Dr. Levy Anena Juu Ya Wema Sepetu.

Mwananchi wa chini

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
227
597
30 years now. Unafanya upuuzi uliofanya ukiwa na miaka 20. Unajirekodi faragha na bwanaako mkilambana ndimi kibwege. Unasambaza mitandaoni. Unasubiri uone mihemko ya watu, kisha unaita waandishi na kuomba radhi.

Na hii siyo mara ya kwanza kufanya upuuzi huo. Na kuna mazuzu wengi wanaokusifia, kukutetea, na kuwatukana wale wanaokukosoa. Hukui kiakili. Hutaki kuonekana mtu mzima. Unauchukia uzee. Hutulii na hutaki kukubaliana na ukweli ulio wazi kwamba umepitwa na muda. Hutaki kuamini kuwa umeshindwa kila kitu.

Kuendelea kukupa moyo ni makosa. Tutakupoteza zaidi. Ni bora tuwe wakweli kwenye hili, kwamba sasa unahitaji siyo tu kubadili tabia bali kubadili mpaka jina lako. Maana haliendani na matukio yako, siyo kwa umaarufu wake bali kwa maana halisi ya jina lenyewe. Umevuka daraja la kufanyiwa maombezi.

Umeua brand yako. Umeua biashara zako. Sasa unataka kuua na ndugu zako. Wanaoteseka ni ndugu waliokuwa na wewe siku zote na watakuwa na wewe mpaka unakufa. Utatengwa na boyfriend, shost na wasanii. Lakini ndugu utakuwa nao mpaka unaoza. Na hao ndiyo unaowaua taratibu kwa hayo unayofanya.

Ukipoteza muda ukajiuliza na kutafakari. Utagundua ni wewe uliyebaki kama 'misheni town' wa kike. Wale wote Waliokuzunguka wana maisha yao mpaka mawifi zako wa kale na wapya. Wewe uko 'bize' na mizuka ya insta. Unataka 'kutrend' siyo? Yaani kutoka kuigwa na madem wa mjini mpaka wewe kuwaiga kina Amber Rutty?

Unaweza kuwa umezoea 'skendo' na maneno ya watu, lakini wanaoteseka ni ndugu zako na watakaoteseka zaidi ni kizazi chako. Wema hivi umerogwa au umekata tamaa ya maisha?

Tumechoka kukuelekeza. Kukukumbusha. Kukuonya na kukubembeleza. Mara ya kwanza niliapa kuwa nikitaka kuajiri watu, wanaomzunguka Wema wakileta CV zao nawatandika makofi na kuwaweka ndani. Kwa kufeli kazi rahisi mno ya kuingiza mamilioni ya pesa kupitia jina la Wema. Wataweza kazi ipi zaidi hapa duniani?

Lakini hivi sasa nimebadili mawazo. Nikiwa na jambo la kufanya cha kwanza ni kuwatafuta wanaomzunguka Wema. Maana mtu anayeishi na Wema kikazi, kirafiki au kindugu anaweza kuvumilia na kufanya lolote, popote na wakati wowote. Kumbe kuishi na Wema ndiyo kazi ngumu zaidi kuwahi kutokea katika uso wa dunia hii.

Tukio la usiku mmoja linagharimu maisha ya familia yote miaka nenda rudi. Lakini bado mastaa wetu hawakomi. Na takataka zingine zinazotaka kujenga majina mjini zinatumia mitandao kufanya ujinga wao ili wapate nafasi ya kuongelewa. Hawataki kuishi katika fikra za hofu kwa maisha yajayo kwao na kwa familia zao.

Mitandaoni hasa insta ndiko ambako unakutana na mrembo mzuri mpaka unaogopa. Amewiva na maelezo yake mengi anatumia kiingereza. Kila siku anatupia picha mpya, nywele mpya na nguo mpya. Na zaidi maeneo anayopigia picha ni tofauti tofauti na yote hayafanani na maisha ya Mtanzania wa kawaida.

Kadiri unavyomfuatilia kila siku kwenye ukurasa wake, ndivyo ambavyo na wewe unaanza kuishi kwa mawazo. Unajiona umechelewa maisha. Unahisi kutengwa na dunia. Unadhani pengine ni wewe tu unayekula ugali bamia nchi hii. Wanakutisha mpaka unatamani kushika bunduki 'ukamteke Mo' mwingine.

Lakini kumbe hamna kitu. Pamoja na urembo wake, hamjui Makamu wa Rais. Hamjui Waziri Mkuu wa taifa hili na hata alichosoma shuleni hana kumbukumbu nacho. Anawajua WCB tu. Sasa hawa ndiyo wanaowatia uchizi kina Wema mitandaoni mpaka wanaenda 'lesi' na kuishia kutia aibu familia na wanawake wa taifa zima.

Vyovyote iwavyo staa hasa wa kike kujidhalilisha katika mitandao ya kijamii ni kitu kibaya na siyo cha kiungwana. Mungu alitutofautisha na wanyama kwa utashi wa kifikra. Sasa inakuaje wenzetu wanatenda mambo kama wanyama kwa kukosa utashi. Kibaya zaidi ni walewale siku zote.

Wanaiga umagharibi kipuuzi, wakati wenzetu huoni wakitumia mitandao ya kijamii kufanya ujinga huu. Wanakoiga huonesha maungo kwenye maeneo maalumu kwa kazi hiyo. Tena kwao wana sheria kali zaidi hata siyo tu kujiweka utupu bali hata kuwapa watoto vilevi ni kosa kubwa.

Unafiki ni pale mtu mzima anaomba radhi kwa tendo alilofanya makusudi. Na makusudi inakuja kutokana na tendo hilo kulitenda mara kadhaa. Ifike wakati hawa wenzetu tuwapuuze. Lakini ustashangaa kwenye tukio zito lenye kuhusisha jamii mtu kama Wema anawekwa mbele.

