Dr Garang roho za wa south Sudan zinakulilia ,approach yako ya Guerilla war bado inawatafuna

craq

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
859
1,865
Jimbo la Catalonia inapatikana kaskazini mashariki ya Spain ni moja ya jimbo ambalo linapigana kujiengua na kudai Uhuru wao.Ni miaka sasa tangu Catalonia kudai haki yao ,tukiangaazia nyuma alikuwepo mtawala dictator nchini Spain General Franco ambaye aliwachukia mno wacatalunya na kuwapendelea mno Castilians "wanaopatikana Madrid.Franco alipiga marufuku lugha ya ki-catalunya kuzingumzwa ,bendera za catalunya kupepea nk na pia kulikuwepo na tukio mashuhuri ambayo ilitokea ,klabu ya Barcelona inayopatikana catalunya ilikuwa inacheza na Real Madrid kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la copa del rey mechi ya kwanza Barcelona iliibuka na ushindi wa magoli 3 kwenye mchezo wa marudiano dictator Franco aliwapiga mkwara wachezaji wa Barcelona na kuwaambia endapo wasiporuhusu kufungwa magoli 11 basi wangeuliwa na kweli kwenye mechi ile Real Madrid iliwafunga Barcelona magoli 11 hiyo ilikuwa Franco Era .Catalunya kwa nyakati tofauti wamekuwa wakipigania Uhuru wao wa kutambulika kama taifa kamili kupitia bunge,memorandum nk.na saizi wamefikia hatua nzuri ni hivi karibuni wananchi wa Catalunya walipiga kura kama wanataka kujitenga au wasijitenge,matunda yanaanza kuonekana.

Leo hii catalunya wakipata Uhuru wao watakuwa na maendeleo makubwa ,sababu miji yao imejengeka ,kuna mahospitali makubwa mfano hospitali ya Barcelona inafanya research kutafuta tiba ya ukimwi na mwanga wa dawa ya ukimwi ishapatikana kuna mwanaume alikuwa na maambukizi ya ukimwi tangu 2009 lakini alipona baada ya madaktari ku transplant damu kutoka kwenye umblical cord na bado wanaendelea na utafiti.

Wana vyuo ,miundo mbinu nzuri ,timu za mpira kama Barcelona,Espanyol ambazo zinatamba.

Endapo wakichukua Uhuru Taifa la Catalonia haitokuwa na shida,kasumba yeyote sababu governors wao,rais kivuli walifanya kazi kubwa kuhakikisha wanaletewa maendeleo kutoka kwenye serikali kuu wakati wakiendelea na kupigania Uhuru.


90c73b7c59e8612f1edff91019e7c664.jpg


b5aba1d29269bb2c24c8d3a24ab99078.jpg


71ddcf8dd79e78e17e0070b0565733b5.jpg


Barcelona

2.case nyingine ni Zanzibar ni moja ya jimbo ambalo lina ukakasi wapo wanaopigania watambulike kama taifa kamili ,wapo wanaodai serikali 3 pia wapo ambao wanataka hali ibaki kama ilivyo.kwa namna moja au nyingine Zanzibar kuna maendeleo kwa kiasi chake ,idadi ya wasomi ni kubwa ,miundo mbinu angalau inaridhisha ,watalii wanapata nk ,endapo wale wanaotamani wawe Zanzibar ipate mamlaka kamili wakifanikiwa basi Zanzibar haitopata tabu sababu idadi ya shule,hospitali, wasomi ipo kubwa na nyanja zingine lakini Zanzibar hawana ushirikiano kama catalonia.asilimia 99 kama sio 100 ya wa Catalunya wana msimamo mmoja lakini Zanzibar ni minorities tu wanataka mamlaka kamili ,wengine wapo ccm wengi wakitaka hali hii iendelee na wengine wapowapo tu.

415e7ee680e2bbed4d888080ccfb38c4.jpg


87118d901292eb3f69d027329ea8fd05.jpg


Zanzibar

3.South Sudan

Nimesoma habari Jana kwamba watu 20,000 ndani ya wiki hii wameyakimbia makazi yao Sudan kusini na kuelekea white Nile kutokana na vita vinavyoendelea kwa mujibu wa UNHCR na wengine 50,000 wanatizamiwa kukimbia ila kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha wamekwama.

Takwimu pia zinazoenyesha watu 375000 wamekimbilia Sudan kupata malazi na 1million wapo duniani kote kujihifadhi.

Leo hii idadi ya waliosoma ya wasudan kusini ni asilimia ndogo ndogo sana ,maendeleo 0, shida ,njaa nk.

Mimi binafsi lawama namtupia Dr Garang na wenzake approach waliyotumia mpaka leo inawatafutana baada ya civil war na treaty yao angetulia na kupigania maendeleo yafanyike eneo lake huku akipigania mamlaka kamili kwa njia mbadala lakini alitumia njia ya guerrilla war miaka kwa miaka na siku zote sehemu penye vita "juba" maendeleo hayatokuwepo kivyovyote vile,leo hii hamna shule ,waliosoma ni diasporas tu.

South sudan mamlaka kamili wangepata tu sababu

1.ukiondoa utofauti wao wa ukabila wote walikuwa na msimamo mmoja ya kutaka mamlaka kamili hivyo AU,UN wangewapa pressure Bashir na mamlaka kamili yangepatikana.


f19756cbe1896a318b2c43630455ee78.jpg


Leo hii watoto wa waheshimiwa wanatembelea vog ,vx wakisomesha watoto wao Nairobi,south Africa huku million ya wananchi wakikimbia,kimbia ,wakiendelea kufa ,vijana bado wanatumika kwa mabwana zao ,njaa inawakabili.

Dr Garang approach uliyoitumia bado inawatafuna wa south Sudan.Roho zao zinakulilia na zitaendelea kulilia

Tanbihi: Zanzibar mna bahati mlipata viongozi wenye hekima la sivyo mngepotea.
 
Ni changamoto kwa AU,ukabila umezidi Africa.Binafsi sioni kama Dr Garang ni Muunganishi Bali naona dalili za ukabila na kulewa madaraka.Angeitumia vizuri hiyo Nafasi ya kuwa Raisi wa kwanza, nchini humo angejijengea historia iliyotukuka na kukumbukwa vizazi na vizazi badala ya kuishi leo tuu.
 
Ni changamoto kwa AU,ukabila umezidi Africa.Binafsi sioni kama Dr Garang ni Muunganishi Bali naona dalili za ukabila na kulewa madaraka.Angeitumia vizuri hiyo Nafasi ya kuwa Raisi wa kwanza, nchini humo angejijengea historia iliyotukuka na kukumbukwa vizazi na vizazi badala ya kuishi leo tuu.
Dr, garang alikuwa kabla ajamaliza na kupata Uhuru wa Sudan kusin hajawai kuwa raisi
 
Ipo siku raia watakimbia wote na hapo ndipo watakapoanz kuuana viongozi wachache waliopo
 
Back
Top Bottom