Dovutwa wa UPDP, keshanunuliwa?

Wanajanvi, mi sikumuelewa kabisa huyu Dovutwa kujitoa kwenye ligi muda wa mwisho huku serikali imeharibu pesa kwa ajili ya huyu mgombea, kwa kuchapisha picha zake za matangazo na mengine mengi. Kwa nini mtu huyu asishitakiwe?

kuna umuhimu wa kuangalia sheria za uchaguzi kwa watu kama hawa,suala la mgombea binafsi litakapoanza tutashuhudia vituko zaidi!la msingi wahusika kama wapo makini waangalie sheria ya kuwabana hawa wahuni!
 
Wanajanvi, mi sikumuelewa kabisa huyu Dovutwa kujitoa kwenye ligi muda wa mwisho huku serikali imeharibu pesa kwa ajili ya huyu mgombea, kwa kuchapisha picha zake za matangazo na mengine mengi. Kwa nini mtu huyu asishitakiwe?

FIKIRIA VIZURI....>Ndio sirikali ilimgharamia hivyo vifaa na matangazo kama unavyosema...lakini sirikali hiyohiyo ndio iliyochapisha vibaya jina lake kwenye hizo picha za kwenye ballot papers!!.

KWANINI?....>Mpango mzima wanaujua Kivaitu, Dovutwa mwenyewe na. . . Nafikiri utakuwa umeshapata jibu hapo:peep:.

Suala la kushitakiwa ni wote wawili waunganishwe kwenye shitaka hili, halafu watawataja waliowatuma kufanya upuuzi huo. Tena kumbuka Kivaitu alichapisha ballot papers millioni moja za nyongeza eti kwa ajili ya emergency!. Kwanza alisha-tudanganya kuwa zitachapishwa bongo halafu wakapeleka ulaji Uingereza kimya kimya!..

Nasikia Mafisadi wana kamsemo kao kuwa "hela ya wavuja jasho haina hasara".
 
mkuu waweza fafanua kidogo kwani hatujakupata uzuri, unaongelea mambo ya ndani kwelikweli wangu...
 
Wala hakujitoa, mbona alishiriki kutangazwa kwa Mshindi pale Diamond Jubilee???? Dovutwa Msaniii
 
Hii ilifanywa intentionally wanajamvi. NEC walifanya makusudi kukosea jina ili ionekane kuna sababu ya "msingi" ya Dovutwa kujitoa na kutangaza kumuunga mkono kikwete na magazeti (ya ccm na serikali) yaandike kuwa wapinzani wameona JK ni tishio na wameamua kumuunga mkono na hatimaye wananchi wadanganyike. Ni propaganda za kitoto sana tatizo ni pale tunapowaona watu wenye heshima zao nao wakihusishwa katika hili.

Haingii akilini NEC kukosea jina la mgombea wakati fomu wanazo na kabla ya kuprint kuna proof reading ambayo inatakiwa ifanyike. Kama ni kweli jamaa walikosea kiukweli bali NEC ina matatizo makubwa kuliko tunavyofikiria
 
alikula PESA yake saafi si unaona aliyemtaka watu wamchague na kuchafua vyama vingine eeeti vya KIDINI yule BANGI zinamsumbua tuu!
 
Kuna haja hapa ya kutofautisha kati ya wanasiasa wa kweli na watu walioko kwenye siasa( yaani wanasiasa uchwara). Dovutwa ni mwanasiasa uchwara ambaye survival yake inategemea kuwalamba miguu akina JK na mafisadi wenzake !! Dovutwa hana cha kujivunia kwa watoto wake (kama anao) kwa style hii ya maisha ya ukuda na ukuadi!!! Shame on him!!!!!
 
Kabla ya heka heka za uchaguzi Dovutwa nilikuwa simfahamu kabisa, mara ya kwanza kumuona kwenye luninga nilidhani askari wanyama pori kajichanganya anazungumzia uchaguzi. Huyu wala siyo mwanasiasa ni mganga njaa tu, kavuta za NEC kwa ajili ya kampeni, kisha akatoa shukurani kwa kumuunga mkono mshikaji, halafu anaingia mitini hataonekana tena kuzungumzia mustakbari wa Taifa hili. Watu kama hawa ni matokeo ya ufisadi uliokomaa.
 
Uyu jamaa naona alikuwa anataka kukuza CV yake.
Alafu mi najua artwork kabla ya kuwa printed client lazima aaprove na kunakuwa na back and from nyingi tuu mpaka inakuwa printed.
Apo NEC hawawezi kutudanganya it must have been intentional
 
To be honest, sijamuelewa huyu jamaa, eti anawataka viongozi wa dini watoe msimamo wao kuwa ni wanasiasa au wahubiri. Mimi nadhani viongozi wetu wa dini wanayo nafasi kubwa na muhim katika kukosoa na kusahihisha mambo mbalimbali yahusuyo ustawi wa Taifa letu.
 
Kuna maswali mengi kwa aliyoyasema lakini kikubwa tunamwelewa anatafuta kuwalamba miguu CCM wamtupie mfupa. Huyu si ndiye aliyejitoa na kusema anamuunga mkono JK kwenye uchaguzi?

Inategemea anakemea kundi lipi la viongozi wa dini. Kuna kundi linalotetea haki kwa watanzania wote ambao wanaona mambo hayaendi sawa. Kundi la pili ni viongozi wa dini vibaraka wanaotumiwa na viongozi wa serikali kuwahadaa watanzania kuwa serkali ya sasa inaandamwa kwa kuwa JK ni mwislamu. Hili kundi la pili ndilo kundi hatari sana kwa mustakabali umoja na amani ya taifa letu.
Kwa hiyo Kama dovutwa anakemea kundi la pili tunampongeza ila najua ni ngumu sana kuwa anakemea kundi hili la wachochezi wanotumiwa na watawala walioshindwa make alishaonyesha toka mwanzo yuko tayari kuwapigia magoti watawala ili wamrushie mfupa kama wanavofanya hao viongozi wa dini wanaochafua uislamu uonekane kama dini ya kuwaficha waovu machoni pa watu wenye hekima na uzalendo.
 
CHAMA cha UPDP kimekitupia shutuma Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kudai kuwa kelele zinazopigwa na chama hicho kupinga serikali ya Rais Jakaya Kikwete, lakini kimekuwa kikipenyeza maombi ya siri ya kusaidiwa ili kujipanua.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara viwanja vya Bakhresa Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa UPDP, Bw. Fahmi Dovutwa alisema kuwa CHADEMA wamekuwa wakisimama na kumpinga Rais Kikwete, ambapo wamefikia hatua ya kuomba asifike mwaka 2015,

Alisema hata hivyo wamekuwa wakifanya mawasiliano ya siri na Rais Kikwete kuomba msaada wa fedha ili kuimarisha chama mfano msaada wa elimu walioomba katika jimbo linaloongozwa na mbunge wa chama hicho.

"Maombi hayo yamefanya na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bw. Zitto Kabwe kwa niaba ya chama chake, bila shaka ameambiwa na Katibu Mkuu Bw. Wilbrod Slaa mbaye naye ameelekezwa na sekretariet
i. CHADEMA hawakuishia hapo tu kwa Rais Kikwete bali wametembeza bakuli hata kwa wanaowatuhumu kuwa ni mafisadi, wameomba na wamepewa watu hawa wanatuchezea shere,"alisema Bw. Dovutwa.

Alisema kuwa kwa matusi na kebehi zinazofanywa na CHADEMA dhidi ya Rais Kikwete bila aibu mchana, lakini ajabu wamekuwa wakizungumza na CCM usiku,
na kufika mbali zaidi kwamba kwa kitendo hicho ni cha kisaliti na kama kweli CHADEMA kungekuwa na waadilifu, Mwenyekiti wa chama hicho Bw. Freeman Mbowe na Dkt. Slaa wangejiengua.

Aliionya CHADEMA kujifunza kupitia chama cha FORD cha nchini Kenya, ambacho kiligawanyika baada ya kiongozi wa kutokea magazetini asubuhi Ikulu na aliyekuwa Rais wa Kenya Bw. Daniel Moi, na kuonya viongozi hao kuacha usaliti kwa wafuasi wao.

Bw. Dovutwa alitoa jukumu la amani na utulivu wa nchi kuwa mikononi mwa waandishi wa habari, na kuepuka uchochezi wa CHADEMA ambao mnamo miaka ya hamsini, vita vingi vilivyopiganwa vimetokana na mikono ya waandishi wa habari.

Source: Gazeti la Majira, Mei 28, 2011
 
Back
Top Bottom