DOWANS itasababisha Baraza la Mawaziri kuvunjwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DOWANS itasababisha Baraza la Mawaziri kuvunjwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 12, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,669
  Trophy Points: 280
  DOWANS kuvunja Baraza la Mawaziri
  • LHCR wamuunga mkono Sitta, Wafungua kesi kuipinga Dowans

  na Nasra Abdallah na Betty Kangonga


  [​IMG]
  SAKATA la malipo ya fidia kwa Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans Tanzania Ltd limechukua sura mpya baada ya kuwapo mpasuko mkubwa ndani ya serikali unaotishia kumeguka au kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri la Rais Jakaya Kikwete, Tanzania Daima Jumatano limebaini.

  Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa siku kadhaa sasa, umebaini kuwa tangu serikali ilipoamriwa kuilipa Dowans sh bilioni 185, kumekuwa na mzozo mkali wa wazi na wa chinichini miongoni mwa mawaziri, baadhi wakiapa kwamba wako tayari kujiuzulu kuliko kuona fedha hizo zikilipwa.

  Kundi la mawaziri wanaopinga kulipwa kwa fedha hizo, linaongozwa na Spika wa zamani wa Bunge, Samuel Sitta, ambaye kwa sasa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC).

  Kwa upande wa pili, kundi la mawaziri walioridhia malipo ya fedha hizo linawajumuisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, ambao kwa nyakati tofauti wamepata kunukuliwa wakisema taifa halina njia ya kukwepa faini hiyo.

  Taarifa kutoka serikalini zinaeleza kuwa kundi la mawaziri wanaokubaliana na maamuzi ya ICC limekumbwa na mgawanyiko mkubwa miongoni mwao kuhusu hatua anazopaswa kuchukuliwa Sitta.

  Baadhi ya watu walio ndani ya serikali waliozungumza na Tanzania Daima Jumatano wanasema wako wale wanaotaka kuona Waziri Sitta akipuuzwa huku wengine wakimtaka Rais Jakaya Kikwete amfukuze kazi kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kukiuka kwake misingi ya uwajibikaji wa pamoja.

  Habari nyingine ambazo gazeti hili halijazithibitisha zinaeleza kuwa wako baadhi ya mawaziri ambao wamefikia hatua ya kutafakari uamuzi wa kuendelea kubakia ndani ya Baraza la Mawaziri iwapo suala hilo litashughulikiwa isivyo.

  Tangu Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC Court), ilipotoa hukumu yake Novemba 15 dhidi ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO), kutaka ilipe fidia ya sh bilioni 94, Sitta amekuwa waziri wa kwanza kupinga hadharani hukumu hiyo akiitaka serikali isilipe.

  Kundi la mawaziri linalounga mkono msimamo wa Sitta, linadaiwa kufanya vikao vya faradha katika siku za hivi karibuni kupanga mkakati wa kupinga ulipaji wa fedha hizo na msimamo wao wanatarajia kuuweka hadharani katika kikao cha Baraza la Mawaziri, kinachotarajiwa kufanyika wakati wowote mwezi huu, chini ya uenyekiti wa Rais Kikwete.

  Duru zaidi za siasa zinasema kuwa nje ya Baraza la Mawaziri suala la malipo ya Dowans, linatarajiwa kulitikisa tena Bunge, kupitia hoja binafsi ya Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), na mjadala huo unaweza kusababisha baadhi ya mawaziri kuachia ngazi.

  Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano, Sitta alisema anashangazwa na hatua ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kutangaza msimamo wa serikali kuilipa Dowans bila suala hilo kujadiliwa na kupitishwa na Baraza la Mawaziri.

  “Nimekuwa wa kwanza kupinga serikali kulipa fedha hizi na anaendelea kusisitiza hatuna sababu ya kuzilipa, bado tuna nafasi kisheria ya kupinga, lakini kibaya zaidi nashangaa kusikia Waziri wa Nishati na Madini, ameutangazia umma kwamba serikali inajiandaa kuilipa Dowans. Uamuzi huo umepitia Baraza gani la Mawaziri,” alihoji Sitta.

  Alisema fedha hizo ni nyingi kuilipa Dowans ambayo alisema ina mkono wa mafisadi watatu, wanaotaka kuzitumia fedha hizo kwa maslahi yao kisiasa.
  Wiki iliyopita, Ngeleja alikaririwa akisema, Serikali imekubali kuilipa Dowans dola za Marekani za Kimarekani milioni 65, sawa na sh bilioni 94.

  Alisema sh 185 bilioni zilizokuwa zikitajwa kwenye vyombo vya habari ndizo ambazo kampuni ya Dowans iliiomba ICC ilipwe fidia kwa TANESCO kwa kukatiza mkataba walioingia wa kufua umeme, lakini mahakama iliafiki ilipe dola 65 milioni za Marekani.

  Alisema fedha hizo zitalipwa baada ya pande husika kusajili uamuzi huo katika Mahakama Kuu.
  “Serikali (hii serikali ni akina nani walioamua hivi?)tumekwishaamua kuwa tutailipa Dowans dola za Marekani 65 milioni, kama ilivyoamuliwa na ICC ambazo ni sawa na sh 94 bilioni, kuchelewa kuwalipa kutatufanya tulipe riba ya asilimia 7.5,” alinukuliwa akisema.

  Katika mkutano huo, Ngeleja pia aliwataja wamiliki wa Dowans Tanzania Ltd na hisa wanazomiliki katika mabano kuwa ni Dowans Holding S.A ya Costa Rica (81) na Portek.
  Huku akirejea barua ya Wakala wa Usajili wa Kampuni (Brella), aliwataja wakurugenzi na nchi wanazotoka kuwa ni Andrew James Tice (Canada) na Gopalakrishnan Balachandaran (India).
  Wengine ni Hon Sung Woo (Singapore), Guy Picard (Canada), Sulaiman Al Adawi (Oman) na Stanley Munai (Kenya).

  Wakati Ngeleja akitamka kwamba serikali inajiandaa na kulipa fidia hiyo haraka, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo, ameibua utata mwingine baada ya kuutangazia umma kwamba wizara yake haina fedha na haina mpango wa kutenga fedha katika bajeti ijayo kwa ajili ya kuilipa Dowans.

  Mkullo alisema TANESCO kupitia wizara yake ya Nishati na Madini, inatakiwa ijipange kusaka fedha za kuilipa Dowans na kamwe fedha hizo hazitatoka Hazina.

  Kiini cha sakata hilo kilianza mwaka 2006, wakati TANESCO ilipoingia mkataba wa mauziano ya umeme wa TANESCO na kampuni ya Richmond Development LLC.

  Miezi sita baadaye mkataba huo ulihamishiwa kwa kampuni ya Dowans Holdings ya nchini Costa Rica na baadaye kwa Dowans Tanzania Ltd.

  Wakati wa utekelezaji wa mkataba huo, ilizuka hoja kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo wabunge kwamba mkataba baina ya TANESCO na Richmond haukuwa halali kisheria hivyo usingeweza kurithiwa na Dowans.

  Suala hilo lilizua mjadala mkubwa hali ambayo TANESCO kwa kuwatumia mawakili wa kampuni ya Rex Attorneys ya jijini Dar es Salaam walivunja mkataba huo.
  Baada ya kuvunjwa kwa mkataba huo, ndipo kampuni hiyo ikalipeleka suala hilo ICC kama walivyokubaliana na TANESCO kwenye mkataba.

  Uamuzi huo wa ICC ulizua mjadala katika siku za hivi karibuni baada ya viongozi wa serikali kutofautiana kuhusu kuilipa kampuni hiyo au kutoilipa.

  Katika hatua nyingine, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHCR), kinatarajia kufungua kesi Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa serikali kukubali kuilipa Dowans.

  LHCR, pia inapinga kusajiliwa kwa tuzo hiyo Mahakama Kuu kwa sababu mikataba ya awali ilipatikana kwa rushwa na kukiuka maslahi ya umma.

  Mkurugenzi wa kituo hicho, Fransis Kiwanga, alisema walitarajia kufungua kesi hiyo jana na itasimamiwa na Kampuni ya Uwakili ya The South Law Chembers Advocates.
  Sambamba na hilo pia kituo hicho kimeitaka TANESCO kutokubali kuilipa Dowans hata senti moja kwa kuwa haikuridhia kurithishwa na kuhamishwa kwa mkataba wa Richmond kwenda Dowans.

  Aidha ameitaka Wizara ya Nishati na Madini kuacha mara moja kuwabebesha Watanzania mzigo wa kulipia gharama zinazotokana na uzembe, ubadhirifu na ufisadi wake yenyewe huku ikiingilia uhuru na utendaji wa Tenesco kwa kuitaka iilipe Dowans.

  “Kwa taifa maskini kama letu lenye matatizo mengi kama ukosefu wa umeme, mfumko wa bei na mengineyo, kutumia hela nyingi hivyo kulipa kampuni ambayo iligundulika kwa uchunguzi sahihi kuwa ni hewa, inatia shaka kwenye umakini wa serikali,” alisema.

  Mkurugenzi huyo alisema katika suala la Dowans kuna mambo ya kujiuliza ikiwemo kama Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lilithibitisha kama Richmond ni kampuni hewa, inawezekanaje kuwa na mkataba wa kurithisha mali zake kwa Dowans kwani uhalali wa kisheria wa milki ya Dowans kwa mali ya Richmond, haupo na kuhoji kwa nini serikali haikutaifisha mali za Ricmond tangu awali.
  Maswali mengini ni ikiwa Dowans haikurithi kwa uhalali mali ya Richmond, inawezaje Dowans kuwa na madai halali dhidi ya serikali kuhusiana na mali iliyopatikana kwa uhalifu.

  Hali kadhalika serikali kuharakisha kuilipa Dowans kuhusiana na mali iliyopatikana kwa uhalifu, je nini hasa maslahi ya Wizara ya Nishati na Madini na kuhoji wizara hiyo inamuwakilisha nani katika suala la Dowans.

  Hata hivyo wanaharakati hao walionyesha wasiwasi wao kwa serikali inaposema kuwa inalazimika kuilipa Dowans huku wakihoji kama imefuata taratibu za kisheria na kama shauri hili lilipowasilishwa katika mahakama ya ICC, wananchi walijulishwa kuhusu shauri hilo.

  Kwa mujibu wa Kiwanga sababu za kuliendesha shauri hilo kwa siri na kutohudhuria mahakamani kwa mawakili wa serikali, zinatia dosari mwenendo mzima wa suala hili ukizingatia kuwa limegubikwa na ufisadi tangu awali.

  Alitoa wito kwa wananchi wote kujitokeza kupinga hukumu hiyo ya kimataifa na nyingine kama hizo pamoja na maamuzi yoyote ya serikali yasiyokuwa na maslahi kwao zisitekelezwe. Naye Mkurugenzi wa Tamwa, Annelia Nkya, alivitaka vyombo vya habari kuendelea kupigia kelele sakata hili hadi kuona fedha hizo hazilipwi kwa Dowans.
   
 2. n

  niweze JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama Kweli Sitta Anaweza Kumobilize Opposition Ndani ya CCM, Wananchi Tutamsifu Sana na Kukweza Kama Shujaa. Dowans Mpaka Sasa Hivi Inaweza Kusimamishwa na Mawaziri na Watu Ndani ya CCM. Kama Itashindikana Ndani ya CCM, Wananchi Tukifahamu Wameshindwa Tutafute Migomo Nchini Nzima na Maandamano Ambayo JK Hataweza Kudhibiti. Dowans ni Sawa na Kupigwa Risasi Kichwani.
   
 3. R

  Ribyata 2010 Member

  #3
  Jan 12, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kazi ipo......... patachimbika hapo.!!!! ngoja tuone
   
 4. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  LHCR watakuwa na stand gani kwenye hiyo kesi wanayotarajia kufungua? Halafu The South Law Chembers Advocates sio ya akina Mwakyembe?
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,274
  Likes Received: 19,416
  Trophy Points: 280
  yeleuwiiii!!!!!!!!! Natamani sitta angeendelea kuwa spika, kingewaka sana huko chamwino.
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,274
  Likes Received: 19,416
  Trophy Points: 280
  ribyta ujue mi nilisoma ukrain mwaka 89. Kak ti chornnii
   
 7. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #7
  Jan 12, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  hawa LHRC nawaamini sana. ni the leading NGO kwa masuala yoyote ya kimataifa na hasa ya kisheria hapa nchini mwetu na wanawakilisha mtandao mzima wa wanaharakati wote kwa masuala ya kisheria na pale yanapohusisha wigo wa kimataifa. wana mtandao mkubwa sana nje ya nchi kuliko tunavyoweza kufikiri. ndio wanaoongoza lobbying za kisheria na kisera za wanaharakati wote hapa nchini kwetu na wamefanikiwa almost kila walipolobby. hakika hiyo kesi watashinda, labda ufisadi ushike hatamu huko mahamkamani, lakini kwa hoja zao hizo watashinda. . Yaani JK anaruhusu tunatapeliwa pesa nyingi kiasi hicho waziwazi hivi? nawaombea Mungu awe pamoja nao maana they are undertaking a holy mission, go my heroes, gooo!
   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Jan 12, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mpaka kampuni ya kimaruani Dowans kulipwa ndani ya taifa hili, watu wengi sana watakua wakwishaachishwa kazi na hata pengine wengine wengi zaidi kuombwa kufidia hasara kutoka katika mifuko yao binasi.

  Kwa kifupi, mambo bado ni magumu kupita kiasi na mwenye kuweza kusheherekea kitu hayupo hapa. Ama Dowans will go down the memory lane alone or be accompanied by scores of unfaithful servants.

  Ngoja tumalize maziko na kuhamia hili huku tukipia jaramba taifa zima mswada wa Katiba Mpya Bungeni ambayo nayo huenda ikawa A MAKE OR BREAK kind of affairs incase the current leadership shall not have read very well the reccuring public mood since the October 2010 stolen elections.

  However, our deep prayers are for a smooth sail in the best interest of the general public and with minimal hurdles on the path to full-fledged democratic constitutionalisation without any further delays.
   
 9. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #9
  Jan 12, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Hili sakata kwa kweli tukiwa siriaz hawa dowans hawalipwi!
   
 10. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #10
  Jan 12, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Asante kwa majibu lakini suala lilikuwa wanastand gani ya kisheria kwenye hiyo kesi watakayofungua? Au kama wataalamu wenyewe wanavyosema does LHRC has a locus standi? Kumbuka Dowan is a contractual issue and its people who are privy to the that contract can sue.
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Jan 12, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  aah wapi.. kwa kadiri ya kwamba wakuu wa nchi nchi hii wana maslahi na Dowans, hawajibishwi mtu. NOPE.
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Jan 12, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,669
  Trophy Points: 280
  Nani wa kumgusa Rostam? Alitakiwa awe lupango siku nyingi sana lakini anavyoogopwa kwa kuwa ndiye aliyemuingiza jamaa IKULU utafikiri ana uwezo wa Mungu...hata kutaja jina lake tu wanaogopa!!!!

   
 13. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #13
  Jan 12, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Halafu BAK!!
   
 14. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #14
  Jan 12, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,844
  Likes Received: 11,962
  Trophy Points: 280
  Hatimaye wanaanza kujitokeza Mwakyembe naye ndani ya nyumba patamu hapo, mama Quinine hebu niongezee chai naona sinema ndio inataka kuanza.
   
 15. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #15
  Jan 12, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kweli kwenye hili la dowans, nimeamini kwamba common sense is not so common!
   
 16. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #16
  Jan 12, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Tuanze kuimba "fyeka, fekya pori, tumsake joka hilo"
   
 17. Y

  YE JF-Expert Member

  #17
  Jan 12, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kazi ipo, hata wa kuaminika hajulikani, ngoja tuendelee kubana p¥^bu!
   
 18. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #18
  Jan 12, 2011
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  kwa hiyo ina maana sita anapambana na bosi wake lakini anajidai anapambana ra
  na pinda nae inaonekana kashaambiwa atapelekwa kubadilisha damu mpaka mauti yake akitetea dowans
   
 19. M

  Msharika JF-Expert Member

  #19
  Jan 12, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Lazima kitaeleweka, tukaze buti, Misri walitoka wengi sana kuelekea kaanani , lakini walifika watatu tu, tukazane hata kizazi kijacho kione juhudi zetu. Wale matunda ya nchi yao ya hahadi, Tanzania
   
 20. M

  Membensamba Senior Member

  #20
  Jan 12, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 157
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tanzania amka, umeibiwa vya kutosha. Acha kukumbatia wauaji wako. Serikali ya ccm haina haya. Ni juzi tu imeingia madarakani na sasa inachukua fedha zetu kuilipa (au kujilipa) Dowans huku ikishindwa kuwaajiri waalimu elfu kumi na tano waliomaliza mafunzo na shule hazina waalimu, huku umeme ukipanda na maisha kuendelea kuwa magumu. Haya shime wananchi andikeni mabango twende barabarani kwa mamilioni tuiambie TUMECHOKA TUMECHOKAAAAAAAAAAA!
   
Loading...