Mungi
JF Gold Member
- Sep 23, 2010
- 16,975
- 9,580
Huyu jamaa kwa ukali anaoendelea nao ndani ya bunge, kwa kitendo cha kupinga sera na itikadi za ccm, na kutetea maslahi ya wananchi wa Nzega, hatadumu. Nawaambieni 2015 watamfanya walichomfanya Selelii kwenye kura za maoni. Amepinga bajeti ya wizara ya maji kwa 100%. Anasema naweka kumbukumbu sahii kwenye hansard, ili baada ya miaka 50 wajukuu zake watakaoingia humu wakaisoma hansard wasije wakamwona ni punguani kwa kuunga mkono hoja. Ghasia kaomba mwongozo wa spika kutaka Dr. Kigwangala afute kauli yake ya punguani, akilalamika kuwa inamaana wabunge wanaounga mkono hoja ni punguani. Spika kamtetea Dr. Kigwangala.