kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,931
- 7,828
Mwenye macho haambiwi ona, lakini akiona ajabu anaweza kuduwaa kimya mithili hajaona kitu. Kufutwa na DPP kesi iliyokua inamkabili Idi Simba Na wenzake kwa makosa ya uhujumu uchumi ni jambo lililowastaajabisha raia wengi.
Makosa yao ilikua ni pamoja na kuchakachua hisa za shirika la UDA kwa kuzionyesha zina thamani ndogo kuliko hali halisi na kuziuza kwa kampuni ya Simon group hisa hizo kwa bei sawa na bure. Kosa linginne ni kupokea fedha za mauzo ya kampuni hiyo na kuziweka kwenye akaunti zao binafsi.
Ushahidi wa CAG dhidi ya watuhumiwa ulikua barabara ndio maana kesi ikapandishwa daraja kua ya uhujumu uchumi. Wanaoelewa walianza kutilia shaka pale watuhumiwa walipokubaliwa dhamana kwani kesi ya uhujumu uchumi haina dhamana.
Baada ya kufutwa kesi hiyo yapo maswali yanahitaji majibu
1. Je uuzaji wa UDA sasa kisheria ikoje, ndio wizi huu wa mali ya umma umebarikiwa?
2. Hiyo fedha ya umma iliyowekwa mfukoni kwa watu binafsi ndio wizi huo umehalalishwa na DPP?
3. Je DPP kwa nini asiwajibishwe kwa kufuta kesi hiyo?
Hakuna shaka tena katika nchi hii ushirika wa chama tawala serikali na mafisadi ni imara sana. Tulisikia waziri mkuu hivi karibuni akimtaja Idi Simba bungeni kwa unyenyekevu 'Mzee wetu Idi Simba'
Jeuri ya mafisadi sasa iko wazi kutokana na mbinu ya hadaa sasa kugonga mwamba kwani wananchi wamefumbua macho. Sasa ufisadi umeanza kutumia ubabe kwa kuwashambulia raia kwa njia binafsi na kutumia polisi. Juzi waziri mkuu amewaeleleza polisi kuwapiga raia.
Bila shaka polisi watatumiwa kuwapiga wapinzani wa kisiasa kwa kisingizio cha kutotii amri. Msisahau Hoseah wa takukuru naye anamlalamikia DPP kwa kuwekea kifua kesi za mafisadi papa.
Wana jf nawasilisha.