PreGE2025 Dr. Askofu Stephen Munga: Nawapa pole CHADEMA kwa adha

PreGE2025 Dr. Askofu Stephen Munga: Nawapa pole CHADEMA kwa adha

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,881
Reaction score
828,458
1744395182593.jpg


“Siku ile kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa hao mitume.
Watu watauwa wakamzika Stefano, wakamfanyia maombolezo makuu.
Sauli akaliharibu kanisa, akiingia kila nyumba, na kuwaburuta wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani.”
(Matendo 8:1-3)

Hiki ni kipindi kigumu kwa chama cha siasa Chadema. Katika mtiririko wa matukio walianza na mivutano ya chaguzi zake za ndani. Chaguzi hizo zilikuwa na ushindani mkubwa, hasa kwa nafasi ya Mwenyekiti wa chama wa taifa ambapo Wakili Tundu Lissu alichaguliwa. Uchaguzi huo ulikigawa chama: walioridhika na wasioridhika na matokeo.

Baadhi yetu tuliona hayo kama mambo ya kawaida baada ya chaguzi na kwamba huwa majeraha yanapona polepole. Mvutano huu pia ulizaa mvutano mwingine wa kutokwenda pamoja katika dondoo yao kuu ya “no reforms, no election”. Hili nalo halikuwa gumu sana kulimaliza kwani inategemea ikiwa kauli na msimamo huo ni wa viongozi binafsi au ni maamuzi ya vikao vya juu vya chama.

Hali wangali wanavutana na wakati huohuo wakiuza sera yao hiyo ya “reforms, no election” wakakumbwa na tukio gumu la kule Mbinga, Songea ambapo pia wananchi waliohudhiria mkutanoni walitawanywa na jeshi la polisi kwa mabomu ya machozi. Katika tukio hilo mwenyekiti alikatwa na jeshi la polisi na kuchuliwa kwa Dar mahojiano na baadae kupelekwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka mnamo tarehe is 10/4/25 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, Dar es Salaam. Kulingana na hati ya mashtaka iliyosambazwa mitandaoni Lissu anakabiliwa na mashtaka ya “uhaini” kwa kusambaza taarifa za uongo na kuchochea uasi.

Hii ni kesi kubwa ya hatari lakini ambayo sio giza nene. Kwa kuwa kesi iko mahakamani basi tusubiri kuona itakavyokwenda na hukumu ya mwisho itakapotolewa. Nampa Lissu pole kwa yaliyompata.Tamanio letu kubwa ni kuona haki inatendekao.

Kwa uzoefu tunajua kwamba wanachama wa Chadema pamoja na familia ya Lissu wako kwenye maumivu na hofu kwa ajili ya adha hii iliyotokea. Bila shaka Chadema hawatatawanyika. Badala yake watasahau tofauti zao na kuungana pamoja chini ya uongozi wao uliopo ili kuvuka salama katika kipindi hiki kigumu. Tunahitaji vyama vya upinzani imara na vyenye nguvu kwa ajili ya kutunza uwiano na haki ya kisiasa. Pia ni kuitii katiba ya JMT ambayo inazungumzia TZ kama nchi ya utawala wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa:
Mungu ibariki Tanzania!
1744395188246.jpg
1744395182593.jpg
1744395193728.jpg
 
Kwani hiki ni chama cha kanisa? Mbona toka Braza K akamatwe matamko kutoka viongozi wa dini moja yamekuwa mengi?
 
Yaani Askofu mzima anafananisha mambo Yesu na Chadema

Hamna Askofu hapo Walutheri poleni

Ya Yesu hayafananishwi na kitu chochote
 
Kwani hiki ni chama cha kanisa? Mbona toka Braza K akamatwe matamko kutoka viongozi wa dini moja yamekuwa mengi?
Kile kingine kikongwe sio Cha bakuata,manake hatujawahi kusikia kikikemea uovu wa chama tawala; badala yake kinawaonya wapinzani kukaa kimya
 
Back
Top Bottom