DPP Feleshi unajua tabia za Wakili Kombe kule Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DPP Feleshi unajua tabia za Wakili Kombe kule Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nakandamiza Kibara, Dec 20, 2009.

 1. N

  Nakandamiza Kibara Senior Member

  #1
  Dec 20, 2009
  Joined: Jul 17, 2007
  Messages: 143
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sisi wakazi wa Arusha tumeona pa kukimbilia ni JF kwa kuwa si PCCB wala Ofisi ya DPP inaweza kutusikiliza kirahisi . Kwa kuwa tuna amini JF ni mrwisho wa maelezo leo tunaweka swali hili kwa DPP Feleshi .

  Baada ya Serikali kusema Polisi sasa basi kuwa waendesha mashitaka na ili kutoa haki zaidi kwa watanzania mawakili wa Serikali kwenye maeneo haya wamekuwa hatari kubwa na wa kutisha .Wanachukua rushwa kwa nguvu na leo nataka kukueleza kwamba Kombe ni hatari na anatishia Mahakama ya Arusha .Kombe ni gumzo yuko tayari kufuta kesi ama kusimamia kunyimwa dhamana kwa pesa ndogo tu . Ndugu Feleshi naamini wewe ndiye Muhusika funguka masikio nan mulika Arusha Kombe anatishia haki za watanzania mahakama ya Arusha . Ushahidi upo mwingi wa kumwaga tuta uweka hapa tena wiki hii inayo isha amechukua laki kadhaa kw akushirikiana na mwananchi mmoja kumpa mtu dhamana .Ameshiriki hata kumtumia hakimu mmoja rafiki kujipangia kesi ili wachukue laki kadhaa .Kesi iko mahakamani wengine wako magereza kwa kushindwa masharti magumu .
   
 2. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #2
  Dec 20, 2009
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  dah... kazi ipo kumbe huyu jamaa anatabia hii chafu.......
   
 3. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #3
  Dec 20, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mmh mi naogopa kujadili hili.Je unaushahidi wa kutosha?sio huo wa maneno
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Dec 20, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,546
  Likes Received: 18,204
  Trophy Points: 280
  Pole sana NK, hiyo ni keesi ya nyani unampelekea ngedere, ni mwendo wa kila mbuzi kwa usawa wa kamba yake, kama Hosea ndio bosi wa kuzuia rushwa huku ni mvutaji mzuri tuu, unategemea nini. Unadhani unamwambia kitu kipya Feleshi, mbona hakuna asichokijua!. Ukiondoa majaji, mahakimu ni mwendo wa usawa wa kamba zao na hakuna asiyejua.

  Japo pia naunga mkono, kupiga kelele, jamaa atapunguza kidogo speed.
   
 5. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Ndugu yangu,

  Je sheria inasemaje kuhusu dhamana inayotakiwa kwa mtu aliyefanya kosa kama la huyo ndugu/rafiki/jirani/.... yako?

  Cha maana ni kujua sheria inasemaje kuhusu hilo kosa. Kama wanaenda kinyume na hiyo sheria ndio uwasilishe malalamiko yako kwa judge, na wahusika wengine wa juu.

  Sidhani kama hawa ma-judge na mawakili wanatakiwa kuamka asubuhi na kusema leo kila kesi dhamana yake itakuwa kiasi fulani tofauti na sheria.

  Kama hivyo ndivyo alivyofanya, una haki ya kumpeleka ngazi za juu.
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Dec 20, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Tatu umekurupuka nadhani .
  Mleta mada kasema ndugu wa mtuhumiwa pamoja na kukidhi masharti ya dhamani yet wamelipa laki kadhaa na hizo zime enda kwa Kombe pesa hizi kachukua kaweka mfukoni mwake .
   
 7. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #7
  Dec 20, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Ila pccb wachunguze maana ukute kuna ukweli maana nchi na serikali imeharibika kabisa kwa rushwa...hasa arusha mwz jamani watu ni miungu watu haki za watu zinapotea bure....pccb wachunguze kama kuna ukweli waingilie kati....bado nina aimani na pccb hasa wilayani na mikoani ila sio makao makuu......
   
 8. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #8
  Dec 20, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  eh
  duh
  Feleshi chukua hatua kwa kuchunguza na maamuzi mazito
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Dec 20, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nakandamiza Kibara naona umepotea njia! Unapodai kuwa vyombo km PCCB vimeshindwa kwa hiyo umeleta malalamiko yako JF ili DPP Felesh apewe ujumbe! Kwani DPP anashughulikia nidhamu za mawakili au upelelezi? Na kama una ushahidi wa rushwa kwa nini upoteze muda wa kuwasiliana na DPP huku ukijua hahusiki na masuala ya kupeleleza rushwa au makosa ya jinai? Hata kama ukiwasiliana naye atalipeleka suala hilo PCCB kwanza kisha wakishalichunguza ndio watampelekea yeye ili afikishe kesi mahakamani! Kumbuka DPP si mpelelezi, yeye anapokea majalada yaliyopelelezwa tayari! Kwa hiyo kama hujui uliza badala ya kutema upupu wa kuwapotosha watu makusudi! Otherwise ukikaa na ushahidi wako au kuuanika hapa JF utakuwa hujasaidia kitu na utaonekana kuwa wewe ni sehemu ya tatizo la rushwa!
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  Dec 21, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Mzee umeshusha maneno ya bure . Hawa jamaa wako chini ya Feleshi nma ni sahihi Feleshi kupewa taarifa na hata kuchunguza pia anaweza kabla ya hao PCCB
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  Dec 21, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 21,997
  Trophy Points: 280
  JAMII FORUMS TETEa wanyonge
   
Loading...