PISTO LERO
JF-Expert Member
- Mar 8, 2011
- 2,819
- 1,458
MWENDESHA Mashitaka Mkuu wa Serikali (DPP), Eliezer Feleshi, alibadilisha mashitaka pamoja na washitakiwa katika kesi dhidi ya Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara, Idd Simba, hatua iliyosababisha Serikali kushindwa katika kesi hiyo, Raia Mwema limeambiwa.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ilikuwa imependekeza kwamba ili Simba na wenzake watiwe hatiani, ilipaswa ashitakiwe kwa makosa machache na pia Mkurugenzi wa Kampuni ya Kisena Group, Simon Kisena, atumiwe kama shahidi badala ya mshitakiwa.
Ile kesi ya Simba ilikuwa iko wazi kabisa. Ushahidi ulikuwa unajitosheleza na Serikali ingepata heshima kama haki ingetendeka. Tatizo ni kwamba ofisi ya DPP ilibadili mashitaka na washitakiwa, na hilo liliathiri kesi nzima, kilisema chanzo cha kuaminika cha gazeti hili ndani ya Takukuru.
Juni 19 mwaka huu, DPP alitoa hati ya kufuta kesi hiyo (Nole Prosequi) chini ya kifungu cha 91 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, akidai kuwa hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.
Awali, Simba na wenzake, aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Salim Mwakinginda na Meneja wa UDA, Victor Milanzi, walishitakiwa kwa makosa yanayofanana Aprili mwaka jana.
Walipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Aprili 29 mwaka jana, Simba na wenzake hao walishitakiwa kwa mashitaka manane ya kula njama, kughushi, kuchepusha fedha, matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia UDA hasara ya Sh. bilioni 2.4.
Hata hivyo, kesho yake, Aprili 30, mwaka jana, upande wa mashitaka ulifuta kesi hiyo na kuwafungulia kesi ya uhujumu wa uchumi ikiwa na makosa sita yakiwamo ya matumizi mabaya ya ofisi, rushwa na kulisababishia shirika hasara ya Sh. bilioni 8.4.
Katika kesi hiyo mpya, DPP aliamua kumuunganisha Kisena kwenye kesi hiyo kama mtuhumiwa wakati awali alitakiwa kutumika kama shahidi wa upande wa mashitaka.
Katika kesi za namna hii, kuna kitu kinaitwa tumia samaki mdogo ili ukamate samaki mkubwa. Hii maana yake ni kwamba, mkono wa sheria unakubali kumwachia aliyefanya kosa kidogo kwa lengo la kumkamata aliyefanya kosa kubwa.
Kwa kumpoteza Kisena kama shahidi, Serikali ilikuwa imejifunga bao la kisigino. Huyu ndiye angekuwa shahidi muhimu zaidi kwa Serikali lakini kwa maamuzi haya ya DPP, Serikali ikashindwa katika kesi hii muhimu, kilisema chanzo kimoja cha gazeti hili kutoka upande wa mashitaka.
Simba na Milanzi walikuwa wakidaiwa kuwa walipokea rushwa ya Sh. milioni 320 kutoka kwa Kisena ili auziwe hisa za UDA ambazo zilikuwa hazijagawiwa bado. Kosa hilo linadaiwa kutendeka kati ya Septemba mwaka 2009 na Januari mwaka 2010.
Ingawa TAKUKURU imethaminisha thamani ya UDA kwa gharama ya Sh. bilioni 22 kutokana na uchunguzi wake, Kisena aliuziwa UDA kwa kiasi cha zaidi kidogo ya Sh. bilioni moja.
Katika mahojiano yaliyofuata baada ya kuibuka kwa kashfa hiyo ya UDA, Simba alidai kwamba fedha anazodaiwa kupewa na Kisena zilitokana na malipo ya kazi za kitaalamu (consultancy fees) alizofanya na kampuni ya Simon Group ingawa Kisena mwenyewe aliwahi kunukuliwa akisema hajawahi kufanya kazi za kitaalamu na Simba.
Fedha hizo za ununuzi wa UDA ziliingizwa kwenye akaunti binafsi ya Simba na si ya shirika hilo kama ambavyo ilitarajiwa.
Ni kweli kwamba kuna uwezekano Kisena alitoa rushwa kwa akina Simba.
Lakini, kama wewe unataka kununua nyumba yangu na mimi ninakupa akaunti namba ya kulipia na ukatekeleza hilo, kuna kosa gani?
Inawezekana kabisa ya kuwa kwa kufanywa shahidi, Kisena asingeshitakiwa. Lakini ushahidi wake ungewatia hatiani watu wazito na wakubwa zaidi, na hili lingekuwa funzo tosha kwa watu wengine wenye mamlaka.
Kwa kumshitaki Kisena, fursa hii ilipotezwa, alisema mmoja wa wanasheria waliohusika kwa karibu katika kesi hiyo.
Alipoulizwa na Raia Mwema kueleza ukweli wa madai kwamba ofisi ya DPP ilibadili mashitaka dhidi yake, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dk. Edward Hosea, alisema kwa kadri ninavyofahamu, kesi hiyo inafanyiwa review (mapitio) kwa sasa. Sitapenda kuzungumza chochote kuhusu hilo.
Katika hatua nyingine, juhudi za kumpata DPP kuzungumzia suala hilo hadi tunakwenda mitambaoni hazikuzaa matunda, ingawa alimjibu mwandishi wetu kwa ujumbe mfupi wa simu ya mkononi kwamba apigiwe simu baadaye kwa sababu alikuwa mkutanani, lakini hata alipopigiwa simu Jumatatu wiki hii iliita bila majibu
- See more at: Raia Mwema - Hii ndiyo siri Idd Simba kufutiwa kesi