Dotto Bulendu amchambua Paul Makonda

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
121,947
95,237
Kuna kipindi huwa najiiliza maswali mengi sana Na miongoni ya maswali hayo.

1.Hivi Watu wanapokuwa Kwenye nyumba za kuabudu (Makanisani Na misikitini) huwa wanakwenda Kwa ajili ya kujionesha ama wanamaanisha?

Kwa nini najiuliza

Leo asubuhi nimeamka na kukutana na Vidio ya Kiongozi tena wa Serikali ambaye mara kwa mara huwa namuona anakaribishwa mpaka kwenye madhabahu ya kanisa na kupewa nafasi ya kuhubiri ,leo anaamka na kuandaa mkusanyiko halafu anaanza kumkebehi Mzazi wa mtu kuwa anashukuru sana huyo mtu mwanae kupatwa Ugonjwa wa Corona.Hivi kweli dini zinatufundisha kuombeana watu mabaya?kufurahi wengine wanapopata shida na kuteseka ?

2.Swali la pili,huwa najiuliza hivi Shuleni na Vyuoni yanayofundishwa ndiyo yanayofanyika huku nje?maana nakumbuka nilipokuwa Chuo Kikuu,nilisoma kidogo Kwa muhula mmoja somo ya Uongozi.

Nilifundishwa kuwa unapochaguliwa kuwa Kiongozi basi fahamu miongoni mwa Kazi zako ni Kuwa Mfariji Mkuu.

Sasa leo nimeamka asubuhi na kukutana na vidio ya Kiongozi mkuu wa ngazi ya Mkoa,anatangaza kwa kukebehi huku akifurahia moja ya wananchi ndani ya Mkoa wake kukutwa Na maambukizi ya Virusi vya Corona,kisa Baba wa huyo mtoto wanatofautiana Vyama vya Siasa.

Najiuliza Prof aliyenifundisha kuwa unapokuwa Kiongozi wewe ni mfariji mkuu,alikuwa ananiongopea?mbona baadhi ya Viongozi(Kama alivyofanya mkuu wa mkoa) ameshindwa kusimama Kwenye nafasi ya Mfariji mkuu na badala yake kaamua kuianza siku Kwa kwenda Kwenye mikusanyiko na kumtangaza mwanafamilia wa ndani ya Mkoa kuwa anaugonjwa wa Corona huku alienda mbali zaidi Kwa kusema anamshukuru Mungu familia hiyo kupatwa na janga la Corona?

Mungu Ibariki Tanzania

In God we Trust
 
Ndio maana huwa nasema humu ni aheri wapagani kuliko sisi tunaojidai kumjua Mungu kumbe wengi tu ni wanafiki tu.

Yanayoendelea katika nchi hii na jinsi baadhi yetu tunavyoyachukulia, unaweza kuona hata kwenda kanisani au msikitini ni kupoteza muda tu(tunafanya dhambi kwa mazoe alafu tunasali kama fashion).

Watu wanafanyiwa kila aina ya uovu, dhuluma, uonevu, mateso n.k, lakini wanaokemea ni wachache huku wengine wakiona hayawahusu halafu Jumapili na Ijumaa watu hao wanamiminika kwenye nyumba za ibada eti kwenda kusali!

Yaani watu hawaguswi na huu uovu kisa tu anaetendewa si ndugu yake wala jamaa yake na wewe unaeguswa watakwambia achana na mambo ya siasa..

Pathetic!!
 
IMG_20200324_213457_000.jpg
 
Malipo ni hapa Hapa duniani ili walimwengu wakuone na wajifunze
Hakuna anayemwombea mwingine mabaya yeye abaki salama! Kuna mzazi mmoja alikuwa anamcheka mtoto wa mzazi mwingine kuwa "kicha chake kimepinda" na ndivyo ilivyokuwa. Mungu si Athmani, huyo mzazi naye alipata ujauzito na yeye akajifungua mtoto ambaye kichwa chake kilikuwa kimepinda pia.

In God we Trust
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom