Dr. Bilal: Nitaongoza nchi kisayansi

Dr. Bilal: Nitaongoza nchi kisayansi

Cardinal06

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2015
Posts
963
Reaction score
327
Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal amesema nchi inaendelea kupoteza maadili, hivyo kuahidi kusimamia uwajibikaji katika sekta ya umma endapo atapitishwa na CCM na kisha kuchaguliwa kuwa rais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu ya kuomba kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi huo, Dk Bilal alisema Serikali yake haitavumilia uvunjwaji wa miiko ya uongozi.

Huku akisisitiza kuwa kaulimbiu yake, ni Mabadiliko ndani ya Umoja, Dk Bilal alisema vipaumbele vyake ni kusimamia matumizi mazuri ya rasilimali za Taifa na kuboresha na kusimamia matumizi ya mapato.Alitaja kipaumbele kingine kuwa ni kulinda haki za binadamu na kuhakikisha nchi inasimamiwa kwamisingi ya sheria.

"Nitahakikisha Serikali ya Awamu ya Tano inaendelea, kusimamia na kuimarisha utawala wa sheria, haki za binadamu, haki za kina mama na watoto, walemavu hasa wa ngozi, haki ya kuunda na pamoja na uhuru wa kupata habari. "

Dk Bilal alisema atahakikisha analinda misingi ya utaifa ulioasisiwa na wazee na ambayo imelifikisha Taifa katika miaka 54 likiwa moja, imara, lenye upendo na mshikamano.

Alipotakiwa kuwatoa hofu watu wanaodhani kuwa ana mitazamo ya kihafidhina, Dk Bilal alisema yeye ni mwanasayansi na siku zote sayansi inabadilika kulingana na mazingira.

"Hakuna uamuzi uliokuwa sahihi zaidi ya uamuziwa kisayansi. Mimi siku zote uamuzi wangu unafuata utaratibu huo, ndivyo nilivyolelewa na kufunzwa na nitaendelea kuongozwa kisayansi," alisema.

Akijibu swali lililomtaka afafanue mtazamo wa watu kwamba sasa ni zamu ya Zanzibar kutoa Rais, Dk Bilal alisema chama chake hakina vitu hivyo, bali kinachagua kiongozi au mwanachamaambaye ataweza kuwavusha.

"Hatujali wapi ametoka, hatujali rangi yake, hatujali kabila lake, hatujali dini yake ilimradi ni Mtanzania. Mimi ninadhani ninaweza kulivusha Taifa hili," alisema.

Alisema amejitokeza kwa sababu anayo hamu na uwezo wa kulifikisha Taifa liwe la kutiliwa mfano.Alisema Muungano ulivyo hivi sasa si kama hapo zamani, sasa unakabiliwa na changamoto nyingi zaidi kwa hiyo ni jukumu lake kuhakikisha kuwa anashirikiana na wadau mbalimbali ili kutatua changamoto zilizopo.

Hali ilivyokuwa
Kabla ya kuingia ndani ya ukumbi, wakati na baada ya kuzungumzia na waandishi wa habari, Dk Bilal alikuwa akishangiliwa na wapambe wake kila mara alipojibu swali la mwandishi au kumaliza hatua moja kwenda nyingine.

Mbali na kushangiliwa wakati anaingia baadhi yawapambe walijipanga nje ya mlango wa kuingiliajengo la makao makuu kwa ajili ya kumlaki. Alisindikizwa kwa nyimbo za hamasa za CCM naza kumpongeza.

Wapambe hao na baadhi ya watumishi wa ofisi za makao makuu ya chama walikuwa wamevalia mavazi yenye rangi za chama. Baadhi ya nyimbo zilizosindikizwa na makofi ni pamoja ‘Dk Bilal tutamlinda na kumtetea'.

Dk Bilal ni nani?
Alizaliwa Februari 9, 1945 na kuhitimu Shule ya Msingi Makunduchi mwaka 1958. Aliendelea na masomo ya sekondari katika Shule ya Beit-el-Ras mwaka 1962 na baadaye Lumumba zote za visiwani Zanzibar.

Kabla ya kuhitimu kidato cha tano, alipata ufadhili wa kwenda kusoma Marekani katika Chuo Kikuu cha Howard na kuhitimu Shahada yaFizikia na Hesabu mwaka 1967. Dk Bilal aliendelea na masomo ya Shahada ya Uzamili ya Fizikia na kuhitimu mwaka 1969, kisha alianza kufanya kazi akiwa mhadhiri msaidizi na baadaye kuwa mtafiti msaidizi katika Kampasi ya Berkely katika Chuo Kikuu cha Carlifonia.

Mwaka 1976, alitunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD), ya Fizikia chuoni hapo. Baadaye, alijiungana Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akiwa mhadhiri na mwaka 1983 alipandishwa cheo hadi kuwa Mkuu wa Idara ya Fizikia ya Nyuklia.

Dk Bilal alishiriki katika ukuzaji wa sekta ya nyuklia nchini kwa kuwa mmoja wa walioanzisha taasisi ya Serikali inayoshughulikia masuala ya mionzi na mwaka 1988 aliteuliwa kuwa Mkuu waKitivo cha Sayansi cha UDSM. Mwaka 1990 alipandishwa cheo na kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu.

Safari ya kisiasa ya kada huyo wa CCM ilianza mwaka 1995 alipoteuliwa kuwa Waziri Kiongozi katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hadi mwaka 2,000 aliporithiwa na Shamsi Vuai Nahodha. Mwaka 2010, mwanasayansi huyo aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Makamu wake baadaya Ali Mohammed Shein kuchaguliwa kuwa Raiswa SMZ.


Chanzo: Mwananchi
 
kumbe urais ni kitu rahisi hivyo,nami ningekuwa na katumilioni ningechukuwa fomu lol!
 
sayansi ni pana sana kuliko idadi ya vinyweleo vyake.Sijui km anajua anchosema na nini ktk anavyodhani ktk sayansi vinaweza msaidia kuongoza?Km alishindwa isaidia sana TZ ktk uranium akiwa km mtaalamu wa atomic akakimbilia ktk siasa huku akiwa busy na mkasi ataweza vipi nchi?Kwanza tutengependa jua shida yake ya kusikia baridi full time na kuongea kwa timing imeanza lini na nini?
 
Daaah, kuna watu kweli wana tamaa ya madaraka, hivi huyu kwa nafasi aliyonayo anakosa nini hadi atamani urais
 
Huyu nayeee!!!

Leo hii anapolalamika kuporomoka kwa maadili,ye yuko wapi?
Si

Wasituchanaganye hawa.
 
Huyo si alikuwa na au yupo kwenye uongozi, kipi kafanya cha maana?

Unaaandika km Shangazi mpika maandazi.
Unataka utajiwe kimoja kimoja alichokifanya Nchi hii? We muhutu au?
Km ni Mtanzania Basi lzm utajua Mchango wake. Muulize muajiri wako Atakupa ripoti za Huyu Dr.

Galatia wahed!
 
Kuna wazee wana utani...

Miaka 10 ya umakamu wa urais kafanya nini zaidi ya kuzindua visima...?
 
huyu babu akiongeaga huwa nahisi muda wowote anadondoka chini na roho inaacha mwili!!!!too damn old with that sick vibrating tone....enjoy your pension old man.
 
Kipi kilichomshinda kuendesha nchi kisayansi kama Makamu wa Rais hadi asubiri kuwa Rais ndiyo atumie hiyo sayansi yake kuendesha nchi? Na hii sayansi yenyewe anayozungumzia ni sayansi ipi?
 
Huyu ni raia wa nchi ya Zanzibar,Wazanzibar wana uraia wa Zanzibar hala wana uraia wa hiyari wa Tanzania ambao mara nyingi hawautaki kabisa wanautumia pale unapokuwa na manufaa kwao mfano passport,kupata viwanja,mashamba na nk huku Tanganyika.Zanzibar ina wimbo wake wa taifa,ina bendera yake,ina vitambulisho vya utambulisho wa mzanzibar,ina bunge lake ukipenda liite baraza la wawakilishi ambalo sheria zake zina nguvu kuliko sheria zinazopitishwa na bunge la JMT.

Kumteua Dr Bilal kutawala Tanzania ni matusi makubwa kwa raia wote wa Tanganyika kwasababu zifutazo.

1. Dr Bilal ni raia wa nje (nchi ya Zanzibar) Tanganyika kutawaliwa na raia wa kigeni haiwezekani bora kabisaaa.

nch ipi hiyo atakayoongoza huyu?
 
He is the second person from top, why can't do all these. Huu ni ubabaishaji. Kimemshinda nini kufanya akiwa hapo kwa miaka kumi? Huyu anaongeza genge tu
 
sasa hivi inaongozwa kichawi?....mana yeye ni makamu wa rais
 
Huyu ni raia wa nchi ya Zanzibar,Wazanzibar wana uraia wa Zanzibar hala wana uraia wa hiyari wa Tanzania ambao mara nyingi hawautaki kabisa wanautumia pale unapokuwa na manufaa kwao mfano passport,kupata viwanja,mashamba na nk huku Tanganyika.Zanzibar ina wimbo wake wa taifa,ina bendera yake,ina vitambulisho vya utambulisho wa mzanzibar,ina bunge lake ukipenda liite baraza la wawakilishi ambalo sheria zake zina nguvu kuliko sheria zinazopitishwa na bunge la JMT.

Kumteua Dr Bilal kutawala Tanzania ni matusi makubwa kwa raia wote wa Tanganyika kwasababu zifutazo.

1. Dr Bilal ni raia wa nje (nchi ya Zanzibar) Tanganyika kutawaliwa na raia wa kigeni haiwezekani bora kabisaaa.

We mbona unajidhalilisha? Kwani inatawaliwa Tanganyika au Tanzania? Mi ndo kwanza weye nikuskie kuwa rais anatawala Tanganyika, hahahahaa!! Hakuna nchi inayoitwa tanganyika wewe!!!
 
Back
Top Bottom