Dr. Bilal: Nitaongoza nchi kisayansi

Dr. Bilal: Nitaongoza nchi kisayansi

Huyu kakosea njia badala kwenda hospital kaenda kuchukua form,alitaka vipimo vya kisayansi maabara sasa kesho atarudisha form na kuomba samahani.na hiyo misayansi atumie kipindi kilichobaki.home mzee umechoka,kumbe patamu hapo.
 
Haaa haaa wewe ndio utakuwa unajidhalilisha au umekubali kushikiwa akili au umekariri hutaki kuifikirisha akili yako au vyote kwa pamoja.

Mosi, Jamhuri ya muungano Tanzania ni muungano wa nchi mbili ambazo ni Tanganyika na Zanzibar.Tanganyia haipo Zanzibar ipo.

Pili, Zanzibar ipo ina rais wake anapigiwa mizinga 21 kwakuwa ni mkuu wa nchi,ina bendera yake ya taifa la Zanzibar,ina baraza lake la wawakilishi kazi yake kuu ni kutunga sheria kwaajili ya nchi ya Zanzibar,ina vikosi vyake vya ulinzi na usalama,ina mawaziri wake wenye hadhi sawa na mawaziri wa JMT,Zanzibar ni nchi yenye mipaka yake,Zanzibar ina wananchi wenye uraia wa Zanzibar !.Wewe ukienda Zanzibar huna haki ya kuchagua wala kuchaguliwa lakini ukienda Tanga,Kilimanjaro au Lindi maadamu una kitambulisho cha kupiga kura una haki ya kuchagua na kuchaguliwa,Ukienda Zanzibar huwezi kumiliki ardhi ya nchi ya Zanzibar lakini mzanzibar akija huku Tanganyika ana haki ya kumiliki ardhi,haki ya kuchaguliwa na kuchagua.Mzanzibar ana uraia wa nchi mbili mosi ni raia wa Zanzibar pili ni raia wa Tanzania.Mtanganyika ana uraia wa nchi moja tu nayo ni mtanzania tu haki zake zipo ndani ya mipaka ya Tanganyika tu akienda Zaznibar yeye ni mgeni sawa na raia wa Kenya,Uganda au Msumbiji.

Tatu,Ukirejea hoja yangu ya kwanza ukaielewa hapa utakuwa kama unamsukuma mlevi.Ni hivi kama unakubali muungano ni baina ya nchi mbili Zanzibar na Tanganyika mbona Zanzibar ipo ina serekali yake lakini Tanganyika haipo.Ukiwa rais wa Tanzania mamlaka yako yanaazia wapi na kuishia wapi ?.Jibu ni rahisi sana kama utapenda kuishughulisha akili yako kiduchu.Mamlaka ya rais wa Tanzania yanaanzia Tanganyika na kumalizikia Tanganyika.Bunge la JMT kule Dodoma linatunga sheria kwaajili ya Tanganyika ingawa liaitwa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwakuwa sheria zote zinazoigusa Zanzibar lazima zipelekwe baraza la wawakilishi kwaajili ya kuridhiwa.

Ni haramu na matusi makubwa ikiwa rais wa Tanzania atatoka Zanzibar ikiwa katiba ya Zanzibar itabaki kama ilivyo sasa.

Tafakari chuku hatua


We mbona unajidhalilisha? Kwani inatawaliwa Tanganyika au Tanzania? Mi ndo kwanza weye nikuskie kuwa rais anatawala Tanganyika, hahahahaa!! Hakuna nchi inayoitwa tanganyika wewe!!!
 
Back
Top Bottom