Dr Festus Limbu (Magu MP)?

Kwani yeye ni daktari wa nini?

Ni daktari wa PhD ya Uchumi, Thesis ameandika kuhusu mambo ya Agricultural Marketing System hapa Tanzania. Ameisomea Ujerumani.

Alikuwa Lecturer wa UD kabla ya kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Magu.

Lakini pia ni opportunist mzuri sana. Aliporudi toka Ujerumani alikuta 'upepo wa mageuzi' ukivuma kuelekea NCCR. Akaombwa na Wazee wa CCM agombee, akasita akaamua kupitia NCCR. Marehemu Mzee Ernest K. Nyanda akamshinda. Baadaye Mzee Nyanda akafariki, wakaitisha uchaguzi mdogo, Limbu akaamua kwenda kutubu kwa CCM, wakampitisha agombee, akadondoshwa na John Momose Cheyo (UDP). Finally, mwaka 2000 ndipo aliposhinda na kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Fedha.

But I guess kuna madudu aliyanusa akiwa hapo Wizarani. Mwaka 2005 hakuwekwa kwenye Baraza la JK na ndipo nikamshangaa anauliza swali Bungeni kuhusu Alex Stewart, wakati hiyo kampuni ilipokuwa ikipewa tenda ya kushughulikia Kampuni za Madini, Dr. Limbu alikuwa Naibu Waziri wa Fedha. I expected kwamba angeweza kuwa na info zote maana ndiye alikuwa Naibu wa Mramba (Mzee wa Kula Majani).
 
Keil Mzee Nyanda alifariki kabla ya uchaguzi wa 1995. Katika uchaguzi huo ccm walimsimamisha Bwana Lupondije na akamshinda Dk. Limbu na wagombea wengine wa upinzani. hata hivyo naye hakudumu sana, alifariki pia. uchaguzi ulipofanyika Cheyo wa UDP alishinda kwa kumshinda Dk. Limbu aliyekuwa CCM kwa wakati huo.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom