Double Standards Ugaidi

Double Standards Ugaidi

Mwanaukweli

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2007
Posts
4,789
Reaction score
1,732
Ukiangalia clip hii, huyu Mwana CUF Omar Mussa Makame anaamrisha hadharani Zanzibar waunde vikundi vya kiharamia. Dakika ya 3.40 na kuendelea.

Polisi/Usalama wa Taifa Double standards?
 
Last edited by a moderator:
Huyu alichofanya hapa siyo ugaidi bali na kutumia haki yake ya ki-demokrasia ya kueleza mawazo yake. Tofauti ya huyu na Rwakatare ni kwamba huyu ameyasema mawazo yake hadharani, mbele ya makundi ya watu na kwa kutumia kipaza sauti. Amewataja wanasiasa ambao kwa mtazamo wake anadhania hawana uchungu na nchi yao na amependekeza kwamba kuingia msituni ni moja ya njia za ukombozi, kitu ambacho ni kweli.

Rwakatare amezungumza kwenye usiri, na alikuwa anapanga kumdhuru mtu binafsi ambaye anafanya kazi kama mwandishi wa habari kwa kutumia sumu, dawa za usingizi, malaya wa barabarani na kadhalika.

Mapinduzi na ugaidi ni vitu viwili tofauti.
 
Mkuu nadhani umekurupuka, hukutafakari kabla ya kupost.

Unamaanisha raia akiona amechoshwa na serikali/viongozi anaruhusiwa kuhamasisha KUANZISHA KIKUNDI CHA UHARAMIA?

Ni kwa Zanzibar tu au hata kwa Bara?
 
Dunia nzima mkuu. Democracy ni mfumo mzuri sana kama wananchi wenyewe wameuchagua. Panaposhindikana democracy mapinduzi hufanyika ili kuwezesha democracy kuota. Marekani, South Africa, Kenya, Zanzibar n.k zimekombolewa kimapinduzi.
Kitu ambacho kinawapa wazanzibari uhalali wa kufikiri kimapinduzi ni vitu viwili.

Kwanza: Muungano hauna ridhaa yao. Nadhani wengi watakubali kwamba wazanzibari kama wangekuwa na chaguo la kidemokrasia basi wangechagua kujitawala wenyewe nje ya muungano.

Pili: Historia ya Zanzibar. Wazanzibari ni watu wenye mwamko wa hali ya juu sana kisiasa kuliko waafrika wengine wengi sana. Na hii inachangiwa na wao kutokuwa na tofauti za kikabila na kiimani. Ni rahisi sana kwao kuwa "organised" na kusonga mbele kama taifa. Na ndiyo maana wameweza kufanya mapinduzi na kutwaa uhuru wao kwa kupigana.

Kwahiyo mimi sishangai kuona mzanzibari anafikiri kimapinduzi.
 
Huyu jamaa anafanana na mtuhumiwa wa mauaji ya padri Mushi. Wataalamu tusaidieni ku connect dots... Kwa uchunguzi wangu binafsi wa haraka haraka naona ni yeye, kwani anajitamburisha jina kuwa yeye ni Omari Mussa Makame. Jina linalo machi na mtuhumiwa wa mauaji ya padri Mushi

attachment.php

attachment.php

Source: MICHUZI: MTUHUMIWA WA MAUAJI YA PADRI MUSHI MAHAKAMANI
 
Dunia nzima mkuu. Democracy ni mfumo mzuri sana kama wananchi wenyewe wameuchagua. Panaposhindikana democracy mapinduzi hufanyika ili kuwezesha democracy kuota. Marekani, South Africa, Kenya, Zanzibar n.k zimekombolewa kimapinduzi.
Kitu ambacho kinawapa wazanzibari uhalali wa kufikiri kimapinduzi ni vitu viwili.

Kwanza: Muungano hauna ridhaa yao. Nadhani wengi watakubali kwamba wazanzibari kama wangekuwa na chaguo la kidemokrasia basi wangechagua kujitawala wenyewe nje ya muungano.

Pili: Historia ya Zanzibar. Wazanzibari ni watu wenye mwamko wa hali ya juu sana kisiasa kuliko waafrika wengine wengi sana. Na hii inachangiwa na wao kutokuwa na tofauti za kikabila na kiimani. Ni rahisi sana kwao kuwa "organised" na kusonga mbele kama taifa. Na ndiyo maana wameweza kufanya mapinduzi na kutwaa uhuru wao kwa kupigana.

Kwahiyo mimi sishangai kuona mzanzibari anafikiri kimapinduzi.
Uharamia/ugaidi na mapinduzi ni dhana mbili tofauti kabisa.
 
Hii ilikuwa April 2012.

Amekamatwa lini? na kwa kosa gani? Hili ni sawa?

kama hata hujui kakamatwa kwa kosa hustahili kujenga hoja yoyote make hujui mambo yanavyokwenda.
 
Dunia nzima mkuu. Democracy ni mfumo mzuri sana kama wananchi wenyewe wameuchagua. Panaposhindikana democracy mapinduzi hufanyika ili kuwezesha democracy kuota. Marekani, South Africa, Kenya, Zanzibar n.k zimekombolewa kimapinduzi.
Kitu ambacho kinawapa wazanzibari uhalali wa kufikiri kimapinduzi ni vitu viwili.

Kwanza: Muungano hauna ridhaa yao. Nadhani wengi watakubali kwamba wazanzibari kama wangekuwa na chaguo la kidemokrasia basi wangechagua kujitawala wenyewe nje ya muungano.

Pili: Historia ya Zanzibar. Wazanzibari ni watu wenye mwamko wa hali ya juu sana kisiasa kuliko waafrika wengine wengi sana. Na hii inachangiwa na wao kutokuwa na tofauti za kikabila na kiimani. Ni rahisi sana kwao kuwa "organised" na kusonga mbele kama taifa. Na ndiyo maana wameweza kufanya mapinduzi na kutwaa uhuru wao kwa kupigana.

Kwahiyo mimi sishangai kuona mzanzibari anafikiri kimapinduzi.
Kuna wakati ni vizuri kutokuandika chochote, huu ni zaidi ya upuuzi, kuanzisha vikundi vya uharamia unasema ni uana mapinduzi! Na unaona njia sahihi, kwa hiyo unaamini kama ndiye aliyemuua padri basi yuko sahihi, maana aliongea hadharani, Ushabiki ukizidi unatutoa akili..
 
Lugha ya mkosa hoja ni hiyo hapo kwenye red. Nimetoa maoni yangu ya awali kwa mujibu wa video ambayo iliwekwa kuhusu huyu jamaa akihamasisha mapinduzi katka nchi yake anayoipenda. Kwenye ile video hakuna neno wala picha ya padri yoyote, na nilitegemea maoni yatokane na ile video.
Kwanza kabisa mimi sijui uhusiano wa huyu mtu na kifo cha padri mushi, na siwezi kukubali kuuawa kwa mtu yeyote yule awe padri mushi au sheikh ilunga. Kumtandika mtu risasi ni ugaidi. Alichokisema huyu brazamen kwenye ile video yake ni uanamapinduzi.
Naomba nikupe somo dogo tuu.
1. Serikali ya uingereza ilimwita general Washington gaidi wakati Marekani inapigania uhuru wake dhidi ya utawala wa uingereza.

2. Uingereza na marekani walimwita Mandela gaidi kwa sababu hizohizo.

3. Jomo Kenyatta na wakenya wenzake (sipendi kutumia neno mau mau) waliitwa magaidi wakati wakipigania uhuru wao.

Sasa hili neno gaidi ni neno "subjective", na gaidi wako wewe anaweza kuwa mpigania uhuru wa mtu mwingine.
Kwa mujibu wa hiyo video hapo juu, hakuna ugaidi hapo, bali ni uanamapinduzi.

Lakini kwa kuwa tuna elimu za viwango tofauti, kwa hiyo umuhimu wa "evidence" nao pia ni tofauti kutoka mtu mmoja mpaka mtu mwingine.
 
Back
Top Bottom