DOWANS itasababisha Baraza la Mawaziri kuvunjwa?

DOWANS itasababisha Baraza la Mawaziri kuvunjwa?

Unajua dawa mbona imeshaiva, swala hatuzungumzii tena kuhusu kutaka na kutokutana, kama wao wameua rais wasio na hatia, sisi tunangoja nini kutengeneza majeneza ya wezi hao wanaolelewa kama watoto wachanga. Huko ndiko walikotufikisha, kata kata kata kata, kata kila kitu kata
 
aah wapi.. kwa kadiri ya kwamba wakuu wa nchi nchi hii wana maslahi na Dowans, hawajibishwi mtu. NOPE

kwa mwenendo ulivyo na mwamko wa watanzania, Serikali ikilipa nadhani nchi inaweza kupasuka. Ni kweli uongozi uliopo unaweza kushindwa kuwawajibisha watu, lakini ni vyema viongozi wetu wajue kwamba haitakuwa rahisi kubaki na tanzania hii tunayoifahamu baada ya kutoa malipo tata.
 
Wanaotajwa kumiliki Dowans ni usanii mtupu


lC.gif
Lula wa Ndali-Mwananzela​

Januari 12, 2011
Raia Mwema

bul2.gif
Kwa nini Karamagi alishinikiza TANESCO iingie mkataba na Dowans?

LILIKUWA ni shinikizo la aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wa wakati ule Bw. Nazir Karamagi lililosababisha TANESCO kukubali kuhamisha mkataba wake na Richmond kwenda Dowans Holdings SA.

Bw. Nazir Karamagi alikuwa ana uhusiano wa kibiashara na kampuni ya Portek Systems and Instruments ya Singapore ambayo ilishiriki kuleta mawinchi kwa ajili ya kampuni ya TICTS ambayo wakati ule Bw. Karamagi alikuwa ni mbia mkuu.
Ni kampuni hiyo Portek Systems and Instruments inayotajwa katika nyaraka za BRELA kuwa na asilimia 39 ya hisa kwenye kampuni ya Dowans Tanzania Limited. Bila uchunguzi huru haijulikani ni kwa nini Bw. Karamagi alishinikiza Shirika la Umeme la Tanzania ((TANESCO) kubadili mkataba wake na kuupeleka kwa Dowans Holdings ya Costa Rica.
Kuhusika kwa Karamagi kunatajwa mara ya kwanza kwa kina kwenye ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe. Sehemu ya ripoti hiyo ilijaribu kuelezea kuhusishwa kwa Wizara ya Nishati na Madini katika kuingilia watendaji wa TANESCO.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wakati TANESCO wamewaandikia kampuni ya Richmond kutaka maelezo juu ya ucheleweshaji wa kuingiza majenereta na uhalali wa kampuni hiyo huko Marekani au uwezo wake wa kifedha, ilikuwa ni Wizara ndiyo iliyoingilia kati kuikingia kifua kampuni hiyo ya Richmond.
TANESCO wakaamua kuiandikia kampuni ya Richmond taarifa ya tahadhari (default notice) kuwa inaonekana walikuwa wanaelekea kushindwa kutekeleza mkataba. Ripoti hiyo inaongeza na kusema kuwa: "Wizara ya Nishati na Madini haikufurahishwa na mwelekeo huo wa TANESCO wa kuvunja Mkataba huo licha ya kwamba hali ya maji nchini ilizidi kuwa nzuri na kampuni hiyo ya Marekani ilikuwa haionyeshi dalili ya kuweza kutekeleza mradi huo kinyume na makubaliano."
Alikuwa ni Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Karamagi akipitia Kamishna wa Nishati Bw. Bashir Mrindoko, aliyetaka maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa TANESCO ya kwa nini shirika hilo liliandika taarifa hiyo ya tahadhari kana kwamba kuashiria kuelekea kuvunjwa mkataba.

