Dr Kitila Mkumbo amwanika Mwigulu Nchemba

Dr Kitila Mkumbo amwanika Mwigulu Nchemba

Nashukuru bwana Kitila hakusema uchaguzi mdogo kijijini kwao walipozalowa wazazi wake pia ulisimamiwa na Mwigulu na yeye alipeleka magari, pesa, na kundi maalum la vijana kufanya fujo halafu matokeo anayajua mwenyewe.

Ahahahaha CCM wameanza kufananisha chaguzi za vijiji Singida na viti 5 walivyopteza vya udiwani mikoa tofauti tofauti ahahahaha!

CCM inaelekea kufa na hilo halina ubishi!Muda wanao wa kujirekebisha!
 
Na kama Ccm wakiendelea kumtumia Mwigulu kwenye Chaguzi , basi Bila shaka wategemee Maumivu zaidi , maana kwa uchunguzi nilioufanya ; hasa kwenye Eneo la Tanganyika , ukiacha SHETANI anayelaaniwa kwenye nyumba zote za Ibada , mwingine anayefuatia kwa kulaaniwa All over the country ( Tanganyika ) anaitwa MWIGULU NCHEMBA .

Naunga mkono hoja 100%
 
Mwigulu hachafuki hata mkijikusanya na kutumia matope ya aina yoyote.

CHADEMA mlikuwa mmezoea vya kunyonga kwa sasa hali ya kisiasa ndani ya CCM imebadilika na kwa sasa tunawaletea vya kuchinja na kama mlivyo weupe kihoja, vimewashinda.

CHADEMA hawana hoja tena mezani kwa sababu ngoma ya hoja ya ufisadi mlio wake wananchi wameuchoka kuusikia ikichukuliwa kuwa ndani ya CHADEMA kuna ufisadi wa kila siku unaoharalishwa kupitia CHADEMA Central Commettee.

Baada ya kuwajibu hoja zao kwa sasa wanakuja na style ya political cherry picking. Huyu Dr. Kitila hata watu wa kijijini kwake hawakumpa kura halafu ndiyo anapata moral authority ya kuisemea Tanzania. He's making hullabaloo for nothing.

Dr. Kitila. Welcomme to ground zero.

Bwana Mdogo siku tukianza kuwapiga Makofi hawa polisi wanaowasaidia hadi wanajidhalilisha nadhani ndiyo utakapojua maana ya nguvu ya UMMA ! NOTHING LASTS LONGER ! Stay tuned .
 
Bwana Mdogo siku tukianza kuwapiga Makofi hawa polisi wanaowasaidia hadi wanajidhalilisha nadhani ndiyo utakapojua maana ya nguvu ya UMMA ! NOTHING LASTS LONGER ! Stay tuned .
Mwigulu ni chukizo la Chamdomo kipenzi cha wanyiramba.
 
Mbona msomi na mfuasi mzuri wa chadema dr Kitila anamzungumzia Mwigulu? Kwani ccm ikishindwa si ndio furaha kwa chadema? Mwigulu ni tatizo kwa chadema.
 
Mtu ana doma linamwaga matusi mazito! Kwenye facebook alikuwa anawadhalilisha dada zetu kisa wanaenda mwezi! Ni mwanasiasa mchafu wa maneno.. Hana hekima kwa kweli..
Bila kuweka unazi viongozi wengi wa ccm kwa sasa si viongozi.. Ni watu wa ajabu ajabu.. Sijui wameokotwa wapi..

wanavurugukiwa akili .kwani damu ya watanzania waliyomwaga inawalilia
 
Siku zote chama kinachotawala kikitaka kufa lazima kiue sana,soma history hata KANU n.k. Hasa Afrika,imekua kama kupe unapomchomoa kwenye ng'ombe wako lazima damu itoke.Ila Mungu yupo watahukumiwa
 
Kitila ameshindwa kuonysha ushindani ht kwenye kitongoji na kijiji alichozaliwa. Kinaongozwa na chama cha mapinduzi, anatoa wapi uhalali na ujasiri wa kumzungumzia mbunge wake??? Huyu ni lost generation
 
Nipeni jibu hapa wakuu, kijiji alichozaliwa kitila mkumbo, kinaongozwa na chama gani???
 
