DPP Tupilia mbali kesi zote za madawa ya kulevya zilizotengezwa na RC na Kamanda Sirro

EWGM's

JF-Expert Member
Jul 22, 2013
1,521
2,112
Ripoti iliyotolewa leo na Tume ya muda mfupi ya Nape Nnauye kuchunguza yaliyotokea Clouds yamedhibitisha bila shaka kuwa RC Bashite a.k.a Makonda na Kamanda Sirro walifanya ule mchakato kihuni na kwa hila.

Kama aliweza kuwatishia watangazaji kuwa watahusishwa na kesi za madawa ya kulevya hivyo pasipo shaka hata kesi zilizopita zimeshaingia najisi kwa sababu kutakuwa na walakini kwenye uendeshaji wa kesi hizo zote zinazowahusisha hawa wahuni wawili.

Tafadhali pia, mahojiano ya Kamanda Sirro na watuhumiwa wala yasitumike tena kama kielelezo cha ushahidi mahakani kwa sababu bila shaka Kamanda mwenyewe si msafi na kuna walakini mkubwa wa utendaji wake wa kazi kwenye kila kona kwa sasa. Yeye ni msimamia sheria za nchi zifwatwe lakini kushiriki kwake kwenye haramu hii moja kwa moja ama kupitia vijana wake basi amekosa sifa za kuliongoza jeshi la polisi.

Ofisi ya DPP na watendaji wake chukueni tahadhari hii ili muweze kunusuru kodi za wananchi na zikatumike sehemu nyingine inapostahiki na siyo kwenye mambo yaliyotengenezwa na genge hili la kihuni linaloongozwa na hawa watu wawili.

Tupilia mbali majarada yote shimoni na zile zilizopelekwa mahakani tayari tafadhali zifuteni sababu mtapoteza muda na kodi zetu.
 
Kama hujui namna DPP anavyofanya kazi yake bora ungekaa kimya tu mkuu! And by the way, Ripoti ya waziri ni ya upande mmoja tu! Haki ya kusikilizwa kwa mkuu wa mkoa haikuzingatiwa!
 
Kama hujui namna DPP anavyofanya kazi yake bora ungekaa kimya tu mkuu! And by the way, Ripoti ya waziri ni ya upande mmoja tu! Haki ya kusikilizwa kwa mkuu wa mkoa haikuzingatiwa!

Kwanini alikimbia kuhojiwa?? Mnataka kutufanya sisi watoto wadogo kuweka wahuni kwenye ofisi za serikali??
 
Sasa kama mkuu wa mkoa ameweza kutengeneza video kumchafua Gwajima unashangaa kutengeneza yale majina ya kihuni kama ya akina HOW COME MPEMBA au ROSE WA TANGI BOVU au MACHINE

Sema tu huyu dogo ana mahaba makali sana toka kwa mkuu wa nchi kiasi kwamba hasikii wala haoni. Huwezi kuwaita watuhumiwa na dawa za kulevya na kuwapa siku mbili, hata kama uliferi mara mbili mtihani wa darasa la nne na ulipata zero form four
 
Kama hujui namna DPP anavyofanya kazi yake bora ungekaa kimya tu mkuu! And by the way, Ripoti ya waziri ni ya upande mmoja tu! Haki ya kusikilizwa kwa mkuu wa mkoa haikuzingatiwa!
Kaone!!
 
Usipoteze dira na msingi wa hoja. Vita ya unga iendelee kwa utaratibu sahihi chini ya Kamishna Siang'a.

Na Makonda ashughulikiwe kinidhamu na kisheria kwa makosa aliyoyatenda.

Mamlaka husika zianze upya zoezi la madawa ya kulevya siyo kutumia yale majina ya hawa wahuni wawili
 
Kama hujui namna DPP anavyofanya kazi yake bora ungekaa kimya tu mkuu! And by the way, Ripoti ya waziri ni ya upande mmoja tu! Haki ya kusikilizwa kwa mkuu wa mkoa haikuzingatiwa!
hakutaka mwenyewe ni kama usipoenda mahakamani hakimu atakuhukumu. Huyu jamaa sana anadhani kuwa mkuu wa mkoa basi uanfanya kila unalotaka. lakini simlaumu maana hata kaka yake pia hajui madaraka yake pia.
 
Sirro na Daudi hawaelewani. Ni utii tu kwakua daudi ni Roman Catholic ila sio ma friend.
 
Sirro na Daudi hawaelewani. Ni utii tu kwakua daudi ni Roman Catholic ila sio ma friend.

Kwanini asiseme jamani mimi hili siliwezi tafuteni mtu mwingine sababu sheria haifwati. Yeyey ndiye anyesimamia sheria za nchi zifwate halafu akiwa anashiriki kwenye najisi kwa sababu ameshurutishwa aliingii akili kabisa
 
Kama hujui namna DPP anavyofanya kazi yake bora ungekaa kimya tu mkuu! And by the way, Ripoti ya waziri ni ya upande mmoja tu! Haki ya kusikilizwa kwa mkuu wa mkoa haikuzingatiwa!
stroke, sikuzote hua haujali. Hata argument zako ni za kuudhi.

Karma is Real, bigdog
 
Kama hujui namna DPP anavyofanya kazi yake bora ungekaa kimya tu mkuu! And by the way, Ripoti ya waziri ni ya upande mmoja tu! Haki ya kusikilizwa kwa mkuu wa mkoa haikuzingatiwa!

Back to your point,Ulitaka haki ipi aipate kama aliwakimbia hao watoa haki?
Mtu alikuwa radhi kupitia mlango wa nyuma kuikimbia tume bado unasema hakupewa haki.

Uungwana ni vitendo na hivyo tumsaidie kijana mwenzetu aweze ku realize kwamba alichokifanya ni kosa na anapaswa to the least kuomba msamaha.
 
Back
Top Bottom