Samahani nimeajiriwa na kampuni ya utalii hapa Arusha yenye magari kama 500 hivi. airuhusiwi kufanyia kazi gari isiyo ya kampuni hata la kwangu nafanyia nje. Ila kwa ushauri uwe na uhakika nitautoa bure.Mkuu kama una garage ya uhakika nikuletee VW yangu nipi mbeya huku kumwaga oil tu mafundi wanaharibu waneshaniharibia sana hii gari next month mwishoni nakuja nayo mjini kuitengeneza kama upi fit nikutafute matatizo mengi ni umeme lakini
asante mkuukaribu
- Zima gari lako unapopaki hata kama unaingia na kutoka. Utaokoa mafuta yako
- Warmup unapowasha gari asubuhi ni upotevu wa mafuta, anza kuendesha tu taratibu (unless upo Makete 🙂)
- Ukiwa kwenye foleni ndefu zima gari pamoja na taa uache parking lights tu
- Epuka breki za ghafula, unamaliza mafuta, na breki zenyewe
- Kama hakuna joto wala vumbi, kiyoyozi cha nini? :shock:
Wanasiasa wanafiki sana.
Huwa hawaoni kabisa positove side ya JF.
Imagine watu wangapi wamefaidika na hii thread!
Big up Chemwali
1. Hata kama uko makete hakikisha walau mara moja kila wiki unawasha AC kwa muda usiopungua nusu saa kusudi AC ya gari yako idumu.
2. Kila baada ya kupita kwenye mazingira yenye vumbi vumbi kagua cabin filter, ibadilishe ikibidi ili AC yako iendelee kukupa hewa safi
3. Epuka safari za mwendo mdogo (mf below 60km/hr) kwa muda mrefu. Kama kuna ulazima wa kusafiri kwa spidi ndogo kila mara (kwa sababu ya foleni au ubovu wa barabara) hakikisha unapata safari ya mwendo kasi (angalau 80km/hr) kila wiki au baada ya wiki mbili kuiweka gari katika hali nzuri
4. Usisahau betri za maji zinahitaji ku-refill mara kwa mara ili betri yako idumu
5.Taa ya oil ikiwaka wakati wowote gari ikiwa inatembea hakikisha unapunguza mwendo haraka na kusimama ( haijalishi kama uko katikati ya serengeti). Ni kwa faida yako na gari yako.
6. Taa yoyote (hasa usiyoielewa) ikiendelea kuwaka kwenye dashboard (hata kama gari inaweza kutembea) waone wataalamu mara moja.
7. ....mengine itabidi tuweke tozo kidogo...ha ha ha...watu wanaweza kugraduate humuhumu bure..lol
Ni masuala ya lubrication kwenye moving parts, ni darasa refu kidogo lkn yatosha tu kusema kwamba hayo uliyoeleza ni sahihi (ukiacha la ulaji wa mafuta) lakini pia kuna pros and cons kwa kila jambo. Mengine not that much obvious. Pokea tu huo ushauri kama unataka engine, wheel-bearings etc zidumuhebu tufafanulie kwanini niepuke kuendesha 60km/hr....kwa sabubu nijuavyo mimi 60km/h ni nzuri kwa ulaji wa mafuta na usalama wako na watumiaji wengine wa barabara(speed limit sehemu nyingi urban ni btn 40-60km/hr
Samahani nimeajiriwa na kampuni ya utalii hapa Arusha yenye magari kama 500 hivi. airuhusiwi kufanyia kazi gari isiyo ya kampuni hata la kwangu nafanyia nje. Ila kwa ushauri uwe na uhakika nitautoa bure.
okay thanks mkuu hata kwa ushauri bado utakuwa na msaada sana kwangu
Haahahahahhaaa......usiweke chini ya mti....kinyesi cha kunguru kinaua gear box.
JF ina vitu vingi sana, kwa sababu inakutanisha watu wa fani anuwai. Ndio faida yenyewe ya mtandao huu.
karibu sana