Ripoti inasema: "Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO akajieleza kwa barua aliyomwandikia Waziri moja kwa moja yenye Kumb. Na. MD/ 003 ya tarehe 23 Novemba, 2006" . Ilikuwa ni siku tano baada ya barua hii, kwa mujibu wa Ripoti ya Mwakyembe, Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Balozi Fulgence Kazaura alimwandikia barua Mkurugenzi wa TANESCO na kumueleza kuwa amepokea mawasiliano ya simu toka kwa Waziri Karamagi akiwa nchini Canada "akimuarifu kwamba Richmond Development Company LLC walikuwa wanataka kuhamisha majukumu yao yaliyobaki katika mkataba wa uletaji mitambo na uzalishaji umeme wa dharura kwa kampuni nyingine."

Jambo hili ni muhimu kulizingatia kidogo. Wawili waliotajwa na Waziri Ngeleja, hivi karibuni, kuwa ni sehemu ya wakurugenzi wa kampuni ya Dowans Tanzania Limited ni Wacanada. Hawa ni Bw. Guy Arthur Picard na Bw. Andrew Jamess Tice. Hilo peke yake haliwezi kutushtua sana isipokuwa wasifu wa mmoja wao unatufanya tudadisi kidogo.

Bw. Andrew James Tice anatajwa kuwa ni mtaalamu wa mambo ya kibenki. Wasifu wake ulioko kwenye mitandao mbalimbali unatudokeza juu ya utaalamu wake uliobobea katika kulinda maslahi ya wateja wake ambao wanaaminisha fedha na majina yao kwake.

Kwa maelezo yake mwenyewe amefanya kazi hii ijulikanayo kama fiduciary kwa wateja wake wa Mashariki ya Kati na Afrika huku akiwakilisha maslahi yao katika nchi za Mauritius, Guernsey, Singapore na Cayman. Nchi zote hizo pamoja na Costa Rica ni miongoni mwa nchi ambazo zina usiri sana katika masuala ya makampuni.

Kutokana na nafasi yake hiyo, Bw. Tice ni mtaalamu anayejua jinsi ya kufungua makampuni hewa au yale ya kificho ambayo wamiliki wake halisi hawataki kujulikana. Hii ni sehemu ya kazi yake.

Ndipo hapa suala la Karamagi kuwepo Canada na kutoa maelekezo kwa TANESCO kuwa mkataba wa Richmond upelekwe kwa kampuni nyingine linapoonekana kwa mwanga zaidi. Je yawezekana kuwa ni wakati ule ndipo Bw. Karamagi alipewa taarifa na "vigogo" wahusika waliotaka huduma ya Bw. Tice kuwafungulia kampuni huko Costa Rica ambayo itarithi mkataba wa Richmond?

Naomba nipendekeze kuwa hivyo ndivyo ilivyo kwani msisitizo uliofuatia hapo hauwezi kuelezewa isipokuwa kulikuwa na nguvu kubwa nyuma ya Karamagi iliyotaka kampuni pekee ambayo ingerithi mkataba huo iwe ni Dowans.

Kitu cha kwanza ambacho ripoti ya Mwakyembe inasema Bw. Karamagi alifanya ni kuhoji (ninaamini alikuwa anajua) kama mkataba wa Richmond/TANESCO "unaruhusu" kukabidhi majukumu kampuni nyingine.

Jibu la Mkurugenzi wa TANESCO kama inavyoelezwa na Kamati hiyo kwenye ripoti ni kuwa "uongozi wa TANESCO ulimshauri Mwenyekiti wa Bodi amtaarifu Mhe. Waziri kwamba Kifungu cha 15.12 cha mkataba huo hakiruhusu kukabidhi majukumu ya mkataba kwa kampuni nyingine isipokuwa kwa maafikiano ya pande mbili za mkataba".

Pamoja na ukweli huo, Richmond wakaiandikia TANESCO barua tarehe 4 Disemba, 2006. Ikapokea barua kutoka kwa Richmond Development Company LLC ikielezea makusudio ya Richmond kuhamisha majukumu yake yote ndani ya mkataba huo kwenda kwa Dowans Holdings, S.A"

TANESCO, katika ujasiri wa kupingana na Wizara yake mama, ikaandika barua siku hiyo hiyo kupinga mpango huo. Ripoti ya Mwakyembe inatudokeza kuwa TANESCO walitoa sababu tatu za kwa nini jambo hilo haliwezekani. Sababu hizo ni kuwa "(i) Kifungu 15.12 cha mkataba kinataka kuwepo kwa makubaliano ya pamoja ya kimaandishi (written mutual agreement) kutoka kwa wahusika wote wa mkataba (parties) kabla ya kufikiwa uamuzi wa kuhamisha mkataba. (ii) Richmond Development Company LLC haijatoa sababu zozote za msingi kwa pendekezo hilo la kuhamisha Mkataba. (iii) TANESCO haifahamu historia, uzoefu wala uwezo wa kifedha wa hao wanaopendekezwa kuhamishiwa mkataba."

Lakini wizara haikujali hoja za TANESCO na badala yake tarehe 21 Disemba 2006 ikaandika barua kuilazimisha TANESCO kuhamisha mkataba huo kwenda Dowans wakati dharura yenyewe ilishakwisha.
Dk. Mwakyembe alitutaarifu kuwa: "Uamuzi huo wa kuruhusu uhaulishwaji wa mkataba kipindi ambacho nchi ilikuwa imeondokana na hali ya dharura, tena kwa masharti yaleyale ya kulaliwa yanayoweza kukubalika pale tu ambapo nchi imebanwa kweli kweli na tatizo, ulimfedhehesha hata Mkurugenzi Mwendeshaji wa Dowans Holdings S.A, Bw. Guy Piccard, raia wa Canada, alipohojiwa na Kamati Teule tarehe 27 Disemba, 2007."

Kwa maneno mengine, maelezo kuwa TANESCO ndiyo italipa gharama ya kesi iliyopoteza kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Biashara inashangaza sana. TANESCO walikataa kuhamisha mkataba, na walitoa sababu ambazo hazikujibiwa.

Kwamba Serikali ya Tanzania, kupitia Wizara ya Nishati na Madini chini ya Karamagi, ndio waliilazimisha TANESCO kuhamisha mkataba kwenda Dowans badala ya kuuvunja kama walivyotaka na wao ndio walipe bilioni 94, ni jambo linalotakiwa kumuudhi na kumkera kila Mtanzania.

Hasara hii ambayo ukijumlisha na fedha nyingine ambazo zimeshalipwa kwenye suala hili hadi sasa ambayo zinakaribia zaidi ya bilioni 50 (nina uhakika Ngeleja na wenzake wanataka tuamini kuwa bilioni 94 ndio malipo pekee), ni lazima iende na vichwa vya watu!

Vyama vya siasa vikatae, kina mama wakatae malipo haya haramu, na vijana wa Tanzania wayakatae. Viongozi wa dini watoe tamko na kukataa malipo haya ya kidhalimu; kwani kuyaendekeza ni kuendekeza kunyonywa na kutawaliwa kimabavu.

Lakini vile vile kuna watu wanatakiwa watoe maelezo kwa taifa miongoni mwao ni Bw. Nazir Karamagi na kundi zima la wanasiasa waliohusika na kuliiingiza taifa katika aibu hii. Na binafsi ninaamini Rais Kikwete mwenyewe ni lazima atoe msimamo kwani toka mwanzo alikuwa anajua kilichokuwa kinafanywa na marafiki zake wa karibu.

Kwa nini ameridhia serikali ibebeshwe mzigo huu? Kwa nini Watanzania walipe gharama ya uzembe wa viongozi ambao yeye amewateua? Rais Kikwete ana uwezo ndani yake wa kuliepusha taifa na aibu hii. Akitaka.
hs3.gif
​
 
Kumbe kikwete amerogwa maskini, amegeuzwa mjingamjinga, hasemi kitu, yaaani yuko kimya badala ya kutoa msimamo na kukemea yanayotokea, Sheikh yahya kamuongezea majini karibia 20 kichwani yaani anakuwa kama amevuta weed. We nchi gani kila mtu afanye na kusema anavyotaka hata aiingize nchi kwenye hasara, we unachekacheak haaaaaaaaaaaaa. Nahisi kutapika
 
MSIBA WA MASHUJAA: CHADEMA wailiza Arusha
• Mbowe atoa tamko zito, ahamasisha maandamano nchi nzima

na Waandishi wetu


amka2.gif
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), jana kililiteka tena Jiji la Arusha katika ibada, maandamano na mazishi ya mashujaa wake, ambayo yalifanyika kwa amani bila ulinzi wowote wa polisi.
Polisi pekee waliooekana ni wale tu wa usalama barabarani. Barabara kadhaa za jiji la Arusha zilifungwa, na maelfu ya wananchi walitanda kando ya barabara hizo, kushuhudia msafara wa miili ya marehemu ikitoka chumba cha maiti kuelekea viwanja vya NMC, na baadaye kuelekea eneo la mazishi, USA River alikozikwa Ismaili Omar. Mmoja wa marehemu hao, Denis Michael, atazikwa leo Rombo, mkoani Kilimanjaro.
Mashujaa hao waliuawa na polisi waliokuwa wanapambana na wafuasi na viongozi wa CHADEMA katika kuzuia maandamano na mkutano wa hadhara uliopangwa kufanyika viwanja vya NMC, Januari 5, mwaka huu, kudai marudio ya uchaguzi wa meya wa Jiji la Arusha na naibu wake.
Zizi la Arusha lilizizima kwa maelfu ya wananchi waliojitokeza kwa kishindo katika ibada maalum ya kuaga miili ya marehemu hao.
Katika ibada hiyo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alitoa tamko zito lililolaani vikali mauaji hayo, huku akitangaza maandamano mapya yatakayofanywa na chama hicho nchi nzima yakibeba madai kuu nane likiwamo la kutaka kuitishwe mkutano wa kitaifa utakaofanikisha kuandikwa kwa katiba mpya.
Katika madai hayo, Mbowe alitangaza msimamo mkali wa kutaka mashitaka yote yaliyofunguliwa dhidi ya viongozi wa ngazi zote wa chama hicho - wanachama, wafuasi na wananchi wengine wote waliokumbwa na kumba kumba ya Jeshi la Polisi - yafutwe bila masharti yoyote, vinginevyo hawatahudhuria mahakamani tena, hata kama kwa kufanya hivyo kutafanya wakamatwe na kurudishwa tena gerezani.
"Tunasisitiza katika jambo hili kwamba viongozi, wanachama na wafuasi wetu wote waliokamatwa na kufunguliwa mashtaka haya hawatahudhuria mahakamani tena kuhusiana na kesi iliyofunguliwa dhidi yao, hata kama kwa kufanya hivyo kutafanya wakamatwe na kurudishwa tena gerezani," alisema Mbowe.
Alitaka kuundwe tume huru ya uchunguzi ya kimahakama (Judicial Commission of Inquiry) itakayoongozwa na majaji wa Mahakama ya Rufani ili ifanye uchunguzi huru, wa kina na wa wazi wa matukio yote yaliyosababisha IGP Mwema kupiga marufuku maandamano ya amani na mkutano wa hadhara kabla ya Jeshi la Polisi kufanya vurugu zilizosababisha mauaji ya wananchi wasiokuwa na hatia.
Dai lingine ni kutaka Waziri wa Mambo ya Nchi Shamsa Vuai Nahodha na Inspekta Jenerali wa Polisi Saidi Mwema wawajibike wajiuzulu. nia.
"Kujiuzulu kwao kutapisha uchunguzi huru na wa kina wa matukio yote yaliyosababisha wananchi wetu kuuawa, mamia kujeruhiwa na mamia mengine kukamatwa bila sababu yoyote na kuwekwa rumande na baadaye kufunguliwa mashtaka ya uongo ya jinai," alifafanua na kuongeza:
"IGP Mwema, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha Andengenye na wale wote walioamuru au kutekeleza amri ya kuvunja maandamano na mkutano halali wafunguliwe mashtaka ya jinai kwa matumizi mabaya ya madaraka na kwa kusababisha mauaji ya wananchi wasiokuwa na hatia."

