Dotto: Kama kweli watanzania wanaumia na wizi huu wa mali za umma tuanze shinikizo la haya yafuatayo

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,509
2,000
Anaaandika Mtangazaji wa Startv Dotto Bulendu .
Kama kweli watanzania wanaumia na wizi huu wa mali za umma tuanze shinikizo la haya yafuatayo!.

1.Tuilazimishe serikali itake isitake Rasimu ya Warioba irejeshwe na kupitishwa ili kuondoa kinga kwa maraisi wastaafu na wafike mbele ya vyombo vya sheria na wawaambie watanzania kwa nini haya yalifanyika chini yao na sheria ichukue mkondo wake!.

2.Wale wote waliohusika kuichakachua Rasimu Warioba waombe radhi na wachukuliwe hatua za kinidhamu!.

3.Waliokuwemo kwenye "cabinet"kuanzia cabinet(baraza la mawaziri) la 1990-1995,ambapo walipitisha mkataba mmoja.1995-2005,waliopitisha mikataba ya hovyo mitano na hawa wa 2005-2015,waliopotisha mkataba mmoja wote washtakiwe kwa kuiingizia nchi hasara,masuala ya nchi hufanyika kwa uwajibikaji wa pamoja(collective responsibility)na siyo individual responsibility!.

4.Wabunge wote waliopiga kura ya ndiyo kupitisha sheria ya kodi na ile ya uwekezaji ya mwaka 1997,pamoja na sheria ya madini ya mwaka 2010,wafikishwe mahakamani kwa kuliingizia taifa hasara!.

5.Wabunge wote waliopitisha hoja ya kumfukuza Zitto Kabwe bungeni mwaka 2007 baada ya kumtuhumu waziri Karamagi kuwa alikula rushwa kwenye mkataba kati ya serikali na Barrick Gold wote wafikishwe mahakamani kwa kutetea mkataba wa hovyo na kuipa ruhusa kampuni ambayo haijasajiriwa nchini kuchimba madini na hivyo kulisababishia taifa hasara!.

6.Wale wote waliounda timu ya wataalam wa kulishauri baraza la mawaziri kuhusu mikataba ya madini kuanzia mwaka 1995 mpaka sasa,wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria ili wajibu kama huu ndiyo ulikuwa ushauri wao!.

7.Wale wote waliokuwa wanaopinga sheria hizi na mikataba kuwekwa wazi,watajwe hadharani na kuwaomba radhi watanzania!.

8.Maspika wote walioongoza utungwaji wa sheria hizi nao wafikishwe mbele ya vyombo ya sheria kwa tuhuma za kuhujumu uchumi!.

9.Waandishi wote waliokuwa wanaandika habari ama kutengeneza vipindi vya kutetea wawekezaji nao waombe radhi kwa kutetea wizi huu!.

10.Yote katika yote kama watanzania hatutaanzisha vuguvugu la kuitaka Rasimu ya Warioba tutakuwa hatuvitendei haki vizazi vijavyo na tutakuwa tunapoteza muda!.

11.Usalama wa taifa watuambie je walikuwa wanatoa taarifa kwenye mamlaka juu ya wizi huu?kama hapana nao washughulikiwe!.

11.CCM ya Mkapa na Kikwete iseme wazi kwa nini iliacha kuisimamia serikali na kuacha wizi huu uliolipotezea taifa Trilioni karibu 180?kwa ni waliacha kuisimamia serikali kama alivyowahi himiza Katibu mkuu Kinana?.
 
Prognosticator

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,128

Kwa # 11 Dotto atakuwa anawaonea tu kwani ninachojua kwa mujibu kwa Utendaji wao wa Kazi hakuna jambo ambalo sisi Watu wa kawaida tu tunaliona halafu Wao ambao ndiyo Wataalam kabisa na Wamebobea Kiujasusi wasilione. Ninachojua tu ni kwamba kuna mambo mengi sana hao Watu waliotajwa na Dotto wamewasilisha kwa Viongozi waliokuwepo hasa hasa wa Awamu ya Nne ( 4 ) ila tatizo kubwa Kiongozi huyo alikuwa akizipuuzia na kumuamini sana DG Mstaafu na kuwapuuza wengine ambao kimsingi ndiyo walikuwa wakifanya Kazi ya Kiuzalendo kabisa kwa nchi hii.
 
pakaywatek

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
4,133
2,000
Usiwaamini miccm ni kama kumbikumbi wanaenda na upepo wa mwenyekiti wao, hata leo mwenyekiti wao akibadili upepo na kuanza kutangaza uuzwaji wa ikulu hakuna atakaepinga, ni kama bendera.
Hii mikataba mwenyekiti wao wa enzi hizo ndiye aliyetia saini wakashangilia mpaka wakawafukuza na wapinzani bungeni, leo wamegeuka tena wanakosoa, huyu nae akitoka wanasubiri kumfuata atakae kuja, hawana wanachokipigania ni matumbo yao tu.
 
olyanu

JF-Expert Member
May 30, 2017
1,833
2,000
Wazo lako zuri sana lakini let me tell you mpendwa hilo halitawezekana mpk Yesu atakaporudi. Na ukilikazania sana utaukuta mwili wako uliooza kwenye pori la Geita. Ukibisha nenda kamuulize Mr two oclock kama mnaona na huko kwa Bwana God. Hawa jamaa hawawezekani ila kwa nguvu za maombi tu. Tum lilies Mungu aingilie mwenyewe basi
 
Jile79

JF-Expert Member
May 28, 2009
17,495
2,000
Ccm akiwemo magufuli ni wapumbavu sana kwa sababu haya yote ni sababu yao wote kwa umoja wao dhidi ya rasilimali za watz. Alafu wanaunda mitume kwa kuwapa ulaji wa bure watu wkt walipitisha haya yote kwa mbwembwe huku wakiwatukana watz matusi ya nguoni.
Shame on them ccm + their corrupt leaders
 
Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,509
2,000
Kwa # 11 Dotto atakuwa anawaonea tu kwani ninachojua kwa mujibu kwa Utendaji wao wa Kazi hakuna jambo ambalo sisi Watu wa kawaida tu tunaliona halafu Wao ambao ndiyo Wataalam kabisa na Wamebobea Kiujasusi wasilione. Ninachojua tu ni kwamba kuna mambo mengi sana hao Watu waliotajwa na Dotto wamewasilisha kwa Viongozi waliokuwepo hasa hasa wa Awamu ya Nne ( 4 ) ila tatizo kubwa Kiongozi huyo alikuwa akizipuuzia na kumuamini sana DG Mstaafu na kuwapuuza wengine ambao kimsingi ndiyo walikuwa wakifanya Kazi ya Kiuzalendo kabisa kwa nchi hii.
Tuilazimishe serikali itake isitake Rasimu ya Warioba irejeshwe na kupitishwa ili kuondoa kinga kwa maraisi wastaafu na wafike mbele ya vyombo vya sheria na wawaambie watanzania kwa nini haya yalifanyika chini yao na sheria ichukue mkondo wake!.
 
crocodile

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,183
2,000
Badala ya wananchi kuzuzuka kama mazuzu walitakiwa waingie barabarani kushinikiza ccm aidha waombe radhi au kibwage manyanga..!!
Ukisikia mtu anaamini ujinga wa kuingia barabarani au sijui Ukuta sijui..by 95% plus hana shughuli za kufanya.
 
mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,553
2,000
Hongera sana Dotto Bulembo kwa nondo zako safi na nzito ila, pole saana. Maneno yako ni kama kuupaka tu upepo rangi yeupe. Wapo wanaoyasoma na kuona kuwa ni upuuzi mtupu.
We ni nani utoe ushauri?? Je, ni miongoni mwa washauri waliokubalika? CCM ndio iliyotufikisha hapa tulipo
 
Ngushi

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
9,080
2,000
Haya ukiwaambia ccm wanakuwa wakali!
Kama kweli magufuli ana Nina ya dhati alete katiba ya warioba!
Sio kuhuzunika tu kwenye maiki, hilo halitatusaidia!
Maajabu zaidi hata kinana nae inaonekana anasikitika wakati alikuwepo kipindi hivyo vyote!
Huu unafiki ni wakiwango cha lami
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom