GANG MO
JF-Expert Member
- Dec 6, 2016
- 2,092
- 2,210
Rais Magufuli kaunda tume ya kuchunguza mchango wa sekta ya madini nchini Tanzania,anataka kuona kama kuna ukweli kwenye hii biashara ya madini!.
Rais Magufuli tunakupongeza kwa kuonesha nia ya kuondosha uzania usio sawa kwenye biashara hii ya madini kati yetu na wawekezaji katika sekta hii ya madini nchini!.
Binafsi siwezi kuipongeza serikali kwa kuunda tume ama kwa maneno kutoka kwenye kinywa cha Mh Rais juu ya biashara hii ya madini!.
Suala la tume si jipya,kila serikali inapoingia imekuwa inakuja na maneno makali ya kuonesha kukerwa na biashara isiyo na uzania kwenye sekta ya madini!.
Serikali ya awamu ya tatu ilitoka na ripoti nzuri ya kamati iliyokuwa chini ya Jaji Mstaafu Mark Bomani,ripoti hii imeeleza kinagaubaga juu ya biashara hii ya madini,imeonesha jinsi tunavyoibiwa na nini cha kufanya!.
Serikali ya awamu ya nne nayo ilikuja na kamati yake iliyoitwa kamati ya Masha,nasikia katika ripoti nzuri zenye kuainisha ukweli kuhusu sekta ya madini na hii ni miongoni mwao,Masha na timu yake walipo maliza kazi yao,walikabidhi serikalini na haijawahi somwa,imewekwa sijui wapi!.
Nani anakumbuka hotuba ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete trh 5.2.2006 mkoani Shinyanga,Rais Kikwete alitoa hotuba ya kusisimua akionesha kukerwa na uwekezaji kwenye sekta ya madini na kuahidi kupitia upya mikataba yote ili watanzania wanifaike na biashara hii!.
Mwaka 2009 tukatunga sera ya madini na baadae mwaka 2010 sheria yake ikatungwa,hizi nyaraka mbili zilizotungwa na wataalam kutoka serikalini ndiyo zinazotoa ruhusa huo mchanga kwenda nje,hili limerihusiwa kisera,hawa watu hawafanyi biashara kinyume na sheria wala sera!.
TEIT wamekuwa wanatoa taarifa juu ya mapato kutoka sekta hii ya madini,kumekuwa na ubabaishaji mkubwa,leo hesabi zilizopo TRA,TMAA,na wizarani kihusu mchango wa wawekezaji kwenye GDP,hazifanani kabisa,haya mambo hayafanyiki kwa siri!.
Tanzania tumekuwa tunafanya mambo unabaki kujiuliza hivi tumekutwa na nini?Tulianza kuvuna gesi bila uwepo wa sera na sheria ya gesi,hili ni jambo la ajabu kabisa!.
Hawa wawekezaji hawa,wamepewa kibuti na wataalam wetu kutuibia,nakumbuka mwekezaji kutoka Nyamongo alichimba madini bila kuilipa halmashauri ya Tarime mapato kwa muda mrefu,wameanza kulipa miaka mitatu kama iliyopita!
Nakumbuka nilikuwepo kwenye mkutano wa kuarifu Acacia kuanza kulipa mapato,Mkuu wa Acacia akasema walikuwa hawalipi kwa sababu halmashauri ilikuwa haijatunga sheria inayosimamia ulipaji wa mapato!.
Nikajiuliza hivi hii nchi haina wataalam,haina watu wenye maoni?,nakumbuka wakati wa uhai wake Marehemu Chacha Wangwe alilazikisha mgodi kulipa karo za wanafunzi wote wa jimboni kwake!.
Marehemu Wangwe alifanikiwa,baadhi ya vijana walikuwa wanapata ada mpaka za vyuo vikuu kutoka mgodini,hii hakiwa sehemu ya sera kutoka serikalini,ilikuwa
ni nguvu ya Marehemu Wangwe na wenzake!.
Kuna ripoti nyingine iliyopewa jina la "The gorden opportunity,nayo imeainisha wizi wote kwenye sekta ya madini nchini Tanzania,kuna wizi mkubwa kwenye mapato!wawekezaji hawa wamekuwa hawatoi taarifa za ukweli kwa serikali!.
Wawekezaji hawa,wameua watu kwa Risasi,wamewafanya watu walemavu,huko Nyamongo watu walibabuka ngozi,malipo ya fidia yamefanyika kinyonyaji!.
Unajiuliza hivi tunaunda kamati za kazi gani?kweli biashara hii inafanyika muda wote huu,idara ya usalama wa Taifa (TISS)haijui chochote,hivi ninkweli TISS hawafahamu chochote kuhusu biashara hii?
Ni matarajio yangu Rais Magufuli hatakuwa kama watangulizi wake,waliounda kamati na kuishia kuziweka ripoti kabatini!.
Binafsi nina imani kubwa Rais Magufuli atamaliza huu unyonge wa nchi yetu mbeke ya wawekezaji,mwaka mmoja nilifuatana na viongozi wa dini waliokuwa wanakwenda kutembelea na kujionea hali ya uwekezaji,nilisikitishwa na kilichowakuta viongozi hao,maaskofu,mashehe walijibiwa kwa dharau na hata kuzuiliwa kuongia mgodini!.
Leo kuna wafanyakazi wa mgodini wanahangaika huko Kahama,afya zao ni dhaifu kutokana na kazi za mgodini!.
Mishahara kati ta wazawa na wageni ni mbingu na ardhi huko migodini!.