Mbowe, ambaye pia ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, aliitaka serikali kuwalipa fidia stahili kwa mujibu wa sheria husika za nchi ndugu na jamaa wa wale wote waliouawa kutokana na vitendo vya polisi na wale wote walioumizwa kwa namna yoyote ile na au kuharibiwa mali zao kutokana na vitendo hivyo.
Pia alisema chama hicho kinataka matokeo ya uchaguzi wa viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha yafutiliwe mbali, na uchaguzi mpya uitishwe haraka iwezekanavyo, kwani uchaguzi huo ndio chanzo cha mauaji ya wananchi.
"Sheria ziweke wazi wajibu wa Jeshi la Polisi la Tanzania kulinda maandamano ya amani na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na/au ya wananchi," alisema.
Katika kuhakikisha kwamba madai ya chama hicho yanatekelezwa, alisema chama kimeelekeza viongozi, wanachama na wafuasi wake mikoani na wilayani kuandaa maandamano ya amani nchi nzima ili kulaani mauaji ya wananchi wa Arusha na kudai utekelezaji wa madai hayo.
"CHADEMA Makao Makuu itatuma maafisa wa ngazi za juu wa chama, wakiwemo wabunge na wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA kushiriki katika maandamano hayo kwa ngazi za mikoa na wilaya ili kuyaongezea nguvu na hamasa," alisisitiza Mbowe.
Alimhusisha pia Rais Kikwete, serikali yake na chama chake, akisema waliandaa mazingira ya damu iliyomwagwa Arusha, kwani kwa mujibu wa Katiba, yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama, na pia ndiye aliyewateua IGP Mwema na waziri Nahodha waliosababisha mauaji hayo. Alisema Rais Kikwete pia alitoa kauli tete katika hotuba yake ya kufunga mwaka 2010, ambayo ilihamasisha polisi kujipendekeza kwa CCM kwa kuzuia kazi za kisiasa za CHADEMA.
Katika ibada hiyo, maaskofu wa madhehebu ya Kikristu mkoani Arusha walimkemea Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba, kwa kuitumia Biblia takatifu kuhalalisha uovu; wakamtaka aache tabia hiyo mara moja.
Huku wakimlinganisha na viongozi mbalimbali wanaotajwa kwenye Biblia waliokuwa wakifanya hivyo kulinda uovu wao, maaskofu hao wakiongozwa na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Thomas Laizer, aliyezungumza kwa niaba wenzake, walisisitiza kwamba wataendelea "kuikosoa serikali na chama chochote kile pindi kinapokosea."
Kauli ya Makamba iliyowakera maaskofu hao, na ambayo amekuwa akiirudia mara kwa mara, ni ile aliyotumia kuwakejeli kwa kunukuu maandiko matakatifu ya Kurani na Biblia akisema "tiini mamlaka iliyo kuu." Walisema ufahamu wa Makamba ni finyu katika kutafsiri maana halisi ya neno hilo.
Askofu huyo alisema kazi ya viongozi wa dini ni kukosoa maovu kwenye jamii. Alisema wataendelea kufanya hivyo kila inapowabidi bila kujali ni nani au chama gani kimekosea, kwani kazi ya manabii tangu enzi za Biblia ilikuwa pia kuiongoza jamii katika njia nyoofu.
"Kama serikali wameamua kutuvunjia heshima, basi wasimame kwenye majukwaaa kutetea uovu wao, na sisi tutasimama kwa ajili ya kupinga uovu wao, tuone Mungu atamsikia nani. Sisi tunataka uchaguzi wa meya na naibu wake urudiwe, apatikane kiongozi halali bila kuangalia atachaguliwa kutoka chama gani, " alisema Askofu Laizer.
Kiongozi huyo wa kiroho alielezea kukubaliana na kauli za viongozi mbalimbali zilizotolewa kwa ajili ya kulipatia ufumbuzi suala hilo, huku akipingana na ile ya Makamba na Katibu wa CCM mkoa wa Arusha, Mary Chatanda wanaosisitiza kuwa meya wa jiji hilo alipatikana kihalali na kwa kufuata sheria, na kwamba suala hilo likapingwe mahakamani.
Alisema tabia ya Makamba kurudia lugha hizo mara kwa mara imemuambukiza kwa Chatanda ambaye aliwakejeli maaskofu akitaja wavue majoho na wamfuate kupambana katika uwanja wa siasa, hali ambayo amesema ni kuwakosea nidhamu.
''Maaskofu wamesikitishwa na kauli yake na pia kauli ya Katibu wa CCM mkoa wa Arusha, Mary Chatanda kuwataka kuvua majoho na kuingia katika siasa kwani ni kuwavunjia heshima,'' alisema askofu Laizer.
Katika ibada hiyo, Sheikh Alawi, akisoma dua, alitangaza rasmi kuwa marehemu hao Omar Ismail na Denis Shirima wamefariki kishujaa.
Mbali na Mbowe, mazishi hayo yalihudhuriwa pia na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, muasisi wa chama hicho, Edwin Mtei, na wabunge zaidi ya 18, wakiwamo, Godbless Lema John Mnyika (Ubungo), Halima Mdee (Kawe), Joyce Mukya (Viti Maalumu), Mustafa Akoonay (Mbulu), Philemon Ndesamburo (Moshi Mjini), Lucy Owenya (Viti Maalumu), Susan Kiwanga (Viti Maalumu), Anna Komu (Viti Maalumu), Tundu Lissu (Singida Kaskazini), Susan Lyimo (Viti Maalumu), Pauline Gekul (Viti Maalumu).
Nayo mashirika 50 yanayotetea Usawa wa Kijinsia, Haki za Binadamu, Maendeleo na Ukombozi wa Wanawake Kimapinduzi (FemAct), yamelaani ukiukwaji wa haki za binadamu, demokrasia na uvunjivu wa amani uliosababisha kuumizwa na mauaji ya raia wasiokuwa na hatia mjini Arusha.
Katika taarifa iliyotolewa jana kusainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Usu Mallya, wanaharakati kutoka mashirika hayo walisema:
"Vurugu hizo ziliendana na unyanyasaji na udhalilishaji wa kijinsia kwa baadhi ya waandamanaji, huu ni ukiukwaji wa haki za msingi za kibinadamu na za wanawake…

