Dr.Ben Jochannan: Mtu Mweusi,Amka

mkuu tembelea mapiramidi ya misri au tafuta tu documentary zake utaona kuwa kwenye michoro iliyomo kwenye zile temples ni watu weusi,jet black
unaniambia waethiopia sio weusi!!!
Mcheki Haile salaise,si mweusi. kuna yule jamaa Mariam Mangtse kama sijakosea jina. alipofanya mapinduzi alikuwa anaogopa kujitokeza sababu alikuwa mweusi na haonekani kiethiopia. waethiopia wamekomesha utumwa mwaka 1931.na watu weusi ndiyo hasa walikuwa watumwa. huwa nafikia mkataa kwamba waethiopia siyo weusi. ila ntacheki hizo documentaries nizidi kujifunza.
 
wote wana kinky hair(nywele ngumu),wote ni weusi lakini light skinned

 



Sasa kaka,sababu wewe umetuleta maandiko ya mtu huyu,mimi kuna maswali naomba unijibu badala yake.

1. Kwa mababu zetu mwaka ulikuwa una miezi mingapi ?

2. Siku mpya ilikuwa inabadilika saa ngapi ?

3. Mababi zetu walijuaje kama jambo hili ni baya na hili ni zuri ?

Hayo ni maswali machache tu ya kuanzia.

Kuna kitu tubakiwa tukijue kwamba "UNAWEZA KUKOSEA KATIKA KUKOSOA"

Naanzia hapa
 


Cha kusikitisha ni kuwa muhudhirishaji wa huu muhadhara amelitumia tamko "Zamani" kama kichaka.

Alitakiwa anaposema zamani basi awe amedhibiti muda kwa maana tarehe,kielimu kama hujadhibiti muda na mfano wake sisi tunasema ni kulalama.

Kama anasema ya kuwa binadamuwa kwanza hakuwa ni Adamu,basi atuambie binadamu wa kwanza alikuwa bani nq alikuwa na sifa gani na utamaduni wake ulikuwaje ?

Lakini kuendelea kukariri zamani zamani hizo zina kuwa "Visasili vya muafrika na ngano nyinginezo".
 
1. mwaka ulikuwa na miezi kumi na tatu

2. hapa sina jibu la haraka,mpaka nikachimbe kwa ancestors kwanza

3. natural instincts,ndio maana kwenye "the egyption book of the dead" kuna makatazo 42 ambayo kila mtu alitakiwa kutoyafanya,ancestors walilay down zile moral teachings ili kuwaweka watu kwenye mstari,bahati mbaya,wakristo na waislamu miaka elfu kadhaa baadae walicopy na kusema ni maandiko ya mungu
 
kabla hatujafika huko mbali unakubali kuwa kabla ya adam na eva wa kwenye biblia kulikuwepo watu wanaishi tena kwa miaka zaidi ya 8000 kabla ya akina adm na eva wa kwenye biblia?
 


Kwanza kabisa hapo kwa mtume amani iwe juu yake,amesema uongo wa wazi kabisa. Kwanza hakuna mtu anayeitwa "Bilal bin Rahab" sahihi ni "Bilal bin Rabah".

Halafu mlalamikaji hajatuambia kwamba swahaba Bilal Allah amridhie alimfundisha nini mtume amani ya Allah iwe juu yake ?

Halafu kwanza alitakiwa mtu huyu kabla hajaanza kulalamika angefanya utafiti wa kina sana,tatizo watu hawa huwa hata hawajui wapi au kwa nani akachukue elimu.


Mtume wetu sisi hakuwa na haja ya kujua wala kutaka msaada wa kusomeshwa na kuandika. Kutojua kwake kusoma na kuandika ndio ulikuwa alama au muujiza mmojawapo aliopewa na Allah aliyejuu.

Sasa atuambie au umsaidie kujibu swahaba Bilal bin Rabah alimfundisha nini mtume amani ya Allah iwe juu yake ?
 
kabla hatujafika huko mbali unakubali kuwa kabla ya adam na eva wa kwenye biblia kulikuwepo watu wanaishi tena kwa miaka zaidi ya 8000 kabla ya akina adm na eva wa kwenye biblia?


