“Mtazame mwanaume kwa kuangalia viatu vyake, mkanda wake, saa yake n.k…”
Sawa, tunakubaliana mwanaume anatathminiwa kwa muonekano wake?
LAKINI…
Mwanaume akisema:
“Mavazi yako yanaonyesha tabia au heshima yako…”
Ghafla anaitwa mshamba, controlling, au mwenye wivu zaidi
Kwa nini sheria ibadilike ghafla?
Siku hizi kuna wanawake wanavaa nguo zinabana hadi maumbo yote yanaonekana wazi kabisa. Wengine wanavaa wazi kiasi kwamba hakuna kilichofichika ile mistari ya chupi siku hizi ni jambo la kawaida kuonekana. Lakini bado atasimama kifua mbele kusema: “Mimi sijiuzi.”
Unataka kuheshimiwa vipi wakati unajitangaza kwa mwili kuliko utu wako?
Heshima haiji kwa maneno, inakuja kwa namna unavyojibeba. Na mavazi ni sehemu ya hiyo lugha. Usitake kupimwa kwa utu wako wakati presentation yako inaongea kitu tofauti. Kama mwanaume anapimwa kwa viatu vyake, basi mwanamke naye atapimwa kwa anachochagua kuvaa.
Hii dunia haisikilizi unachosema inaangalia unachokionyesha. Kubali au kataa — lakini ukweli utabaki kuwa ukweli.
Ukituvalia mapambo ya ndani hadharani tutaona kuna biashara unaitangaza.