Ama Kweli Uungwana Ni Vitendo.
Yani sasa nchi ni kama hata haina Rais.
Na mwenyewe sasa yuko wapi?
Hao mambo ya ZIMBABWE SI YASHAISHA?
VIPI KUHUSU ZILE HOTUBA ZAKE SIJUI NI ZA KILA MWISHO WA MWEZI?
SALVA NAYE MBONA KIMYA?
MBONA HAKUNA ANAYEKAMATWA?
KUNA WANAOSUBIRIWA WAFE?
mimi sikubali!je malipo ambayo walikwisha lipa inakuwaje?na wamegundua mkataba si halali walioingia mkataba batili watachukuliwa hatua gani?kusitisha tu haitoshi lazima tuambiwe kama zile pesa zetu zilizolipwa si kihalali zitarudishwa!
Dr. Iddriss Rashid katoa Press Release LEO ambayo inaonesha kuwa mkataba huo hautokuwepo kufikia August mosi mwaka huu. Najua hii ni habari njema kwa walio wengi na mbaya kwa wachache.
Taarifa zaidi tutafahamishana hapa.
Kwa wanaoangalia TBC wanaweza kuona hii habari muda si mrefu
Kama kawaida, cheap popularity, utavunjaje mkataba uliokwisha? na kama kweli ni batili, kwanini mpaka August 1 na si leo July mosi?
Hii ngoma ndo kwaaaanza inaanza, walicho tusaidia hapa ni kukiri kwamba kweli Dowans na baba yake Richmondi ni wizi mtupu na ubatili. Sasa tunataka tuanzie hapa warudishe kila walicho kwapua kinyume cha sheria, lakini pia wote walio husika kufanikisha wizi huu tuone sheria ikichukua mkondowake ipasavyo!
La sivyo watueleze kama sheria ya wizi ni kwa ajili ya wezi wa miwa tu na mikungu ya ndizi!
kampuni iliyoanzishwa kwa mtaji wa dola 100 ikapewa mkataba wa kuleta umeme kwa nchi ya watu milioni 40? Kwa dola mia moja unaweza kunua hata kompyuta ya ofisi?