Sikubali.
 
mambo ya bilal alimfundisha nini ni thread in its own right
kabla hujasema kuhusu tafiti kwa GRAND MASTER DR.Ben,kwanza katafiti historia yake na ubobezi wake
 
Sikubali.
kama unaamini kuwa adam na eva ni watu wa kwanza hapa duniani,tuambie walikuwepo hapa duniani mwaka gani/waliumbwa na huyo yehova miaka mingapi iliyopita?
 


Kaka jibu la tatu nina lipinga sababu ya udhaifu wa binadamu ambao ni silika yake ya kutokukamilika. Je unafikiri sheria zao zilikuwa sawa ?

Je kipi kilikuwa kipimo chao cha ukamilifu ?

Je unaweza kutupatia makatazo hayo 42 ili tuweze kuyajadili moja baada ya jingine ?

Pili,mababu zetu mwezi wao ulikuwa una siku ngapi ?

Je ni wapi tutapata habari za mababu zetu,yaani historia za mababu zetu ?
 
makatazo 42yapo kwenye kitabu kinaitwa the papyrus of ani,the egyptian book of the dead,hata ukigoogle unakipata
kama nakumbuka vizuri miezi yote ilikuwa na siku 30
wapi nimesema walikuwa wakamilifu?
 
Sikubali.
biblia inaonyesha kulikuwepo watu wengine wanaishizaidi ya adam,eva,cain na abel

According to Genesis 4:1-15, Eve give birth to Cain and Abel. This, according to some Christians, implies that there were only four family members on Earth at that time. Now, after Cain had killed Abel there were only three people. But after Cain had slain his brother God appears to him and kicks him out of the Garden of Eden as punishment. Cain then moves to the land of Nod, which is East of Eden, but what Cain then says to God is quite revealing. He tells God that he was worried of being killed by other people who would find him (Genesis 4:15). Then God replies, “Therefore whoever kills Cain, vengeance will be taken on him sevenfold.” (Genesis 4:15) God and Cain both imply that there are other humans besides Adam and Eve. If there were no other people, God would not have had to give him a mark in the first place, and Cain would not have had anything to fear
 
kama unaamini kuwa adam na eva ni watu wa kwanza hapa duniani,tuambie walikuwepo hapa duniani mwaka gani/waliumbwa na huyo yehova miaka mingapi iliyopita?


Swali zuri kabisa,unajua kuna vitu vingine watu huwa hawakubali ya kuwa havijulikani na anaevijua ni Mola aliyetumba,sasa ubaya unakuja pale ambapo watu wanajidai ujuaji wa namba na kuleta hesabu za uongo.

Watu wanatakiwa wajue kwamba dunia imepitia vipindi vingi sana,vipindi ambavyo kulikuwa historia hainukuliwi. Historia ambazo tumekuja kuzijua kupitia mitume.

Kwa ufupi haijulikani Adamu aliumbwa mwaka gani,japokuwa masiku yalikuwepo,muda ulikuwepo na binadamu ndio kiumbe cha mwisho kuimbwa.

Mola wetu anasema "Hakika idadi ya miezi kwake yeye ni miezi kumi na mbili,tangu alipoumba ardhi na mbingu"

Hapo kwanza unatakiwa ujue kipindi ardhi na mbingu zinaumbwa binadamu alikuwa ni kiumbe kisichojulikana kiumbe ambacho kilikuwa hakitajwi.

Sasa mnapotuletea ususuavu wa moyo na urangi lazima elimu sahihi itakupita mbali.

Mtume wa Allah alisema miongoni mwa mambo ya kijinga ambayo hayataisha mpaka kiyama kina simama ni :

1. Watu kulia kwa kuomboleza misibani

2. Watu kujifaragu/ kujifaharisha kutokana na rangi,nasaba,vyeo

3. Pia kubaguana.

Mengine nimeyasahau,au kama alivyosema mtume wa Allah.
 
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…