Malilambwiga
JF-Expert Member
- Jul 19, 2015
- 485
- 296
Kwa kipindi kirefu sasa mtaalam wa tiba mbadala maarufu kwa jina la Dr.Mwaka anayetoa huduma zake ktk eneo la Bungoni amejizolea umaarufu miongoni mwa wananchi wanaofika ktk Clinic yake kupata huduma.
Awali ya yote nampongeza kwa maono aliyopewa na mwenyezi Mungu kwa kuwasaidia sehemu kubwa ya watanzania wenzake na hata wa nchi za jirani hususani kwa tiba ya maradhi sugu yaliyoshindikana hospitali.
Masikitiko yangu kwa Clinic hii nimebaini nilipokwenda kupata huduma tarehe 10.12.2015 kwamba kwa gharama zinazotozwa pale hakika siyo rafiki wa masikini.
Kuanzia kugungua kadi ya kumwona daktari, vipimo na kimbunga ni kwenye kulipia dawa. Kwa yule anayehitaji kuonana na Dr.Mwaka mwenyewe nako kuna gharama zake. Kwa mgonjwa unayetarajia kwenda kwa mara ya kwanza unatakiwa uwe na kiasi kisichopungua laki tatu.
Napenda kutoa wito kwa Dr. Mwaka aliangalie swala la kupunguza gharama ili huduma anayoitoa iweze kuwanufaisha idadi kubwa ya Watanzania.
HAKIKA KUSOMA NI MALI.