"FemAct inalaani kitendo cha halmashauri ya Jiji la Arusha kusimamia na kuendesha uchaguzi batili usiozingatia sheria kanuni na taratibu za uchaguzi ambao ulimpata Meya na Naibu wake 18/12/,2010 na kumpelekea kutokea kwa vurugu hizo.
"FemAct tunalaani kwa nguvu zetu zote ubabe na matumizi mabaya ya vyombo vya dola, hasa Jeshi la Polisi ambacho ni chombo cha ulinzi na usalama wa wananchi kugeuka na kuvunja sheria ya kuwazuia wananchi kutoa sauti zao na kupigania haki zao za msingi…
"Sisi wanaharakati tunalitaka jeshi la Polisi na serikali kuweka wazi muktadha na hali halisi ya tukio la Arusha, kuwataja na kuwachukulia hatua za kisheria walioshiriki kuvunja sheria na kutoa idadi kamili ya wananchi waliojeruhiwa na kupoteza maisha katika tukio hilo."
Waliitaka serikali kuunda tume huru itakayowashirikisha wananchi, plisi, vyama vya siasa, wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu kushughulikia suala hili na kuwahakikishia wananchi wa Arusha kuwa tukio kama hili halitatokea tena.
"Tunaitaka serikali,vyama vya siasa na vyombo vya dola kutokuwanyamazisha wananchi, viongozi wa kijamii na dini wanaolizungumzia suala la Arusha kwani hivyo ni kinyume na demokrasia iliyoendelea na kukomaa nchini."
 
kwa hiyo ina maana sita anapambana na bosi wake lakini anajidai anapambana ra
na pinda nae inaonekana kashaambiwa atapelekwa kubadilisha damu mpaka mauti yake akitetea dowans

Mkuu tazafali, kwani ze PM ana umem.....wa tanesco? au sijaelewa vizuri hapo kwenye redi?
 
Back
Top Bottom