Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,206
- 42,068
Mwanzo wa malumbano kati ya Dr Mengi na Prof .Muhongo wengi tulifikiri yana lengo la kujengana na kulisukuma gurudumu la maendeleo mbele.
Ni kawaida kabisa watu kutofautiana kwa hoja na mitazamo na pengine kwa watu kama Mengi na Muhongo vyovyote vile tungependa malumbano yao hasa kwa hoja yawe yenye kujengana zaidi na kuhakikisha wanarekebishana na kufikia muafaka hili kutimiza malengo ya kuleta maendeleo kwenye nchi yetu.
Ni aibu sana kwa watu wenye umri kama wa wakina Muhongo na Mengi kutumia muda mwingi kulumbana kuliko kufikiria kulijenga taifa kwa nafasi zao.
Pengine lazima watanzania wataamini kabisa wote mmeshindwa kutimiza majukumu yenu ipasavyo na mmejikita kwenye malumbano na kila mmoja akiwaza nini mwenzie ataongea na nini atamjibu, mnaonekana kutumia muda mwingi kufikiri jinsi ya kulumbana badala ya kufikiri kutatua matatizo ya watanzania kwa nafasi zenu.
Bila shaka wengi tulifikiri malumbano yenu yangefika tamati ya kukaa chini pamoja na kuelekezana na kukubaliana katika hoja zenu kuliko mnavyo fanya sasa.
Imefikia wakati watu wakisikia Mengi au Muhongo ataongea wanafikiria malumbano yenu badala ya nafasi zenu katika jamii.
Pengine nyote mmekosa washauri wazuri na kama wangekuwepo haya malumbano yenu yasingekuwepo hadi sasa,pengine wana washauri kushindana badala ya kuwashauri kutumia busara kulingana na umri wenu.
Ni aibu na ni hasara kwa taifa kuwa na wasomi na wafanya biashara ambao hawako tayari kukaa chini pamoja na kukubaliana,kurekebishana na kumaliza tofauti zao katika hoja.
Ni wazi kila mtu anatafuta kuwa mshindi kwa mwenzie lakini msisahau kuwa malumbano yenu hayato leta manufaa au maendeleo kwa nchi yetu.
Ifike wakati muoneshe busara zenu na utu uzima wenu kwa vitendo.Ni watanzania wachache ambao wana kumbuka nini kina wafanya mlumbane.
Kama wote mnapigania maslai ya taifa kwanin msikae chini nakuzungumza kama watu wapenda maendeleo kwa nchi yao?
MUHONGO NA MENGI KAENI CHINI MMALIZE TOFAUTI ZENU AU MKUBALIANE KUTO KUKUBALIANA KULIKO HAYA MALUMBANO YENU.