Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,570
- 19,443
President Jakaya Kikwete has called upon donors to continue providing assistance to Tanzania, saying that the billions of shillings swindled from the Bank of Tanzania (BoT) were not from donors.
Kwa maoni yangu mafupi, nadhani Rais K. I. Kwete anadanganya watu kuhusiana na wizi huu. Nasema hivyo kwa sababu kama nikimpa mwanangu msaada wa shilingi 500 kwa ajili ya matumizi ya shule halafu nikamkuta anafuja hela kwa kulewa kwenye mabaa, sitakubaliana na jibu kuwa fedha anazolewea siyo nilizompa, ila eti analewea fedha zake mwenyewe alizopata kwingineko kwa hiyo nisiwe na wasi wasi niendelee kumpa msaada tu. Sijui kama kuna mzazi yoyote mwingine anayeweza kukubalina na jibu la namna hiyo.