Kitila ameshindwa kuonysha ushindani ht kwenye kitongoji na kijiji alichozaliwa. Kinaongozwa na chama cha mapinduzi, anatoa wapi uhalali na ujasiri wa kumzungumzia mbunge wake??? Huyu ni lost generation

mi naomba tujadili hoja ya kitila, ni kweli mwigulu ana hizo tabia alizozisema? kisha tujadili kama tabia hizo (kama anazo) zinabathari kwa chama chetu na wananchi kwa ujumla. kosa lako hapa ni kumjadili mleta hoja badala ya hoja.
 
Uchaguzi unaosimamiwa mwigulu, lazima vifo vitokee! Mwigulu ndo anayehusika na mauaji ya arusha!

si hapo igunga ktk uchaguzi mdogo kijana wao rafiki yangu walimwagia tindikali na kujidai kuwa cdm ndo ilihusika, akazini na mke wa mtu ana roho chafu kama mkaa.ccm inamfia mikononi mwake
 
Bila ya mgawo wa nyama na Pombe,hongo za fedha tasilimu Mwigulu asingeshinda uchaguzi wa wenyeviti Jimboni kwake Iramba,Tathimini iko wazi kwa Nchi nzima CCM hamtaki Kukubali tu Ila ukweli CHADEMA imewalemea CCM kwa namna zote.
 
Ccm itaondoka tu iwe kwa shari au hiari.
 
Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA na msomi aliyebobea Dr Kitila Mkumbo amesema CCM sasa imezidi kufubaa na kupauka.

Dr Kitila amesema kwa mwaka huu tu CCM imepoteza kata 7 walizokuwa wanashikilia kwa Chadema.

Dr Kitila amesema lililo wazi ni kwamba chaguzi ndogo sasa hivi ndani ya CCM zinasimamiwa na kijana mdogo aliyejaa dharau,kiburi na ulevi wa madaraka anayeitwa Mwigulu Nchemba.

Dr Kitila ameendelea kusema kijana huyu kutokana na dharau zake wananchi sasa wamekuwa wakichukua taswira yake kama ndiyo taswira ya CCM.

Amesema lililo wazi katika kata zote zilizofanya uchaguzi awamu hii ambapo kijana huyu aliweka kambi CCM ilianguka vibaya.

Kata ambazo Mwigulu aliweka kambi ni Kata za Iseke Singida,Iyela Mbeya,Dongobesh Mbulu na Arusha mjini ambapo kote CCM iliangukia pua isipokuwa Arusha ambapo uchaguzi wake utakuwa tarehe 30 June.

Dr Kitila amehitimisha kwa kusema anakumbuka enzi za John Malecela maarufu kama Tingatinga alipokuwa anasimamia chaguzi za chama hicho kwa weledi mkubwa ambapo ilikuwa ni ndoto kwa kata iliyokuwa inashikiliwa na CCM kunyakuliwa na upinzani.

Source:Raia Mwema.

Mkuu Molemo mbona sijaona huo uanikwaji hapa? Mimi nilivyoona kichwa cha habari na ile kujua kwamba Dr. Mkumbo anatoka Singida kama Mwigulu na Dr. ni mhadhiri pale chuo kikuu ambapo nasikia Mwigulu alisoma nikaona sasa Mwigulu huenda kaanikwa toka kwao kijijini hadi chuoni! Kumbe siyo!
 
Last edited by a moderator:
Record zake iko hivi:
Matusi = A+
Busara = 0-
Ujambazi = A
Uzinzi = A
Hekima = 0-
Ugaidi = A+
Uwongo = A+

Ilikuwa lazima apate daraja la juu sana

mkuu tupe source tufuatilia habari hizi
 
Back
Top Bottom