apolycaripto
JF-Expert Member
- Feb 11, 2011
- 644
- 225
Katika kipindi cha mahojiano mnamo tarehe 24/03/2011,Dr Hans Kitine mbali na mambo mengine alidiriki kuangazia ndani ya serikali hii kwa sasa na kusema moja kati vitu vinavyochangia ukosefu wa maadili ni pamoja na kuwapa watu vyeo bila kuwafanyia vetting kupitia vyombo vya usalama.Alidai kuna Katibu Mkuu mmoja ni mchafu kwa maana ya fisadi na watu wanamlalamikia japo hakumtaja jina lakini bado amepewa Wizara tena nyeti zenye fedha nyingi na anaendelea kufisidi kama kawaida.
Tutambue maneno haya ya Dr. Kitine si ya kupuuzwa kwani ni Mzee na Bosi Mstaafu wa Usalama wa Taifa.Nimefanya uchunguzi kupitia kwa baadhi ya watu waliotizama na kumsikia katika mahojiano yale,wengi wamedai Katibu Mkuu anayezungumziwa ni Eng.Omary Chambo.Sina uthibitisho kwa maana ya ushahidi lakini ndiye anayetajwa.
Nashauri suala la kujivua gamba kama inavyosemekana,kuelekee pia kwa hawa Makatibu Wakuu (ambao ndio technical figure na watendaji wakubwa ndani ya Serikali).Haiwezekani Mawaziri wao wachafuke kisha wao wakabaki salama hata kidogo.Kuyumba kwa Serikali kunachangiwa na hawa kwa kiasi kikubwa na si kuishia kwa Wanasiasa pekee.Kikwete hawa watu wanakutafuna hawa!

Kwa haraka haraka ukiangalia wizara inayotia fora kwa ufisadi sasa hivi ni ya Nishati na Madini. Nafikiri hata Katibu wake ndo aliyekuwa anazungumziwa na Kitine. Angalia; Dowans + Richmond, IPTL, Songas, Buzwagi, North Mara, Mirerani, Golden pride, Tanesco. Kote huko ni mikataba hewa tu.
Ingawa nakubaliana na ukweli kwamba wateuliwa wa Raisi ni lazima wafanyiwe 'veting' nasikitika kwamba kwa Tanzania hatua hii imetumiwa ipasavyo na wafanya 'veting' yaani maafisa wa usalama wa taifa kwa kupendekeza majina ya wenzao(Colleagues ) kiasi kwamba asilimia 90 ya viongozi tulionao(mawaziri,makatibu wakuu,wakuu mikoa n.k) ni maafisa wa usalama wa taifa. Wanatumia taarifa walizonazo kujinufaisha kwa kujipanga katika kila nafasi ya uongozi. Athari yake ni kuwa na watu 'Mabogus' kila kona ya uongozi wa nchi.
Kabombe said:Apolycaripto unamjua DR.HASSAN KITINE?
Ana kashfa ya kugushi risiti za matibabu hewa dola 30,000 kwa ajili ya "matibabu"ya mkewe mzungu walipokua Canada.
Serikali ilifuatilia ikakuta hakuna mtu alietibiwa kwa jina na tarehe hiyo.
Jamaa ana hasira tu,lakini ni fisadi wa kutupwa,anaswali sana siku hizi pale bakwata kinondoni,lakini ana kampuni linakopesha kwa riba 30%.
Kwa imani yake haruhusiwi kula riba.
Kitine hana moral authority ya kulipua watu,yeye mwenyewe bado ananuka
Kabombe,
..sasa hivi kuna ufisadi uliopita kiasi na kuvunja rekodi kiasi kwamba hata Kitine ambaye tunaelewa ana madudu yake anapata ujasiri wa kuukemea.
..hata Abdulrahman Kinana ambaye tunajua ni fisadi ktk uuzwaji wa Loliondo, ktk vikao vya CCM amekuwa na moral authority ya kuwakemea mafisadi wa awamu hii.
Kabombe said:Fisadi ni fisadi tu hata akiiba mia.
Tupe details za Kinana kuhusu ufisadi wa Loliondo
usalama wa taifa ulikuwa enzi za mwalimu nyerere (Malehemu-Mungu amulaze pema). Kwa sasa kuna usalama wa masilahi ya watu; hivyo hoja ya kitine inakosa nguvu kwa maana ya usalama wa taifa wa sasa.
Nilimsikiliza tena hiki kipindi kilirushwa mara mbili.
Kitine alisema huyo katibu mkuu si wa wizara ya fedha (akaongeza kuwa wizara ya fedha haina uchakachuaji/pesa nyingi kama aliyoificha)
Akasema ni wazi huyo katibu mkuu anajulikana A-Z na idara ya usalama na anashangaa kivipi anadumu mpaka leo.Aliongeza pamoja na waziri na naibu wake kuwa mzuri ila ni mzigo kuwa na huyu katibu mkuu)
Huyu mtoa mada wa ajabu sana!; kutoka katika maneno ya Kitine hadi kuchukua jina la Chambo mbona hamana 'connection' hii peke yake kwa watu wanao chuja na kufikiri lazima wahisi una-ugomvi na Omary Chambo tena unachuki naye, au la kunajambo lina maslahi kati yako na na yeye.
Hii hoja yako haina namna yoyote hile jinala Chambo linaweza kuingia kama siyo matumizi mabaya ya JF kwa manufaha binafsi, kama hoja yako ni wizara yenye fedha nyingi, mbona Bajeti haionyeshi kama Wizara ya Chambo ndiyo iliyopewa fedha nyingi kuliko Wizara zingine! Kuna Wizara zilitengewa fedha nyingi zaidi ya Ujenzi na kupewa kipaumbele au hujui? Mbona hukuwazia Wizara ya fedha ambayo ndiyo inamiliki Hazina ya kaya?
Ebu lete ushahidi Mkuu hapa unapiga soga tu!
Nafikiri ndugu yangu una maslahi binafsi na Omary Chambo, kwani wewe unataka kutuambia ni wizara ipi iliyopewa pesa nyingi zaidi ya miundombinu? Au unataka kusema ni wizara gani kwa sasa yenye waziri na naibu wake mashuhuri, panachuki gani hapo kama si kutetea ufisadi kama ilivyo kawaida ya wabongo hasa akiwa na maslahi?