Donor funds not embezzled at BoT - JK

President Jakaya Kikwete has called upon donors to continue providing assistance to Tanzania, saying that the billions of shillings swindled from the Bank of Tanzania (BoT) were not from donors.

Kwa maoni yangu mafupi, nadhani Rais K. I. Kwete anadanganya watu kuhusiana na wizi huu. Nasema hivyo kwa sababu kama nikimpa mwanangu msaada wa shilingi 500 kwa ajili ya matumizi ya shule halafu nikamkuta anafuja hela kwa kulewa kwenye mabaa, sitakubaliana na jibu kuwa fedha anazolewea siyo nilizompa, ila eti analewea fedha zake mwenyewe alizopata kwingineko kwa hiyo nisiwe na wasi wasi niendelee kumpa msaada tu. Sijui kama kuna mzazi yoyote mwingine anayeweza kukubalina na jibu la namna hiyo.
 
Nimeenda kwenye website ya IMF kutafuta data za nchi yetu. Hii statement ya IMF ni ya January mwaka huu (2008) na hii hapa chini ni statement ya deni letu kwa world bank. Ninaatach na kama una muda sio vibaya uifungue uisome.

Statement of Loans, Credits, and Grants (As of April 30, 2007; U.S. dollars) Source: World Bank Group

Original Principal $6,639,899,793
Cancellations $241,197,606
Disbursed $5,232,137,342
Undisbursed $1,391,028,338
Repaid $826,193,792
Due $1,160,921,834
Exchange Adjustment $0
Borrower Obligation $1,160,921,834

Hivi unadaiwa dola bilioni 1.6 huku bado unasafiri kuomba misaada kila kukicha, halafu unasema kuwa hela zilizoibiwa sio za donors...WHAT A JOKE!
 
Huyu JK anafanya kamchezo ka kukalukuleti risk. Anajua akisema feza n za wafadhili, likely kutawaka moto ambao anaweza ashindwe kuuzima, lakini watanzania hawatamfanya kitu!, hii si dharau kwa wapiga kura eeh??????????
 
Susuviri,
Mkuu maneno mazito sana hayo!... yaani Mh. JK kweli amefikia kusema fedha zilizoibiwa Benki kuu ni mali ya Tanzania bila hata aibu?....Hivi kweli mtu anaweza iba nyumbani kwake ashindwe kwa jirani hasa pale budget yetu yenyewe inategemea misaada kwa kiasi.
Haya hiyo benki kuu yenyewe ambayo sasa hivi nasikia tunagonga kitu kama 500/m Usd imejengwa kwa fedha gani?...
Mh. JK toka enzi za Mwinyi, kina Kweka walikuwa wakizivuta sana hizi za misaada tena ndio rahisi zaidi kulingana na misheni town wa benki yako kuu, leo unatupa lugha gani ama ndio tufunike kombe mwana haramu apite (huyo irish prime Minister).....
Kifupi wambie unachotaka kuwambia lakini sisi Watanzania tumechoka....Wadanganyika wameanza kusimamisha bendera mpya....safari hii kuna uwezekano mkubwa rangi nyekundu ikijiongeza kama hutakuwa makini kwani yaliyotokea Kenya sii ya kuombea lakini tusije sema haiwezekani!...Mungu apitishie mbali, uyaone haya mapema.
 
"He said the 133bn/- that was misappropriated at the Central Bank belonged to the Tanzanian government. The President promised to recover the money to the last cent once investigations into the scam have been completed."

Yale yale ya radar, muungwana si aliomba waingereza(BAE) waturudishie change

The so called MUUNGWANA anajua anachofanya, nacho ni kutulamba sisi na hao Donors visogo ila naamini mbio hizi zitaishia ukingoni tu siku moja! hopefully soon, I can't wait.
 
Sijapata kuona kuona Rais anayetia aibu na ambaye hafai kuongoza chochote kama Kikwete. Huyu jamaa nadhani ni mmoja kati ya Marais wajinga kabisa duniani na nina wasiwasi hata na elimu yake kama aliipata kihalali. He is beyond stupidity.

Told you, ndio maana alipotoa speech BU (USA) aliulizwa swali dogo sana na akashindwa kujibu "yaani nilificha uso kwa kiganja' basi Prof. aliyemuuliza akasema 'I bet watz wamemchagua huyu kwa uhandsome na wala sio kitu kingine na bila shaka alipata kura nyingi kutoka kwa akina mama" what a shame maneno kama hayo kutoka kwa stranger' Haya kalaghabaho, watz tujaze na kushindilia I can't imagine to have him for 10 yrs! Ohhhh am tired already!
 
Hii statement ya JK ime- summarize kila kitu kuhusu uwezo wa kufikiri wa kiongozi wetu. Unajua kabla ya kumdanganya mtu ni lazima ujue ya kuwa huyo mtu unayetaka kumdanganyaana ana akili pia , kama wengine walivyosema kama mnaweza kula hela za walipa kodi wenu , vipi kuhusu hela za wafadhili ?
 
Back
Top Bottom