Dr. Hamis Kigwangalla, Kugoma ni sawa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Hamis Kigwangalla, Kugoma ni sawa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mgeni wenu, Jan 20, 2012.

 1. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Salaam,nimeskia katika Radio moja ikisoma Magazeti kuwa Tahariri inamlaani Dr(mb)Hamis Kigwangala kugomesha madaktari wenzake,
  Napenda mnisaidie kujua ni sawa kwake kama Mbunge kfanya hivyo?au kama Daktari ni sawa kuacha wagonjwa wafe kwa ajili ya posho?naomba sana kujua kutoka kwenu....
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kwani Kigwangallah ni nani hadi agomeshe madaktari??

  Hebu waaache kumwonea Hamis
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hamna mtu mwene power ya kugomesha watu wengine under normal room temperature, labda kama anawashkia binduki.
   
 4. c

  christer Senior Member

  #4
  Jan 20, 2012
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wamegoma wenyewe kutokana na hali yao wanavyo iona. kwanini serikali isiwajali kama inajua wakigoma tu wagonjwa wanakufa?madaktari wanafanya kazi ngumu sana.mpaka kuingilia muda wao wa mapumziko lakini wanaishi kwa taabu na wakitaka kuongeza kipato ndo kufungua hospitali zao na maduka ya madawa na kuacha hospitali hazina daktari.serikali angalieni maslahi.mbona wanasiasa wakikaa tu kwenye vikao wanapata posho kubwa?
   
 5. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Serikali yenu ni sikivu,ipi mbioni katika upembuzi yakinifu na usanifu stadi ili kuboresha mchakato wa kuifanya iwe mbioni kuangalia suala hili muhimu,tuwaombe tu madaktari wavute Subira maana Serikali ya CCM inawajali sana wananchi wake,Fedha nyingi tulitumia katika mbio za mwenge na kuazimisha miaka 50 ya Uhuru,ukizingatia ndio vipaumbele vyetu hapa Tanzania
   
 6. K

  Kipara kikubwa Member

  #6
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kusema Dr Kigwangala kagomesha madaktari si sawa japo mi navokumbuka naye alikumbwa na hili tatizo wakati akifanya hiyo inten hadi akanyang'anywa leseni na akataka kufungiwa na akaenda mahakamani akitetewa na Tundu lisu tena bure. Dr Kigwangala kihistoria na mpiganaji sema ndo hivo kuna uhuru mwingine ukiwa huko kwa magamba unaufyata kulinda maslahi yako.

  Anaweza akawa anaguswa na tukio hili kwa kukumbuka yalomkuta yeye! Kimsingi hakuna atakayefurahia wagonjwa wafe lakini kama watu hawalipwi posho ambazo wao ndo mishahara maana kama hujaajiriwa unalipwa posho sasa hazilipwi unataka akawaombe wagonjwa?

  Wakati mwingine inabd hii kitu itokee japo huleta madhara na ushauri wangu ni vema serikali wakae wamalize mvutano.
   
 7. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  mgenu wenu,kweli gvt ni sikivu,kama imeweza kuwapa viwanja wakazi wa mabonden mabwepande hata ikibidi kuwabomolea wakazi wa mabwepande mpaka wakalala nje ili watu wa mabonden waishi vema. pia dr hamis kama daktari naye ana haki ya kugoma ili fani ya udaktari idumu. Isiwe kama TUCTA na CWT wanatishia kugoma miaka yote mpaka tumeshawaona wanamaigizo. Gomeni madokta ili gvt idumishe fani yenu maridhawa!
   
 8. magistergtz

  magistergtz JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 282
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni sahihi kabisa, bila posho intern hawezi kuudumia wagonjwa maana hana mshahara
  Ale wapi?
  istoshe, na mhimu zaidi, Dr. Kigwangala kama mbunge wa ccm anajua serikali ya jk sio sikivu; kiasi kwamba bila kugoma watakufa kwa njaa.
   
 9. magistergtz

  magistergtz JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 282
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sio jambo la kawaida kwa kada wa CCM na Mbunge kushauri watu wagome ili kupata haki zao.
  Dr. Hamis Kigwangala kawashauri madaktari kugoma ili walipwe stahili zao.

  Bila shaka kwa hili Dr. Kigwangala alijua kuwa serikali ilikuwa na kawaida ya kupuuza wajibu wake, mfano kwa kutowalipa madaktari na waalimu, na pale ilipokumbushwa wajibu huo hujibu kwa dharau, kiburi na ubabe kama alivojibu B. NYONI.

  Dr. H. K anatambua kuwa haiingii akilini kuwanyima ama kuwacheleweshea stahili watumishi nyeti kama madaktari na mwalimu ktk kipindi ambacho posho za wanasiasa tena wenye mishahara ya mamilioni wamepandishiwa posho za siku zikapindukia kima cha cha chini cha mshahara wa mwezi! Yaani, posho ya siku moja ya waheshimiwa wanasiasa fulani ni zaidi sana ya mishahara ya mwezi mzima ya watumishi wengine wa umma.
  Nimpongeze Dr. Kigwangala kwa uthubutu wake wa kukemea uovu huu. Ni mfano mzuri wa kuigwa ili kwa pamoja tujenge taifa letu.
  Mungu ibarili Tanzania, Mungu iepushe Tanzania na waovu hawa wajilipao posho kubwa huku wakihujumu stahili za madaktari na walimu ili wagonjwa maskini wafe kwa kukosa huduma ; na watoto wa maskini wabakie vilaza kwa kukosa elimu bora.
   
 10. k

  kamimbi Senior Member

  #10
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania nadhani wanaoishi kwa amani ni watu wapumbavu tu, ila kwa mwenye akili sidhani kama wanaridhika na haya yanayoendelea, serikali kama baba imejenga tofauti kubwa sana kati ya aliyenacho na asiye nacho kwa watumishi walio humohumo ndani ya serikali, hili linaonekana na kila mwenye akili timamu hata kama hakubahatika kusoma hata shule ya msingi. kwa upande wangu nakelwa mno na ubadhirifu kama huu, ni unyama wa hali ya juu.
   
 11. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2012
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hata mbumbumbu mzungu wa reli anajua hilo.
   
 12. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  dr hamisi ameingia kwenye siasa ili kukimbia kero zinazokabili madaktari.
   
 13. N

  Nyota Njema Senior Member

  #13
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kinachofanywa na Kigwangala ni uhuni na unafiki tu, si kweli kwamba anakubali kuwa serikali ya Kikwete si sikivu; na sio kwamba haijali wafanyakazi tu bali na hata wananchi kwa ujumla wao. Rais mwenyewe alishaonyesha kwa mifano jinsi ambavyo wafanyakazi wa nchi hii wasivyo na kipaumbele chochote kwake cha maana, alishaahidi kuwatwanga risasi endapo watamkosesha usingizi, sasa wafanyakazi wategemee nini kutoka kwa watendaji wengine?

  Hawa wote ni sawa na nyani, tumbili, ngedele, kima na nguruwe kwenye shamba linaloitwa Tanzania, na wataendelea kuliharibu mpaka pale wenye shamba (waTanzania) watakapoamua kulilinda shamba lao!
   
 14. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #14
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Hivi kati ya daktari asiyelipwa na viongozi wa serikali wasiowalipa madaktari nani ana makosa?
   
 15. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #15
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,719
  Likes Received: 1,628
  Trophy Points: 280
  mmesikia swali? wanasema Dk Kigwa kugoma ni sawa hii ni kama ile ya ITV mie nasema ni sawa ila usiniulize ni kwanini maana hamna swali kama hilo
   
 16. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #16
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Jamani ndugu zangu kiukweli serikali sio sikivu kabisa, kama wangeliwalipa madaktari stahili zao na kuwaacha kwenye vituo vyao na kuwaomba msamaha hivi tusingekua tunaendelea na mjadala huu na hata sauti ya mbunge huyu ingeishia moyoni mwake.

  Lakini serikali yetu imekuwa ikifanya kazi kwa visasi na kukomeshana na hapa ndipo matatizo huanzia. Hivi kulikua na haja gani ya kuwahamisha hao madaktari? Au ni kwasababu wametudai posho yao ngoja tuwakomoe. Hao ni madaktari wanafunzi na muhimbili inavifaa vingi ktk taifa hili, hivyo mngewaacha hapo wajinoe vilivyo ili tupate madaktari wazuri.

  WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII inatakiwa muwajibike kwa hili.
   
 17. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #17
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  msionee kingwangala...any one can become a mbunge but not a human doctor
   
 18. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #18
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Wengi tunafanya kazi serikalini lakini hatuna visasi wala dharau.nimechoka kusikia serikali ina tatizo,sio kweli kuna watu wachache sana serikalini wanaharibu nchi hii,nasema wachache sana na wanatakiwa kushughulikiwa otherwise serikali yote itaingia matatani na wananchi wake.

  Tufike sehemu tuache kulaumu system ambayo ina waadilifu wa kutosha,tuwaisolate wale wachache wenye viburi vya madaraka.
   
 19. zimmerman

  zimmerman JF-Expert Member

  #19
  Jan 20, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 579
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 80
  Siasa ndio inayoharibu serikali. Hasa hao viongozi wa kisiasa wanaowekwa na wanasiasa kuongoza watendaji. Hivi chukulia mfano kama UDSM, hivi kuna mantiki gani Vice Chancelor kuteuliwa na Rais? Hiki ni chuo kikuu kazi yake ni kufanya tafiti za kisayansi kwa matatizo yote yanayomkabili mwanadamu, kutoa elimu bora inayotokana na matunda ya tafiti hizo na kutoa ushauri bora kabisa kwa jamii kwa yanayowasibu. Wanataaluma wenyewe ndio walipaswa kabisa kupendekeza kwamba fulani kutokana na utumishi wake uliotukuka katika chuo chetu anapaswa kutuongoza. Lakini sisi kawekwa pale mtu kwa sababu tu za kirafiki na kupongezana kati ya Rais na mtu mwenyewe. UDOM vile vile. Muhimbili, vile vile. Idara zote za serikali, vile vile. Haya yote yanapaswa kuzungumziwa kwenye katiba mpya. Ni marufuku kuwepo na vyeo vya kuteuliwa na mwanasiasa. Uongozi wote utokane na CV ya kiongozi.

  So system yote inalaumiwa kwa sababu wanasiasa ndo wanaongoza system badala yai system kuongoza wanasiasa.
   
 20. F

  FEELINGS Member

  #20
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 30, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ".....Hamisi Kigwangala kugomesha madaktari wenzake,.." Yeye ni nani hata awagomeshe wenzake!? hilo ni tusi kwa madaktari wetu. Wanataka kutuambia miaka yote mitano waliyosota kupata huo udakitari hwafahamu haki zao mpaka mtu awaambie wagome!!? waandishi waache sentensi za kisiasa na watawala.
   
Loading...