kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,495
- 17,635
Dr. Kashilila ni miongoni mwa watanzania wachache waliopata bahati ya kusoma hadi PhD. Taifa linabidi lijivunie kuwa nao watu wenye kiwango hiki cha elimu kwa sababu wao wanapaswa kuwa fimbo ya kuwaongozea wale wasioona ambao ni ndiyo wengi katika taifa la kimaskini kama letu. Watu wenye PhD ndio wanaopaswa kuongoza vita ya kuelekea full democracy, kupinga dhuluma, ujinga, uonevu, udini, na ukabila ndani ya jamii. Mtu mwenye kiwango hili cha elimu amefundishwa kusema na kutotenda mambo bila ya kuwa na takwimu sahihi (evidence). Mtu wa ngazi hii ana elimu ya what are variables (dependents and independents), mtu wa ngazi hii anajua namna dependent na independent variables zinavyohusiana. Anajua vema uhusiano kati ya dependent na independent variables unaweza kuwa ama causal-effect (causality) au association tu. Hivyo anajua kuwa ili uweze kusema kitu (variable) hiki (A) ndicho kinachosababisha (sufficient cause) jambo lile (B) litokee lazima kuwe na vigezo 9 ambavyo ni strength, consistency, specificity, temporality, biologic gradient, plausibility, coherence, experimental evidence na analogy (vigezo hivi vipo kwenye vitabu vyote vya applied epidemiology). Pia, Ili mtu aweze kusema kuwa kitu (A) kina uhusiano (association) na jambo (B) kutokea pia lazima uwe na hypothesis ambayo unaweza kuipima (significance testing) ili ujue kiwango halisi cha uhusiano kati ya vitu hivyo viwili kutokea pamoja kila wakati vinapokutana (p-value). Mtu mwenye PhD pia anajua kuwa ziko confounders na coincidence katika jambo kutokea ambavyo lazima mtafiti avi address kabla hajasema ama kuamua kutenda jambo.
Baada ya kuwakumbusha wasomi kile walichojifunza kwa kodi za wananchi, sasa ngoja nirudi kwenye hoja ya msingi. Ni hivi karibuni Katibu wa bunge Dr. T. Kashilila amesema kuwa utovu wa nidhamu wa baadhi ya wahemimiwa wabunge (wapinzani) unasababishwa na bunge kurushwa hewani live!! Hivyo wanatafuta umaarufu kwa wananchi. Hivyo dawa yake ni kusimamisha urushaji wa vipindi vya bunge live. Mimi siamini mtu mwenye sifa kama ya Kashilila anaweza kusema na kuamua hivyo, labda kweli amenukuliwa vibaya kama anavyosema yeye mwenyewe. Kashilila kama msomi alipaswa kufanya utafiti japo mdogo wa kina ili agundue vyanzo halisi vya kelele za wabunge bungeni ili agundue kama tatizo hasa ni luninga, kanuni za bunge, matumizi ya kanuni, utovu wa nidhamu wa waheshimiwa wabunge wa upinzani, ugeni wa wabunge bungeni, kukua kwa democrasia ama hali mbaya za maisha na huduma za jamii kwa watanzania?. Kusema moja kwa moja kama tatizo ni luninga sio sawa kitaaluma, na maamuzi ya namna hii hayawakilishi watu wenye taaluma kote duniani, maana hayana harufu ya usomi wowote ila ushabiki. Watanzania walishapata mazoea sasa ya kulifuatilia bunge lao, wanatenga muda wao japo sio kila siku kufuatilia bunge lao likijadili hatima yao. Wako watu wamenunua na kuweka luninga ofisini mwao na wengine viredio vidogo kwa kazi hiyo. Hata wagonjwa wanaposubiri zamu zao za kutibiwa huwa wanapenda kusubiri wakiangalia kipindi cha bunge. Jamani wasomi tumieni elimu zenu kusaidia mambo ya wananchi sio matumbo yenu yaende mbele