DR Congo: 48 Wanabakwa kila saa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DR Congo: 48 Wanabakwa kila saa

Discussion in 'International Forum' started by kilimasera, May 12, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 12, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Utafiti uliofanywa na wanasayansi wa Marekani umeonyesha kuwa takriban wanawake na wasichana 48 wanabakwa kila saa katika Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.

  Utafiti huo, uliochapishwa katika jarida moja la afya,umegundua kuwa wanawake 400,000 kati ya umri wa miaka 15-49 walibakwa katika muda wa miezi 12 kati ya mwaka 2006 na 2007.

  Idadi hii ni kubwa ikilinganishwa na idadi ya awali ya kuonyesha kuwa wanawake 16,000 wanabakwa katika muda wa mwaka mmoja iliyotangazwa na umoja wa mataifa.

  Serikali ya DRC inasema hali hii ya sasa inaonyesha kuwa wanawake wana nafasi ya kutoa taarifa zaidi juu ya matukio ya ubakaji.

  Ubakaji umekuwa kama jambo la kawaida katika mapigano yanayoendelea mashariki mwa Congo.

  Amber Peterman, mtafiti mkuu,anasema: "utafiti wetu umedhihirisha kuwa idadi ya matukio ya awali haionyeshi hali halisi ya matukio ya ubakaji yanayoendelea kujitokeza nchini Congo.
   
 2. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #2
  May 12, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Hua nashindwa kuelewa vita ni ya wenyewe kwa wenyewe, vita imekua triggered na ubishi wa wanaume (si wanawake) wa hio nchi - hasa hapo hua nashindwa kabisa kuwapata kwamba raha yao nini wakibaka hao wanawake? Kwamba one or both sides of the coin wanaweza pigana tu waki rape? Au kwamba itakua wana mganga (mana haya mambo Africa its possible) ambae kawapa masharti ya kushinda kua shurti m-rape wanawake? Tena hawajali binti ni mtoto, mtu mzima wala mzee - utafikiri wameshikwa na vichaa.... Inasemekana katika idadi yote nearly half a million women have been raped in Congo... Naamini watakua wamevunja record ya kubaka duniani....
   
 3. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #3
  May 12, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Utafiti wa kisayansi uliofanywa na wamarekani,..hapo mm ndipo sipaelewi sayansi gani iliyotumika kutafiti ....nafikiri hao wamarekani hao(wanasayansi sijui-pitfall so to speak)wanatafuta njia ya kujitukuza eti wamefanya tafiti za kisayansi,congo ni sawa kabisa kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwa pamoja na ubakaji wa wanawake ,lakn sio wakifanya maulizo ya juu juu wanaanza kujipambanua eti wanasayansi wa wapi mara wapi.........hizo ni gilibu na zisizo na maana.
   
 4. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #4
  May 12, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  IGWE ni kweli kua US wana kichaa cha kutaka kua Mungu but utofautishe kati ya kazi zinazofanywa na serkali ya US na shughuli zinazo fanywa na baadhi ya hummanitarians na mashirika yao ya kimataifa.. Although hata mashirika yenyewe ya US government wanafanya kazi nzuri in terms of research ... Kua wanawake wa ki Congo wanabakwa si maslaha... tena mtu mmoja anabakwa hata na watu zaidi ya kumi... Yaani siwaelewi maana victims are left alive to tell the story... Hasira tulio nayo juu ya US isi cloud our judgement na we have to face the truth of what the women in Congo are going through...

  women raped every day in Congo, study finds

  Researchers cite 'chronic under-reporting due to stigma, shame, perceived impunity'


  [​IMG]
  Pete Muller / AP, file A mass rape victim comforts her son in the town of Fizi, Congo, on Feb. 20. She was among nearly fifty women who were raped by Congolese soldiers on the night of Jan. 1. Her son suffered a head wound when soldiers threw him to the ground prior to the rape. A court later sentenced an army colonel to 20 years in prison, convicting him of crimes against humanity.

  msnbc.com staff and news service reports
  updated 5/11/2011 7:08:36 AM ET

  More than 1,100 women are raped every day in Congo, a study published in the American Journal of Public Health on Tuesday concluded. The study found that more than 400,000 women aged between 15 and 49 were raped during a 12-month period in 2006-2007, AFP reported.
  The findings put the number of rapes at 26 times higher than a previous report from the United Nations, which said the number was 15,000 for the same period.
  "Our results confirm that previous estimates of rape and sexual violence are severe underestimates of the true prevalence of sexual violence occurring," Amber Peterman, lead author of the study, told AFP.
  The study reportedly did not gather data on sexual violence among boys and men, or in girls younger than 15 and older than 49.
  "Even these new, much higher figures still represent a conservative estimate of the true prevalence of sexual violence because of chronic underreporting due to stigma, shame, perceived impunity, and exclusion of younger and older age groups as well as men," Peterman said.
  The study also gave mention to a Human Rights Watch report that sexual violence in Congo doubled from 2008 to 2009.
  The giant Central African nation was mired in civil war from 1996-2002, and the east remains awash in weapons and rebel groups who terrorize civilians.


  The Associated Press and msnbc.com staff contributed to this report.
   
 5. M

  Mzee2000 JF-Expert Member

  #5
  May 12, 2011
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 491
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Hi ni propaganda , in the uk there were 12,165 reported rape during 2008/09 na hizo ni reported,je ukujumlisha zile ambazo polisi hawakujulishwa?
   
 6. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #6
  May 12, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Ubakaji uko dunia nzima hata hapa Tanzania mpaka kwenye ngazi ya household ambalo hakuna vita. Tofauti ni namna na nia ya kutoa taarifa tu. Huko DRC taarifa hazikufikishwa na raia ambaye ni mhanga wa ubakaji ziliripotiwa na mfanyakazi wa peace keeping. Kwa DRC ambayo imetopea kwenye vita vya kugombea utajiri wa madini kubaka ni Kama kutongoza tu.

  Hapa Tanzania tunasikia matukio ya baba mwenye nyumba katembea na hausegirl, binti kabakwa na kijana wa Jirani, na unaona kabisa wazazi wakiwa mbele kuzuia habari Kama hizo zisifike polisi ili jamii isijue.

  Umefika wakati vitendo vya ubakaji vikatangazwa Kama janga la taifa, tuvikemee kwa nguvu zote kinyume cha hapo vitaendelea Kama unavyoona Congo
   
Loading...