Kwa upuuzi kama huu sidhani kama Azam na shughuli yao ya SZIFF mwakani atajumuishwa. Atengwe hata mwaka mmoja ili liwe fundisho kwa wajinga wengine. Leo anafanya upuuzi kesho anatumika kama alama ya jambo fulani, ndipo vitoto vya kike huko mitaani vinaona upuuzi ndo habari ya mjini.

Tunaharibu watoto wetu kwa kulea tabia mbovu za watu wazima aina ya Wema. Kuna wasichana kibao mitaani wanampenda Wema na kumfuatilia kwa kila kitu. Naye kwa kujua anapendwa anafanya anachojisikia. Haangalii jema wala baya, yeye kila siku anafanya lolote tu bila kujali baya na jema. Hana hofu.

Watoto wataacha kumuiga mtu anayejirekodi matukio ya ngono na kupost mitandaoni, halafu kesho wanamuona kwenye kampeni za mgombea urais akiwa mstari wa mbele. Au muda wote yuko na kiongozi mkubwa wa serikalini wakichekeana na kusifiana? Watoto wa kike mitaani wataacha kuona 'Uwema' ndo jambo bora na la maana?

Ifike wakati watu sampuli ya Wema waliwe bati. Wapotezewe mazima. Ukimsikia maneno yake akiomba radhi, huoni dalili ya mtu asiyejua kosa. Alifanya kosa akijua ni kosa. Na kuita waandishi na wao kwenda kujazana pale kama njegere ndo furaha yake. Ndo lengo la Wema kutaka kuongelewa. Kifupi amefanikiwa alichotaka.

Wema amekuwa msichana maarufu miaka 12 iliyopita baada ya kuvishwa taji la Miss Tanzania. Mpaka leo haamini kama ni maarufu ndiyo maana anajiingiza kwenye uhusiano wenye nafasi ya kuongeleka midomoni mwa watu. Nadhani tukubaliane kwamba wanaume wa kuongeleka wameisha sasa anataka matukio ya kuongeleka.

Kuna watu kwenye kurasa zake mitandaoni wamekuwa wakimuonya sana juu ya mienendo yake michafu. Wakati huohuo wapo biandamu takataka wanadai asifuatiliwe maisha yake. Anayesema hivyo naye kaomba urafiki ili kufuatilia maisha yake mitandaoni. Unabaki kushangaa akili hizi zinatoka kwa Mungu huyu tunayemjua au Mungu ana pacha wake?

Hao wanaomtia sifa na kumvimbisha kichwa ndiyo wanaompotosha na kujikuta Wema kila siku anapoteza mvuto. Anapoteza heshima. Anapoteza marafiki. Anapoteza pesa. Anapoteza kujiamini. Anapoteza mpaka mwili wake na ngozi yake. Wema kawa yeyote hivi sasa. Siyo Wema yule tena.

Kutoka Wema wa kusakwa na kamera za waandishi. Kuviziwa, kupigwa picha na kuandikwa magazetini. Leo hii amekuwa Wema wa kutembea na kamera. Kujifotoa faragha. Kuzisambaza video na picha mnato mitandaoni. Kisha kuanza kutafuta waandishi ili aombe radhi kwa jamii. Na bado haishitui watu zaidi ya kukera. Inasikitisha.

Wema katika wakati wake alikuwa 'untouchable', madini matupu kuanzia unyayoni mpaka utosini. Kila aliyemkaribia alimuambukiza nyota ya pesa na umaarufu. Alikuwa staa ambaye hata mastaa wenzake walitamani ustaa wake. Unakuaje kando ya Wema usijukikane na dunia?

Ukiwa muigizaji wa filamu wakati ule na kutoka na Wema unakuwa staa mara mbili. Ndicho alichoambulia Marehemu Steven Kanumba. Na mwanamuziki vilevile, pamoja na juhudi zake lakini joto la Wema lilimpaisha Diamond mara mbili zaidi. Huo ndiyo muda aliotakiwa kutajirika mtoto wa Mzee Sepetu halafu akazembea kindezi.

Wema siyo bidhaa adimu tena. Siyo mchongo kabisa. Yupo daraja moja na kina Amber Lulu, Amber Rutty, Gigy Money na sampuli ya wasichana wa aina hiyo. Hatetemeshi tena wala kuuza kurasa za udaku mitaani. Alichofanya, ametupia utupu wake mitandaoni, ameomba radhi, amekufa.

Nani anamjali tena? Hakuna...
Wema-Sepetu.jpg
 
Nilikuwa nampenda sana Wema lakini amekuwa mtu wa ovyo!!


Hizi team Wema team hamissa team diamond team ali kiba ndio zilizotufikisha hapa... watu wanafanya upuuzi wanasapotiwa na mitimu yao iliyojazana mavichaa!!
 
Ndyo maana Trump huwa anasema sisi watu weusi siyo binadamu kamili,kilizama kivuko cha MV Nyerere lkn suala hilo lilionekana kama ni jambo dogo sana,watumishi wa umma hawajapanda madaraja kwa zaidi ya miaka mnne lkn hakuna anayepaza sauti,wastaafu wapo mitaani na hawajalipwa fedha zao lkn hakuna anayelizungumzia suala hilo pia,ajira hakuna lkn watu wote wapo kimya ila haya yanayofanywa na Wema Sepetu na Amber Rutty pamoja na Amber Lulu juu ya miili yao ndyo yamekuwa mambo ya maana sana
Lazma tukubali kuwa sisi ndyo wenye matatzo kwenye vichwa vyetu na siyo hao akina Wema na Amber (Rutty na Lulu)
 
Back
Top Bottom