Dotto Bulendu : Umuhimu wa Magazeti ya Tanzania Daima, Mwanahalisi na Mawio

wilcoxon

JF-Expert Member
Jun 25, 2017
996
1,000
Ukisoma
nadharia,aina na kazi za vyombo vya habari,kama
magazeti ya Tanzania Daima,Mwanahalisi,na Mawio yangekuwepo hili suala la Lowasa kwenda Ikulu kuzungumza na Mh Rais John Magufuli lingekuwa na uzania sawa jinsi ya kulichakata!

Kukosekana kwa vyombo vya habari ambavyo vilijipambanua kuikosoa zaidi serikali ni Ombwe kwenye habari tunazowapa wananchi wetu!

Kuna kipindi tunahitaji kuwa na vyombo ambavyo vitahakikisha taswira ya serikali inakuwa chanya kila siku,pia tuna kuwa na vyombo vya habari ambayo kazi yao ni kumulika madhaifu ama makosa ya serikali na mwisho tunakuwa na vyombo vyenye msimamo wa kati!

Bado Tanzania inayahitaji sana magazeti ya Tanzania Daima,Mawio na Mwanahalisi,hebu tazama jinsi magazeti kama Tazama Tanzania yanavyoshughulika na vyama vya upinzani hususani Chadema,gazeti hili limejipambanua kusaka udhaifu wa vyama vya upinzani,lipo gazeti lingine Freeman Mbowe hajawahi pata nafasi chanya,kwa mtazamo wangu magazeti ya namna hii ni muhimu sana kikubwa yaandike ukweli!.
 

wilcoxon

JF-Expert Member
Jun 25, 2017
996
1,000
Moods marekebisho hapo kwenye Tanzania sauna inapaswa kuwa Tanzania Daima
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom