DPP mpya aeleza mikakati

DPP mpya aeleza mikakati

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713

Biswalo-Mganga.jpg

Biswalo Mganga

MKURUGENZI mpya wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga, amewataka Watanzania wamwamini katika kazi na watarajie makubwa.

Kauli hiyo aliitoa jijini Dar es Salaam jana alipokuwa akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya simu muda mfupi baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na mtangulizi wake, Jaji Dk. Elizer Feleshi.

Alisema pamoja na kuteuliwa kuongoza ofisi hiyo, lakini hakuna aliyezaliwa na kujua kila kitu kwa siku moja huku akitaka Watanzania kuvuta subira.

MTANZANIA ilipotaka kujua mikakati na matarajio yake katika ofisi hiyo, alijibu kwa kifupi: "Huwezi kuwa na mtoto wako aliyezaliwa leo ukamuuliza uhusiano wa baba na mama, hapana kwanza tusubiri tusiwe na haraka.

"Ni mapema kusema nitafanya nini, kwanza acha tufanye kazi kwani hata wewe unapotoka nyumbani kwako kwenda kazini huwa una mipango, nami ninapenda kukwambia vuta subira," alisema DPP Mganga.

Uteuzi wa DPP Mganga umekuja huku akiwa Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Urejeshaji Mali zilizopatikana kwa njia zisizo halali.

Akiwa katika ofisi hiyo, DPP Mganga, alianza kujitokeza mwaka 2008 kwa kuendesha kesi za EPA pamoja na ya Samaki wa Magufuli ambazo aliweza kuzisimamia kwa uadilifu na Serikali kuweza kushinda.

Mbali na kushika nafasi hiyo, akiwa katika Ofisi ya DPP, alianza kazi kama Principle kabla ya kuwa Mkurugenzi Msaidizi.

DPP Mganga anatajwa kuwa mmoja wa wanasheria vijana ambao wamekuwa hawayumbishwi kwa nguvu ya fedha na muda wote amekuwa akisimamia maadili ya kazi yake.

Taarifa ya Ikulu iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Peter Ilomo jana, ilieleza kuwa Rais Jakaya Kikwete, amemteua Biswalo Mganga kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) uteuzi ambao ulianza Ijumaa iliyopita.

Kabla ya uteuzi huo, Mganga alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na Wakili wa Serikali Mfawidhi.

Awali nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Dk. Feleshi, ambaye aliteuliwa hivi karibuni kuwa jaji wa Mahakama Kuu.

Uteuzi wa Dk. Feleshi kushika wadhifa huo mpya ulianza rasmi Agosti 13 mwaka huu na aliapishwa Agosti 15 mwaka huu.

CHANZO: Mtanzania
 
Nyani walewale kwenye msitu mpya
 
hicho kitengo cha urejeshaji mali zilizopatikana kwa njia zisizo halali ndo sijawai sikia duniani mwenye kukijua tafadhali
 
hicho ni kitengo kipya, na yeye alikuwa mkurugenzi wake. kazi yake ni kupitia Tanzania nzima, wanaangalia kwenye kesi zinazoendelea na zilizoisha, kama kuna fedha bank zinatakiwa kuwa frozen wakati kesi inaendelea wanafanya hivyo ili mwizi asitapanye kuzikwepesha. kama kuna magari, nyumba au mali yeyote iliopatikana kwa wizi, yaani matunda yote ya wizi/proceeds of crimes, wanazikamata na kuzinyang'anya. ni kitengo kipya nimesikia kimeanzisha pale kwa dpp na kikiboreshwa kitakuwa mkombozi sana wa kupokonya mali za wezi.
 
Hute thanx kwa maelezo lakn kuna mwizi anaeombwa arudishe mali au
 
Last edited by a moderator:
Sijui kama kitaweza kufanya kazi...sana sana kitaonea wanyonge,ujambazi kama wa EPA,Meremeta,Escrow......watabaki kukodoa macho tu
 
Biswalo-Mganga.jpg

Biswalo Mganga

MKURUGENZI mpya wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga, amewataka Watanzania wamwamini katika kazi na watarajie makubwa.

Kauli hiyo aliitoa jijini Dar es Salaam jana alipokuwa akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya simu muda mfupi baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na mtangulizi wake, Jaji Dk. Elizer Feleshi.

Alisema pamoja na kuteuliwa kuongoza ofisi hiyo, lakini hakuna aliyezaliwa na kujua kila kitu kwa siku moja huku akitaka Watanzania kuvuta subira.

MTANZANIA ilipotaka kujua mikakati na matarajio yake katika ofisi hiyo, alijibu kwa kifupi: “Huwezi kuwa na mtoto wako aliyezaliwa leo ukamuuliza uhusiano wa baba na mama, hapana kwanza tusubiri tusiwe na haraka.

“Ni mapema kusema nitafanya nini, kwanza acha tufanye kazi kwani hata wewe unapotoka nyumbani kwako kwenda kazini huwa una mipango, nami ninapenda kukwambia vuta subira,” alisema DPP Mganga.

Uteuzi wa DPP Mganga umekuja huku akiwa Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Urejeshaji Mali zilizopatikana kwa njia zisizo halali.

Akiwa katika ofisi hiyo, DPP Mganga, alianza kujitokeza mwaka 2008 kwa kuendesha kesi za EPA pamoja na ya Samaki wa Magufuli ambazo aliweza kuzisimamia kwa uadilifu na Serikali kuweza kushinda.

Mbali na kushika nafasi hiyo, akiwa katika Ofisi ya DPP, alianza kazi kama Principle kabla ya kuwa Mkurugenzi Msaidizi.

DPP Mganga anatajwa kuwa mmoja wa wanasheria vijana ambao wamekuwa hawayumbishwi kwa nguvu ya fedha na muda wote amekuwa akisimamia maadili ya kazi yake.

Taarifa ya Ikulu iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Peter Ilomo jana, ilieleza kuwa Rais Jakaya Kikwete, amemteua Biswalo Mganga kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) uteuzi ambao ulianza Ijumaa iliyopita.

Kabla ya uteuzi huo, Mganga alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na Wakili wa Serikali Mfawidhi.

Awali nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Dk. Feleshi, ambaye aliteuliwa hivi karibuni kuwa jaji wa Mahakama Kuu.

Uteuzi wa Dk. Feleshi kushika wadhifa huo mpya ulianza rasmi Agosti 13 mwaka huu na aliapishwa Agosti 15 mwaka huu.

CHANZO: Mtanzania

tema mate feleshi alisema haya haya
 
Back
Top Bottom