Dr. Kigwangalla hapa umechemka! Huku sio kufikiria hata kidogo

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Umeripotiwa kumpa mwezi mmoja Mganga mkuu wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara Dr Uledi kuhakikisha tatizo la uhaba wa damu linaisha, hii ni pomoja na kujumuisha uongozi mzima wa afya mkoani humo.

Hii kama sio kutesana ni nini? Sasa kama damu hakuna na Wananchi hawataki kujitolea Kutoa damu walazimishwe au iweje? Wakakamatwe watoe damu kwa nguvu au vipi?

Hili tatizo lipo kila mkoa, hapa ni kutaftiana matatizo tu maana hilo suala sio la kujitakia ni la kibinadamu zaidi, huenda Wananchi hawataki kujitokeza Kutoa damu either kwa hali ngumu ya maisha au pengine ni magonjwa au imani zao!

Hapa ndugu Kigwangala bado unakurupuka, hii sio siasa ni zaidi ya siasa! Hii sio kasi anayoisema Rais Magufuli ni kuumizana tu. Nina imani hiyo kofia uliyonayo ni ya muda tu tazama ya mbele ndugu yangu.

Hivi ikisikika umemsimamisha kiongozi kazi kwa sababu ya uhaba wa damu ndani ya hospitali dunia itakuonaje ndugu? Kwakuwa huyo huyu mtumishi atahitaj kulinda nafasi yake kama wewe unavyolinda ya kwako unataka akakamate watu mitaani watoe damu kwa nguvu sio?

Yaani badala ya kufanya majadiliano nmna ya kuhakikisha kua tatizo linaisha lakini wewe unampa mtu mwezi mmoja kama adhabu, huu sio ubinadamu hata kidogo.

Serikali haitoweza kununua damu, inaomba msaada kwa Wananchi wajitolee.
 
~~>Naona wasiwasi sio Wananchi kufa kwa kukosa damu bali wasiwasi ni kufukuzwa kazi.

Huyo anatengenezwa mazingira ya kutumbuliwa... Safari njema.
 
Damu zenyewe hadi zitoke zonal
Blood bank KCMC sasa hapo manyara Kama hakuna wafanye nini? Ngoja tuone mwezi ukiisha atafanya nini
 
Aende machinjioni kuna damu nyingi,au awasiliane na Mkuu wa wachawi pale kigoma,wana ndoo nyingi za damu ya binadamu tena bado mbichi
 
Huyu Kigwangalah mwanzo nilikuwa namuona wa maana kidogo kumbe buuure kabisa.
Tokea apewe huo unaibu wa Afya amekuwa ni mtu wa kuboronga tu.
Anapenda sifa,auze kwenye magazeti.

Lakini afanye nini?Serikali ya awamu ya tano inafanya kazi ya kwenye vyombo vya habari.
Viongozi wanapigana vikumbo kutengeneza headlines!
 
Serikali ya media inajitahidi kuonyesha kuwa haina matatizo bali watendaji ndiyo wenye matatizo, na utendaji wa kutoa matamko tata kwenye vyombo vya habari.

Kama mkuu wa serikali anatoa kauli kuwa kijana anayefeli akafungwe, vijana wasio na kazi wakamatwe wakafanye kazi kwa nguvu, atawatumbua mapadri wakitumia vibaya sadaka anayotoa, inaonyesha dhahiri kukosa weledi.

Mazingira ya shule wanazosoma hao vijana yanawapa nafasi na vifaa (vitabu, maabara, walimu, chakula nk.)?

Serikali yake na hata iliyopita imetengeneza ajira kiasi gani? Kama kazi ni kilimo kuna ardhi na vitendea kazi pamoja na masoko ya uhakika?

Na kwa sababu ya media na kukosa sera zaidi ya kutumbua majipu anaona hata kwenye imani na viongozi wa imani ambao hana uwezo wala mamlaka ya kuwachagua na kuwaondoa eti wakitumia vibaya sadaka anayotoa atawatumbua.

Sasa kama kiongozi wao anaonyesha njia kwa kauli hizi unategemea wasaidizi wake ambao hawajiamini wanafanyaje? Ni lazima watatoa kauli tata kuliko yeye ni kuwaombea tu
 
ha ha ha ha ha ha Umepanic Bro SIASA Mchezo mchafu hizi kauli huwa zinatolewa PUBLIC kwa jazba ila wakiwa chemba anamwambia kishkaji tu,
 
Cjawai kumkubali kigwangala hata siku moja ni mzee wa kukurupuka tu ametusumbua sanaa pale bugango medical school wakat nasoma
 
Back
Top Bottom