekezana na kukubaliana katika hoja zenu kuliko mnavyo fanya sasa.

Imefikia wakati watu wakisikia Mengi au Muhongo ataongea wanafikiria malumbano yenu badala ya nafasi zenu katika jamii.

Pengine nyote mmekosa washauri wazuri na kama wangekuwepo haya malumbano yenu yasingekuwepo hadi sasa,pengine wana washauri kushindana badala ya kuwashauri kutumia busara kulingana na umri wenu.

Ni aibu na ni hasara kwa taifa kuwa na wasomi na wafanya biashara ambao hawako tayari kukaa chini pamoja na kukubaliana,kurekebishana na kumaliza tofauti zao katika hoja.

Ni wazi kila mtu anatafuta kuwa mshindi kwa mwenzie lakini msisahau kuwa malumbano yenu hayato leta manufaa au maendeleo kwa nchi yetu.

Ifike wakati muoneshe busara zenu na utu uzima wenu kwa vitendo.Ni watanzania wachache ambao wana kumbuka nini kina wafanya mlumbane.

Kama wote mnapigania maslai ya taifa kwanin msikae chini nakuzungumza kama watu wapenda maendeleo kwa nchi yao?


MUHONGO NA MENGI KAENI CHINI MMALIZE TOFAUTI ZENU AU MKUBALIANE KUTO KUKUBALIANA KULIKO HAYA MALUMBANO YENU.
 

mwa 4

JF-Expert Member
Oct 8, 2013
3,392
1,250
mengi alizoea kuburuza watu sasa kawaa kisiki mzee kazoea kuibia watanzania.
 

Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
47,862
2,000
mengi alizoea kuburuza watu sasa kawaa kisiki mzee kazoea kuibia watanzania.

ok haya malumbano yao yana faida gani kwa taifa? Kwanini wasitumie busara kumaliza haya?kwanini mmoja mwenye busara kumshinda mwenzie asizitumie na zikaonekana?
 

Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
47,862
2,000
thanx bro. I stand with you.
Lakini mengi ni mfanyabiashara na wafanyabiashara wanathamini kitu kimoja tuu......faida

pamoja na madhaifu ya wote wawili lakini wafike hatua wajue wana lengo gani kwa taifa kama wanavyo sema.

Hakuna mkamilifu kati yao lakini bila shaka wanaweza kukaa chini wakatafakari na kujadili pamoja kuliko kulumbana.
 

Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
47,862
2,000
Nilisha washauri sana hawa jamaa wawili kuwa malumbano yao haya tusidii na hakuna kati yao anaye taka kumsikiliza au kumuelewa mwenzake na wote wana jaribu kutuonesha kuwa upande fulani una muonea.

Hawa malumbano yao hayana maslai ya taifa na wanatakiwa kujua si lazima kila mtu apate anacho taka.

Waangalie wasigeuze bajeti ya ni shati na madini ya kuzungumzia maswla yao.
Na bahati mbaya kuna baadhi ya watu wana taka kulikuza hili jambo.
 

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
41,211
2,000
hii ni fursa nzuri kwa mwanasiasa anayekubalika kuchukuwa ubunge wa jimbo hilo mwakani kwa ufadhiri wa mengi.

huyu muhongo hajajifunza kwa masha na masilingi.
 

Vladmir

Senior Member
Apr 14, 2014
178
0
Mengi ni mbinafsi wa kuptitiliza ,hayupo kwa ajili ya watanzania na hiyo ndiyo tofauti ya Muhongo na Mengi anataka kila jambo apate yeye, na serikali ifuate analotaka . Hana nafasi hata kama ana fedha kiasi gani, amefanyia nchi kitu gani kama si kutafuta maendeleo ya binafsi.

Tunataka serikali itumie nguvu kubwa kuboresha TPDC iwe na nguvu na huko wananchi tutapata ajira kuliko kwa mengi ambaye halipi mishahara na ubaguzi uliomjaa.

Pamoja na juhudi zake zote Mzee mengi za kununua wanahabari , Wabunge mbalimbali na wachimbaji wadogo hatafaulu wananchi tunamfahamu siku nyingi hafai katika taifa hili.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom