78Kuku
JF-Expert Member
- Mar 31, 2021
- 562
- 754
Mfano mtu amesomea u daktari amegraduate hana mtaji unataka ajiajiri kivipi?Usichukulie kama napinga nacho andika nakiona mitaani watu wame graduate ok ajira hakuna lakini hata kujiajiri pia imekuwa shida. Je ni mifumo yetu nje ya elimu haina support kwa hawa wanaomaliza vyuo maana unasema yanafundishwa yote huko sasa nataka ulipe elimu kwanini elimu yetu inadharauliwa? na ukiona mtu anapata heshima ujuwe kaongezea degree huko nje. Kuna baadhi ya nchi tu degree ya Tanzania wanaweka pembeni huko. shida nini?
Hapa tatizo sio elimu ila tatizo serikali imeshindwa kuweka mazingira ya watu ku apply kile walichokisomea ndo maana unaona kuna graduates wengi hawana ajira.
Mi kukwambia ukweli hata mtu asomee Oxford au Cambridge akirudi mtaani kama hana mtaji au hajaajiriwa ataonekana amesoma elimu ya hovyo.
Hata hao wanaharakati, mawaziri, n.k. unaosikia wanapiga kelele ukimtoa kwenye hiyo nafasi ukasema ajiajiri trust me atachemka no matter amesomea wapi.
Kwa hiyo tatizo sio elimu ila tatizo ni mazingira yetu kutokua rafiki.