Dr. Mary Mwanjelwa amekanusha vikali kuwa anataka kuhamia CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Mary Mwanjelwa amekanusha vikali kuwa anataka kuhamia CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by wagagagigikoko, May 7, 2012.

 1. wagagagigikoko

  wagagagigikoko Senior Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hiki kinajulikana wazi kuwa ni chakula cha mkubwa ahame aende wapi, huku CDM watu wa kazi hatupeana uongozi kama pipi. na mwisho wa huyu ni siku mkuu wa nchi ametoka madarakani.

  hii ndio taarifa kamili ya kilichojili kwenye kikao

  MBUNGE WA VITI MAALUM (CCM) MKOA WA MBEYA DR. MARY MWANJELWA AMEKANUSHA VIKALI KUWA ANATAKA KUHAMIA CHADEMA ASEMA YEYE NA CCM DAMU DAMU TOKA KITAMBO

  [TABLE]
  [TR]
  [TD][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]MBUNGE wa viti maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mbeya Dr.Mary Mwanjelwa amekanusha uvumi ulioripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini kuwa anatarajia kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

  Alisema taarifa hizo ni uzushi na uongo kwa sababu yeye ni kada wa CCM wa siku nyingi ambaye amepewa dhamana na chama hicho kugombea ubunge kupitia jumuiya ya wanawake hivyo hatarajii kuwageuka kwa sababu bado anayo dhamana ya kuendelea kuwa Mbunge.

  Alisema, taarifa hizo zimenishtua sana, na hata wapiga kura wangu nao wamepata mshtuko mkubwa na wakanipigia simu ili kutaka kupata ukweli kutoka kwangu hivyo nimeona ni vizuri nitoe ufafanuzi.

  Alisema yeye ni mbunge wa wananchi wote mkoani hapa, hana matatizo yeyote na chama hivyo haielewi sababu za kumfanya ahame chama chake na kujiunga na CHADEMA, kwa sababu ya uteuzi wa baraza jipya la mawaziri.

  "Mimi ni mbunge kwa tiketi ya CCM na pia ni kada wa chama ambacho ndicho kilichonipitisha kugombea nafasi ya ubunge viti maalumu, na hatimaye nikafanikiwa kuchaguliwa sasa iwaje leo nikihame chama,"alihoji Mbunge huyo.

  Aliongeza habari zilizoripotiwa ni za uongo, na kuwa kamwe hawezi kuingilia uteuzi wa Rais Kikwete katika kuwateua mawaziri, kwani hayo ni mambo ambayo hayamhusu kabisa.

  Dk.Mary alisema yeye amekwenda Bungeni kuwawakilisha wananchi wa mkoa wa Mbeya, sikwenda Bungeni kwa sababu ya kutaka kuwa Waziri, hizo ni nafasi za uteuzi na mwenye mamlaka hiyo ni Rais Kikwete.

  Mbunge huyo wa viti maalum Mbeya, aliongeza hivyo ni vyema waandishi wa habari waache kuandika habari za kuchafuana, kuharibiana bali wafuate misingi na maadiri yanayolinda tasnia ya habari.

  Alisema iwapo mwandishi anakuwa amepata taarifa ni vyema amfuate muhusika ili kupata ukweli juu ya habari anayotaka kuiandika iwapo ina ukweli wowote ndani yake.

  Aliongeza kama hayo yalikuwa ni maoni ya wananchi, anashindwa kuelewa yeye anaingizwaje katika habari hiyo, kwani ana mkataba wa kuwatumikia wananchi kwa miaka mitano na amebakiza miaka mitatu.

  "Siwezi kuhamia CHADEMA, kwani CCM haijanifanyia kosa lolote, sikwenda Bungeni ili niteuliwe kuwa Waziri, kikubwa kwangu ni kuingia Bungeni kwa ajili ya kuwawakilisha wananchi wangu wa mkoa wa Mbeya" alisema Dk.Mary.

  Kwa mujibu wa Mwanjelwa alisema kuwa ni kweli alizungumza na Mwandishi aliyeandika habari hizo na kwamba mwandishi huyo alikuwa akitaka kupata ufafanuzi wa uvumi ulioenea ya kwamba kuna baadhi ya wananchi wanataka kwenda kumuona ili wamshawishi akihame chama kwa sababu ya Rais hakumteua kwenye Baraza jipya la Mawaziri.

  "Mimi nilimjibu mwandishi huyo ya kwamba huo ni mtazamo wa wananchi lakini si wa kwangu "alisema Mwanjelwa huku akisisitiza kuwa hicho ni kipindi chake cha kwanza kuingia Bungeni sasa iwaje ashikwe na tamaa ya kutaka kushika madaraka ya juu .

  Hata hivyo, alisema atagombea tena nafasi hiyo kupitia Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), ili wanawake wampe tena kura zao kwani anajijua bado anafaa zaidi ya kufaa, hivyo atajitokeza katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015 kutetea nafasi yake hiyo kwa tiketi ya Chama cha mapinduzi..

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. denoo49

  denoo49 JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 5,647
  Likes Received: 5,237
  Trophy Points: 280
  akipokuwa anasema "hata wapiga kura wake wamepata mshtuko mkubwa" alikuwa anamaanisha nini??
   
 3. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  Haya ndo magarasa pia si ajabu pia ni kawaida kwa wabunge walopata nafasi kwa njia ya mbeleko,
  pia kuna siku atajilaumu kwa kuipuuza hii nafasi haba ya kuamia chadema.
  Mama jivunie tu kuwa mwanachama wa chama cha mafisadi pia chama magamba
   
 4. kivyako

  kivyako JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 8,795
  Likes Received: 4,155
  Trophy Points: 280
  Gamba hilo, alijisahau alifikiri alichaguliwa na wananchi kumbe kawezeshwa!
   
 5. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,866
  Trophy Points: 280
  Ukishakuwa Gamba hata uwezo wa kufikiri unapotea, huyu si viti maalumu? Au vitu maalumu nao wanachaguliwa siku hizi?:nerd:
   
 6. Kapo Jr

  Kapo Jr JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 935
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 60
  Wakuu si ndo aliekwapua hotel kule Arusha,chakula yake nadhani katekenywa karainika
   
 7. wagagagigikoko

  wagagagigikoko Senior Member

  #7
  May 7, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Akula ya mkuu huyu kazaa naye mkuu wa nchi haendi popote
   
 8. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Kazaa na mkulu mtoto wa kiume!alikuwa mda mrefu sana huko Malaysia
   
 9. Arushaone

  Arushaone JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 14,351
  Likes Received: 612
  Trophy Points: 280
  Nimeshtuka sana kama mkuu wa kaya kazaa na huyo mama, ingawa siyo huko tu hata hapa kwetu anao! Nadhani ni wakati sasa awe muwazi kama wenzake kina Zuma na Mswati... Kingine kilichonishtua ni majibu rahisi kwa swali la msingi kama hilo. Sijui CCM wanaendesha nchi kwa kufikiri kwa kutumia nini...
   
 10. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  naomba tumpigie mkulu makofi (tumpashie!)kwa urijali wake wa hali ya juu...maana naona kila siku tunasikia kazaa na fulani kazaa na fulani...Big up Mkulu...keep up the good work of overflooding the world! Hakika unatimiza ule usemi wa mwenyezi Mungu usemao...''Enendeni mkaijaze dunia''
   
 11. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  vitu maalum! sio vitu ni viti.
   
 12. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  tehe tehe tehe tehe we baki hukohuko tu,hiyombeya tuna kuja kuiteka cc CDM hatutataka kuiona bendera ya jembe na nyundo hata moja
   
 13. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #13
  May 8, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  MMMhhh Malaysia ya wapi?? uongo mtupu hata cv yake yenyewe kachakachua!!
   
 14. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #14
  May 8, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Wapiga kura wa VITI MAALUM?
   
 15. D

  Dina JF-Expert Member

  #15
  May 8, 2012
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Sahihisho kwenye 'heading', nafikiri ilitakiwa kuwa Mary na si Tabia, kwani Tabia alikuwa mama mtu.
   
 16. Nyati

  Nyati JF-Expert Member

  #16
  May 8, 2012
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 2,037
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180
  Mama yake ni yule aliyekuwa mwanamziki wa Maquiz miaka ya 1990?!!! ama mwingine?
   
 17. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #17
  May 8, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Makubwa haya..
   
 18. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #18
  May 8, 2012
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Yeah,ni yule aliyeimba wimbo wa Jua...Jua la asubuhi lapendeza,jua la asubuhi lavutiaaa,jua jua jua juaaa....
   
 19. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #19
  May 8, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
   
 20. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #20
  May 8, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,317
  Likes Received: 2,604
  Trophy Points: 280
  itakua hao waliompitisha huko kwenye umoja wa wanawake
   
Loading...