Mimi binafsi simfahamu Dr Kigwa na sijawahi kukutana naye, ila kwa mawazo yangu mapana nafhani kuwa huyu dr alitakiwa apewe hii wizara, huyu kiongozi wetu ni jamaa ambaye ana misimamo yake na ni mtu ambaye nina uhakika ni msikivu na anajua matatizo ya wananchi katika hospitali zetu.
Ni mtu ambaye unaweza kumpata kwa urahisi sana na kumpa ujumbe au malalamika yako na pia kumpa ushauri kama unao.
Nina uhakika huyu jamaa ataenda mbali sana.
Juzi alitembelea Hospitali ya Ilala alikuta madudu na baadhi ya ofisi hakuna huduma na ofisi zimefungwa.
Sijui atachukua hatua gani ila ninachodhani ni kuwa Katika hospitali zetu kuna watu ambao wamejisahau sana na wamesahau wajibu wao, ni wajibu wetu kufanya kazi kama inavyostahili.
Kila la Heri Dr, najua tutapata mabadiliko mengi sana ndani ya hii wizara. Ila muanze kupokea malalamiko ya wananchi na ushauri pia kwa sababu hamuwezi kufika kila sehemu at once na kwenye maamuzi yenu mjue kutenganisha chuki za watu binafsi na reality.
Asante.
saint ivuga.
Ndugu yangu labda wewe ndio unaleta siasa nakumbuka katika mdahalo Dr Kigwangallah alidai macho makavu eti hakuna wagonjwa wanaolala chini ?.Kukataa kukiri tatizo ni tatizo kubwa kuliko tatizo lenyewe Dr Kigwangallah ni tatizo kwakuwa ana sifa ya kuona tatizo.
Sasa mdau juzi si ilikuwa si siku ya kazi unadhan ofisi zooote utazikuta wazi?Grow up brother ! Nimesema kwa mawazo yangu. Labda kama unataka na mimi nianze kuku attack sema, manake naweza sana. Ila nina uhakika umesoma heading tu.
But asante kwa kuchangia thread yangu.
Sijatumwa na kigwa na hawezi kufanya hivyo kwani haina impact yoyote
Huko Amana alienda na Vitanda? dawa za bure kwa ajili ya wazee? majengo ya kulazwa wagonjwa? Kama kazi zao ni kukagua daftari la mahudhurio sioni kipya? Hayo matatizo yanafahamika, wasituletee siasa bali wayatatue. Watawahadaa watanzania, halafu watanzania hao wanakuja kutupigia kelele sisi wataalamu.
Mgonjwa anakuja, unasoma prescription, unamwambia dawa hii hatuna. Utamsikia mzee wa watu analalamika, "tumeambiw dawa zipo, mnatuibia nk..." Inachofanya serikali ni kutuchonganisha watumishi na watanzania. Tatueni kero, acheni siasa. Sasa, nitoe hela yangu nimnunulie mgonjwa dawa? Nitasaidia wangapi?
Wazee wanakumbwa na magonjwa ambayo dawa zake ni ghali; Magonjwa ya moyo & homoni ... Na serikali inapaswa kuwapatia dawa hizi, ndo vitu anavyopaswa kuvisimamia waziri sio kukagua attendance sheets. Zinamsaidia nini mtanzania? Siku akipita ofisini kwangu nitamweleza hayo, sipendi unafiki. Otherwise, mkitaka wazee wenu waishi vizuri wakatieni BIMA, vinginevyo utaingia gharama kubwa sana.
Sasa ndugu huoni kwa kutoroka vituo vya kazi huwezi kuwahudumia walipa kodi no matter what?
Yani nusu ya madaktari wasiwepo vituoni na useme si muhimu kucheki attendance..???
Si muamie kabisa private.... muone kama watawavumilia..
mvumilie. watu wengine wako kupinga kija jambo, iwe mitizamo, maoni, n.k