Dr. JJ Mwaka si rafiki wa masikini

Dr. JJ Mwaka si rafiki wa masikini

Kwa kipindi kirefu sasa mtaalam wa tiba mbadala maarufu kwa jina la Dr.Mwaka anayetoa huduma zake ktk eneo la Bungoni amejizolea umaarufu miongoni mwa wananchi wanaofika ktk Clinic yake kupata huduma.

Awali ya yote nampongeza kwa maono aliyopewa na mwenyezi Mungu kwa kuwasaidia sehemu kubwa ya watanzania wenzake na hata wa nchi za jirani hususani kwa tiba ya maradhi sugu yaliyoshindikana hospitali.

Masikitiko yangu kwa Clinic hii nimebaini nilipokwenda kupata huduma tarehe 10.12.2015 kwamba kwa gharama zinazotozwa pale hakika siyo rafiki wa masikini.

Kuanzia kugungua kadi ya kumwona daktari, vipimo na kimbunga ni kwenye kulipia dawa. Kwa yule anayehitaji kuonana na Dr.Mwaka mwenyewe nako kuna gharama zake. Kwa mgonjwa unayetarajia kwenda kwa mara ya kwanza unatakiwa uwe na kiasi kisichopungua laki tatu.

Napenda kutoa wito kwa Dr. Mwaka aliangalie swala la kupunguza gharama ili huduma anayoitoa iweze kuwanufaisha idadi kubwa ya Watanzania.

HAKIKA KUSOMA NI MALI.

Mkuu mjini watu wanapiga hela kijanja sana, hebu ona huyu tapeli anavoishi kifahari kwa kutegemea hela za masikini wenye shida za kiafya!
 

Attachments

  • 1450175389248.jpg
    1450175389248.jpg
    62.7 KB · Views: 566
  • 1450175405079.jpg
    1450175405079.jpg
    49.3 KB · Views: 555
Aaaanh jamaa ana magari tisa kama sio kumi. . Yalioneshwa kwenye kipindi cha clouds tv, five gear nadhani kama sijakosea

Ni kweli ndugu kwa ule ukwasi wa mali niliona pia ni lazima atie shaka maana madaktari wenyewe tu by profes.!! wanasota lakini yeye kiubweteee katupiga
 
Yule ni Taperi tu,, mi wife Kala Sana DAWA zake bila mafanikio,,, ,, ALIENDA KUPONEA KWA KAIRUKI HOSPITAL,,,tena huyo MWAKA DAWA zake ni gharama kubwa mno na hazisaidii

Acha ujinga wewe, umeona cheti chake alichosomea? Wee umeambiwa huyu traditional healer, yeye kajigeuza dokta wa modern medicine bado unabwek bweka hapa kasomea kasomea.



Tatizo letu waafrika ni kuona kila kilichopangwa na mzungu ndio basi hata kama hakionyeshi faida kwetu.

Wagunduzi siku zote ni watu wa kawaida .
Kazi ya wasomi ni kutafiti huo ugunduzi na kujenga hoja za kuboresha au kuja na formula rahisi zaidi.

Eti tatizo ni kujiita dr.
Hata angejiita Mungu sina shida naye kama anayoyafanya yanalingana na anavyojiita.
Tunao madaktari wengi wasio na wito na waendekeza ufisada na kuiba madawa na vifaa vya serikali ili wafungue maduka binafsi ya dawa.
Hawa ndio hatari kuliko Dr. Mwaka.

Nadhani tumpime Dr. Mwaka kwa uelewa wake juu ya tiba anayotoa ya magonjwa ya uzazi.
Je,ni wapi anatoa maelezo yasiyo sahihi?
Je,hasomea kile anachokifanya na kutoa Elimu.
Tatizo watanzania hasa vijana waliozaliwa mjini hawajui kuwa kuna tiba mbadala za uhakika ambazo zimetumika kwa karne nyingi . Kuitwa sijui dokta sjui ushuzi gani hayo ni madaraja tu ya viwango vya elimu vilivyowekwa na wazungu.
Mwaka naye kwa kiwango cha tiba mbadala ni dokta. Watu ndio wanaomwita hivyo na amejubali wito wa wateja wake. Hakuna dhambi hapo.
Watu watampuuza pale tu wale tuliowaweka kwenye majengo ya umma na kuwapa madawa na vifaa kwa pesa za umma watakapoweza kuwapenda na kuwahudumia wagonjwa kwa ukarimu na kujali. Kwa sasa hata Manyaunyau atajiita dokta kutokana na wale tuliowaamini kugeuza hospitali za umma kuwa vijiwe vyao vya wizi na rushwa.
Na ukiona mtu ameenda kule kwa kina Mwaka ujue amesumbuka sana kwa hizo hospitali za wazungu na akakosa tiba.
 
Kumbe ni 300,000 ndo mana yupo kwenye process ya kujenga ghorofa aiseee...
 
Kwanini asingeanza kwa babu wa loliondo?
Babu wa Loliondo ni retired. wastaafu hawaguswi Tanzania. kama huamini mwambie Magufuli awaguse wastaafu waliomtangulia..ni katiba yetu. Wacha Kigwa ashughulike na akina Mwaka, mwezi, Ndondi, Harubu sijui Rahabu, nk
 
Back
Top Bottom