Huko Amana alienda na Vitanda? dawa za bure kwa ajili ya wazee? majengo ya kulazwa wagonjwa? Kama kazi zao ni kukagua daftari la mahudhurio sioni kipya? Hayo matatizo yanafahamika, wasituletee siasa bali wayatatue. Watawahadaa watanzania, halafu watanzania hao wanakuja kutupigia kelele sisi wataalamu.
Mgonjwa anakuja, unasoma prescription, unamwambia dawa hii hatuna. Utamsikia mzee wa watu analalamika, "tumeambiw dawa zipo, mnatuibia nk..." Inachofanya serikali ni kutuchonganisha watumishi na watanzania. Tatueni kero, acheni siasa. Sasa, nitoe hela yangu nimnunulie mgonjwa dawa? Nitasaidia wangapi?
Wazee wanakumbwa na magonjwa ambayo dawa zake ni ghali; Magonjwa ya moyo & homoni ... Na serikali inapaswa kuwapatia dawa hizi, ndo vitu anavyopaswa kuvisimamia waziri sio kukagua attendance sheets. Zinamsaidia nini mtanzania? Siku akipita ofisini kwangu nitamweleza hayo, sipendi unafiki. Otherwise, mkitaka wazee wenu waishi vizuri wakatieni BIMA, vinginevyo utaingia gharama kubwa sana.